Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri Mkuu wa Rwanda, Bernard Makuza wakati alipoondukoa kwenye uwaja wa ndege wa Kigali kurejea nyumbani Septemba 6,2010 ambako alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais Paul Kagame kuwa Rais wa Rwanda. Katikati ni Mkewe,Mama Tunu Pinda
Rais Paul Kagame wa Rwanda,akiwatubia wananchi wa Rwanda mara baada ya kuapishwa kwenye uwanja wa Amahoro Mjini Kigali jana.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Iddi (kushoto) wakitembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimabali ya Rwanda yaliyopo Mjini Kigali wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipomwakilisha Rais Kikwete katika sherehe za kumwapisha Rais Paul Kagame kuwa Rais wa Rwanda, jana. Katikati na balozi wa Rwanda Nchini, Fatuma Ndagize.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ( wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimbali ya Rwanda, Mjini Kigali jana. Kushoto ni Balozi wa Rwanda Fatuma Ndagize.
Wasanii wakichenza ngoma ya Kinyarwandakwenye uwanja wa ndege wa Kigali wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiondoka kurejea nchini bada ya kumwakilisha Rais Kikwete kwenye sherehe za kumwapisha rais Paul Kagame kuwa Rais wa Nchi hiyo jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. uwanja huu wandege una majani mazuri!! halafu watu wanakaa kumuaga mgeni wao kama kwenye uwanja wa mpira!! kweli rwanda wameendelea, hata nchi zilizotangulia kuendelea hawana uwanja kama huu.

    ReplyDelete
  2. Charles ChrisSeptember 07, 2010

    Anka,hii picha ya chini ni uwanja wa ndege kweli! au umetupiga changa la macho!!

    ReplyDelete
  3. hio picha ya chini ni uwanja wa nesho ndani ya jiji la kigali amahoro unaitwa hapo mzee kijana alikua anaaapishwa kuongoza nchi kwa miaka misaba ijayo.EEH MUNGU endelea kumuongoza mzee wetu na baba wa taifa letu rwanda aendelee kuchapa kazi kwa bidii na kutuletea maendeleo kibao tupo nyuma ya mkulu wetu tunakupenda na kukusupporti mheshimiwa.MUNGU akubaliki saana kwa majukumu wananchi walokupa miaka misaba ijayo.

    mdau kigali makazi boksini kusaka chake

    ReplyDelete
  4. huo ni uwanja wa neshno wee ankali tulikuwepo hapo alaaa,,,usipotoshe watu

    aliapishwa uyo rais mwenye akili ya maendeleo na nchi yao inapaa juu kishenzy....

    God bless Rwanda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...