Hi Ankal,
Habari ya majukumu ya kila siku,
Nina jambo limenisikitisha sana hapa
beach ya oysterbay. Eti kupaki gari inabidi ulipe shs. 1000 Eti
wanadai wametumwa na serikali za mitaa.
Kweli kuna haki hapo? Ukiuliza
hela wanafanyia niñi
Hupati jibu...Kulikoni??
Mdau Coco Beach

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mbona hiyo ni kidogo,ili kupunguza msongomano wa magari kwenye sehemu nyeti inabidi serikali itoze siyo hiyo tu 1000 unayozungumzia, kwa mawazo yangu labda Sh. 5000 ndiyo ingestahili.

    Hiyo ni njia mojawapo ya serikali kujiongezea mapato yake na papo hapo kupunguza msongamano usiokuwa wa lazima. Maeneo yote katikati ya miji parking lazima iwe ya kulipia kwa nchi nzima. Hii pia itasaidia katika kupunguza air polution inayotokana na fuel combustion.

    ReplyDelete
  2. Tusipende sana kulalamika. Sasa ndugu yangu unataka serikali za mitaa zijiendeshe vipi.

    One thousand shillings aka elfu moja, what is that? Mheshimiwa una gari, uwezo wa kulipia unao. Hebu fikiria kwanza uhalibifu unaoufanya kwa kupeleka gari yako beach.

    Halafu, elfu moja ni kiasi kidogo sana kubadilisha beach kwa viwango tunavyovitaka.

    ReplyDelete
  3. nauliza hivi! hii blog ya jamii mwisho wake ni Chumbe? naona haitwambii kitu kuhusu yanayoendelea Zanzibar juu ya mabadiliko ya kisiasa na mustakbali mpya wa kishuna chetu Zanzibar. au hamjayapenda haya?
    nauliza tu.

    hamad
    cph

    ReplyDelete
  4. Ndugu yangu michuzi unatakiwa uwe makini na baadhi ya vitu unavyoweka kwenye blogu yako kama hii hapa juu ameweka mwenyewe au huyo mtu uliyemweka awe anaweka taarifa kwenye blogu leo hajatulia ?

    ReplyDelete
  5. Corrupt leadership=corrupt society

    Wanaolalamika hupokea vijisenti na kuuza kura zao sasa uongozi uadilifu utatoka wapi.

    Sisemi mlalamikaji anauza kura yake lakini hiyo hali ya kawaida.

    Kiongozi akikuhonga na ukimpa kura mumeshamaliza biashara, humdai chochote baada ya hapo.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  6. Kwani huko Tanzania kila mtu anaweka sheria yake anayoamua ama?, kila siku kuna jipya... ila wakulaumu ni wananchi coz hawapendi kuuliza zaid ya kutekeleza

    ReplyDelete
  7. Mdau mie nipo pamoja na wewe, Kutowa Tzsh 1,000 sio tatizo ila tatizo linakuja je Hizo Pesa zinafanyiwa kitu gani? Sababu mpaka leo Pachafu Barabara zinaharibu magari, ufukwe hautamaniki pesa zinaenda wapi?. MZ

    ReplyDelete
  8. Aiseee yani ni kweli mdau

    yani ni upuuuzi sijapata kuona

    ile mali ni ya serekali...kama ni hivo waweke watu na vitambulisho from the government...if u r to base in their reasoning

    but public areas zote dunaini kote HAULIPI...inakuaje coco beach unalipa???

    huu ni wizi juu ya wizi

    Mdau Bongo

    ReplyDelete
  9. 1.NAPENDA TU KUULIZA WANATOA RISITI?
    2.Hatukatai,kulipa sio vibaya ila tatizo huwa zinatumikaje hizi pesa?Hakuna uboreshaji wowote unaoonekana,kuanzia ulinzi,usafi nk.

    ReplyDelete
  10. Chagua DR slaa

    ReplyDelete
  11. Mimi kuna watu wananichefua sana hapa na viingelezo vyao pamoja na kuwachachafya wanaolalamikia kutozwa hiyo 1000.

    Ni kweli mnaweza kuiona 1000 ndogo ila ata kina bilionea kama kina billy gates na wengine walianza kuweka kwanza senti mpaka wakafikia kuhesabu mamilioni. Ki uchumi pesa ni pesa na pesa inaanziwa kuitwa pesa kwenye kuanzia ngazi ya senti.

    Kinachoudhi si kulipa 1000, Unalipa 1000 kwa nani? inatumika kufanya nini? na je kweli hayo mabadiliko yanaonekana ama tuna danganywa tuu kwamba tunaboresha ulinzi na usafi wa mazingra wakati sio kweli manake ata sehemu za taka taka zenyewe hakuna na kama zipo za kuhesabu.

    Jamani msiongee tuu sababu mnajisikia kuongea au kuandika. Kama ni kodi watanzania tunalipa sana hasa wafanyakazi na faida yake hatuioni vile vile zaidi tuu ya kufurahisha na kutunisha mifuko ya watu binafsi fulani fulani.

    Tanzania ngumu sana kwa kweli. Inaniuma sana

    Mkereketwa

    ReplyDelete
  12. kulipia shillingi 1000 sio issue, ila je PESA YETU INATUMIWA KWENYE NINI??sio kwakuwa ni pesa ndogo tu ndio utoe. we mdau wa juu unaesema mlalamkaji kama anagri elfu 1 inamshindia nini unaonekana una upeo mdogo sana wa kufikiri! mimi hata senti yangu siwezi kutoa kama sijui inatumika vipi na kwa manufaa gani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...