Hi Ankal,
Habari ya majukumu ya kila siku,
Habari ya majukumu ya kila siku,
Nina jambo limenisikitisha sana hapa
beach ya oysterbay. Eti kupaki gari inabidi ulipe shs. 1000 Eti
wanadai wametumwa na serikali za mitaa.
beach ya oysterbay. Eti kupaki gari inabidi ulipe shs. 1000 Eti
wanadai wametumwa na serikali za mitaa.
Kweli kuna haki hapo? Ukiuliza
hela wanafanyia niñi
hela wanafanyia niñi
Hupati jibu...Kulikoni??
Mdau Coco Beach


Mbona hiyo ni kidogo,ili kupunguza msongomano wa magari kwenye sehemu nyeti inabidi serikali itoze siyo hiyo tu 1000 unayozungumzia, kwa mawazo yangu labda Sh. 5000 ndiyo ingestahili.
ReplyDeleteHiyo ni njia mojawapo ya serikali kujiongezea mapato yake na papo hapo kupunguza msongamano usiokuwa wa lazima. Maeneo yote katikati ya miji parking lazima iwe ya kulipia kwa nchi nzima. Hii pia itasaidia katika kupunguza air polution inayotokana na fuel combustion.
Tusipende sana kulalamika. Sasa ndugu yangu unataka serikali za mitaa zijiendeshe vipi.
ReplyDeleteOne thousand shillings aka elfu moja, what is that? Mheshimiwa una gari, uwezo wa kulipia unao. Hebu fikiria kwanza uhalibifu unaoufanya kwa kupeleka gari yako beach.
Halafu, elfu moja ni kiasi kidogo sana kubadilisha beach kwa viwango tunavyovitaka.
nauliza hivi! hii blog ya jamii mwisho wake ni Chumbe? naona haitwambii kitu kuhusu yanayoendelea Zanzibar juu ya mabadiliko ya kisiasa na mustakbali mpya wa kishuna chetu Zanzibar. au hamjayapenda haya?
ReplyDeletenauliza tu.
hamad
cph
Ndugu yangu michuzi unatakiwa uwe makini na baadhi ya vitu unavyoweka kwenye blogu yako kama hii hapa juu ameweka mwenyewe au huyo mtu uliyemweka awe anaweka taarifa kwenye blogu leo hajatulia ?
ReplyDeleteCorrupt leadership=corrupt society
ReplyDeleteWanaolalamika hupokea vijisenti na kuuza kura zao sasa uongozi uadilifu utatoka wapi.
Sisemi mlalamikaji anauza kura yake lakini hiyo hali ya kawaida.
Kiongozi akikuhonga na ukimpa kura mumeshamaliza biashara, humdai chochote baada ya hapo.
(US Blogger)
Kwani huko Tanzania kila mtu anaweka sheria yake anayoamua ama?, kila siku kuna jipya... ila wakulaumu ni wananchi coz hawapendi kuuliza zaid ya kutekeleza
ReplyDeleteMdau mie nipo pamoja na wewe, Kutowa Tzsh 1,000 sio tatizo ila tatizo linakuja je Hizo Pesa zinafanyiwa kitu gani? Sababu mpaka leo Pachafu Barabara zinaharibu magari, ufukwe hautamaniki pesa zinaenda wapi?. MZ
ReplyDeleteAiseee yani ni kweli mdau
ReplyDeleteyani ni upuuuzi sijapata kuona
ile mali ni ya serekali...kama ni hivo waweke watu na vitambulisho from the government...if u r to base in their reasoning
but public areas zote dunaini kote HAULIPI...inakuaje coco beach unalipa???
huu ni wizi juu ya wizi
Mdau Bongo
1.NAPENDA TU KUULIZA WANATOA RISITI?
ReplyDelete2.Hatukatai,kulipa sio vibaya ila tatizo huwa zinatumikaje hizi pesa?Hakuna uboreshaji wowote unaoonekana,kuanzia ulinzi,usafi nk.
Chagua DR slaa
ReplyDeleteMimi kuna watu wananichefua sana hapa na viingelezo vyao pamoja na kuwachachafya wanaolalamikia kutozwa hiyo 1000.
ReplyDeleteNi kweli mnaweza kuiona 1000 ndogo ila ata kina bilionea kama kina billy gates na wengine walianza kuweka kwanza senti mpaka wakafikia kuhesabu mamilioni. Ki uchumi pesa ni pesa na pesa inaanziwa kuitwa pesa kwenye kuanzia ngazi ya senti.
Kinachoudhi si kulipa 1000, Unalipa 1000 kwa nani? inatumika kufanya nini? na je kweli hayo mabadiliko yanaonekana ama tuna danganywa tuu kwamba tunaboresha ulinzi na usafi wa mazingra wakati sio kweli manake ata sehemu za taka taka zenyewe hakuna na kama zipo za kuhesabu.
Jamani msiongee tuu sababu mnajisikia kuongea au kuandika. Kama ni kodi watanzania tunalipa sana hasa wafanyakazi na faida yake hatuioni vile vile zaidi tuu ya kufurahisha na kutunisha mifuko ya watu binafsi fulani fulani.
Tanzania ngumu sana kwa kweli. Inaniuma sana
Mkereketwa
kulipia shillingi 1000 sio issue, ila je PESA YETU INATUMIWA KWENYE NINI??sio kwakuwa ni pesa ndogo tu ndio utoe. we mdau wa juu unaesema mlalamkaji kama anagri elfu 1 inamshindia nini unaonekana una upeo mdogo sana wa kufikiri! mimi hata senti yangu siwezi kutoa kama sijui inatumika vipi na kwa manufaa gani!
ReplyDelete