Home
Unlabelled
TBS waanza kukagua bidhaa zinazouzwa madukani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kwa macho wataona nini? Sisi tunategemea wachukue bidhaa na kwenda nazo maabara kuzifanyia uchunguzi
ReplyDeleteWakifanya wenyewe hawataweza kumaliza hii. Ni heri kuwapa elimu watumiaji nao wajue ni kipi bora na kipi sio bora. Na kuwe kila mtu ni watch dog. Kama unaona bidhaa mbaya duka fulani watu waeleze niwapi pa kureport na kujua mahali utafuatilia kuona ni nini wamekifanya baada ya kureport tukio fulani.
ReplyDeleteWakiangalia hapo tu mjini kkule kwa bibi yangu nani atakagua. Haoa wakiona mjini hapausziki kitu watavipeleka kule kijijini kwa kina bibi wasiojua chochote.
Ni heri kuspend hela kuelimisha umma.
Vaeni nguo za kazi koti jeupe, beba vikapu chukuwa bidhaa zipeleke Lab na siyo unasoma juu ya kasha kwani kilichoka ndani ni kitu kingine. Kumbukeni mnalinda wananchi na siyo wafanya biashara.
ReplyDeleteKukagua bidhaa zinazouzwa madukani kunasaidia nini? Kama ni sumu, watu si wtakuwa wamekwisha pata madhara yake? Hebu wekeni viwango vya bidhaa, na kagueni ubora wake (bandarini au viwandani) kabla havijaingia sokoni. Kisha toeni zawadi nono kwa mtu atakayewasilisha kwenu bidhaa feki au mbovu kutoka sokoni. halafu huyo muuza bidhaa feki afilisiwe biashara yake. Hiyo haita chukua mwezi, vinginevyo itakuwa kama issue ya mizani. Ni ulaji tu huo wa hao wapitaji madukani, lakini kikweli hamna lolote!
ReplyDeleteeeee wanatafuta pesa tu hao... watajidai kuangalia angalia na kuwauliza maswali machache wauza duka kuhusu shampoo fulani eti ndio ukaguzi.. baada ya hapo watawaomba 'chochote' hawapiti tena!! washapata ulaji na kazi pia hazifanywi.. babaisha bwege tuuu..lakini watu tuko makini siku hizi...
ReplyDeletehawa ni wakaguzi au ni moja katika wateja wa hivi vipodozi?.
ReplyDeleteMimi nakubaliana kabisa na maoni ya wengine ukweli ni kuchukua bidhaa na kupeleka maabara kuangalia na macho hamna kitu ni kujifurahisha wenyewe kwamba kazi imefanyika maana huo ni ulaji wao tu hata kama kuna makosa watachukua chao na siku zinaenda na watumiaji wanaadhirika.Lazima tuilinde nchi yetu na watu wetu hizi tamaa za wachache italiua taifa.Kamati ya viwango vya bidhaa lazima iende maabara kutuhakikisha kila kitu ni salama.
ReplyDeleteJamani hii nchi yetu kwa kukurupuka tu kurukia mambo hatujambo. Sasa hapo hao wakaguzi (Auditors)wa viwango ndio wameenda dukani kukagua hizo bidhaa? Hebu Ngoja nicheke mie...LOL. Sijaona nchi nyingine yeyote dunia inafanya hivyo. Sasa Bidhaa tayari zipo sokoni wewe unajifanya kukagua nini>? Halafu unaangalia maandishi tuu unajua watu wanatoa maandishi na kubandika mengine? Hebu acheni usanii. Hii kazi inafanya kwenye maabara (Labs) kabla bidhaa hazijaenda sokoni(madukani)
ReplyDeletejamani hawa kwa nguvu ya soda! Wanaibukaga tu! kwanini wasiende kwenye garage za wachina, wanaojidai wanatengeneza magari na magodogo kumbe wanafyatua majenereta, maziwa ya makopo etc feki?
ReplyDeleteUlaji....!!!
ReplyDeleteHivi hawa wanalipwa mshahara kwa mzaha wanaofanya hapo; eti wameeanza kukagua kwani siku zote walikuwa wapi halafu unakagua kwa macho huo ni upuuzi
ReplyDeleteTFDA wakague,Tume ya ushindani wa biashara wakague, Mkemia Mkuu wa serikali na Sasa TBS haya,sitashangaa kesho kusikia TRA nao wanaingia mtaani kutafuta na kukagua visivyolipiwa ushuru na kwenda kuvichoma visivyolipiwa
ReplyDeleteHawa sio wakaguzi ni waangaliaji, TBS na TFDA wanatakiwa wajipange kwenye entry points kama vile bandarini, airports, mipakani n.k ili bidhaa zikaguliwe kabla hazijasambazwa na zile zisizo na ubora ziteketezwe mara moja kabla hazijawafikia walaji. kukagua madukani ni kujidanganya tu.
ReplyDeletenakubaliana na watoa maoni wengine lakini tukubaliane kuwa process ya ukaguzi haianzii maabara, inaanza na inspection, sampling n then lab testing, have u all thot of that!!!!
ReplyDeleteNyie mnatafuta kula tu hakuna cha kukaguwa hapo, hakuna wakaguzi wanokaguwa pekeyao bila mwenye duka kuwepo tumewaona pichani ni matapeli tu. Rudini offisini kweu mkajifunze kazi upya. Msitutie aibu. Ningewaona na kopo la maziwa ya watoto ningesema mpo kazini lakini mankaguwa vitu vya wazee. Je taifa la kesho hamlijali?Michuzi usibanie hii.
ReplyDelete