Jazz Pianist toka Tanzania Lister Elia akipeperusha bendera ya Taifa hivi karibuni huko Tokyo Japani , kwenye tamasha la muziki wa jazz
(Tokyo Jazz Festival )
Ni jambo la kujivunia kuwa na wanamuziki kama hawa wenye viwango vya kimataifa, na wenye uwezo wa kutuwakilisha kwenye majukwaa ya kimataifa.
Unakaribishwa umtembelee kwenye tovuti yake.
http://www.listerelia.com
Ni jambo la kujivunia kuwa na wanamuziki kama hawa wenye viwango vya kimataifa, na wenye uwezo wa kutuwakilisha kwenye majukwaa ya kimataifa.
Unakaribishwa umtembelee kwenye tovuti yake.
http://www.listerelia.com
hii safi kujua muziki si bongoflava tu bali kuna:
ReplyDeleteMuziki wa dansi
Taarab original
Jazz
Blues
Reggae
Bayankata
sululu
Sokomoko
Afrosa
likembe
mchiriku
n.k n.k
Asante Lister kwa kuwakilisha na vijana wa sasa 'wanamuziki' wajifunze aina mbalimbali za mitindo ya muziki na kupiga alama, ili kupata maendeleo ya kweli kimuziki.
Mdau
Honolulu, Visiwani Pasifiki
Nikiwa ni mmoja wa wale wanaofuatilia shughuli zako na naelewa ulivyo makini kivitendo na kinadharia katika taaluma na fani yako, najua unafanya kazi nzuri sana. Unaitangaza nchi yetu vilivyo, na nakutakia mafanikio zaidi na zaidi. Kwa wadhifa wangu kama mwalimu, nawashauri watu wasome maandishi yako pia.
ReplyDeletesafi sana!
ReplyDeleteHuyu jamaa ni noma kwa kinanda...alipokuwa bongo alikuwa akipiga Mk Group pale New Africa ule wimbo wa Kibera acha chuki alifunika ile mbaya...safi sana Lister Nkuhuwala Elia!
ReplyDelete