Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Wanawake na Watoto wa Kisiwa cha Tumbatu kijiji cha Uvivini Mkoa wa Kaskazini Unguja leo alipowasili katika kijiji hicho kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Tumbatu.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa ndani ya Boti maalum akiwapungia mkono Wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu akipokuwa akivuka kurejea mkokotoni baada ya kukamilisha ziara yake ya siku moja ya kuzungumza na Viongozi na Wanachama wa chama cha Mapinduzi wa jimbo la Tumbatu leo.
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM Dk.Ali Mohamed Shein, akipanda Boti Maalum wakati alipiokuwa akielekea kisiwa cha Tumbatu kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Tumbatu leo.
Umati Mkubwa wa wananchi na Wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), ukiwa umefurika kwenye Bandari ya Kisiwa cha Tumbatu Mkoa wa kaskazini Unguja, kwa ajili ya kumuaga Mgombea Urais wa zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein alipokuwa akirejea Mkokotoni baada ya kukamilisha ziara yake ya siku moja ndani ya kisiwa hicho leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Huyo ndio mwana CCM wa ukweli. Mpeni kura wana tumbatu. Wengine wangekuja na mbwembwe za HEDIKOPTA. Yeye hana makuu kakunja sarawili yake kavua viatu vyake kayakanyaga maji kuingia CHOMBONI.

    ReplyDelete
  2. Yakhee huko Tumbatu wakutana na akina ustadhi Ngwale!

    ReplyDelete
  3. WANACCM TUNAKIHARIBU CHAMA CHETU KWA KUKIFANYA KIONEKANE KUWA CHA WAJINGA,TULIISEMA CHADEMA UCHAGUZI ULIOPITA KUHUSU MATUMIZI YA HELIKOPTA LEO HII NA SISI TUNAITUMIA; LAKINI PIA TUNA MADAI YASIYO NA MSINGI KUWA AHADI ZAO ZOTE HAZITEKELEZEKI! CHA AJABU BAADHI YA AHADI HIZO NA SISI PIA TUMEZITOA, KAMA HAZITEKELEZEKI IWEJE NASI TUMEZITOA? AU HUWA HATUWEKI KUMBUKUMBU YA TUNACHOSEMA? TUWE MAKINI ILI TUSIJE TUKAONEKANA KUWA NI WAONGO NA WANAFIKI.

    ReplyDelete
  4. Mimi si mwana CCM ila kura yangu nitaitoa kwa Jahkaya na huyu yakhe maana ndio viongozi haswa wastaarab na wenye uungwana na wasio na majungu kama Sam 6,Butiku,Slaa,Tingatinga,S.A.Salim,Mbowe n.k

    WaTZ twaweza chagua viongozi tuwatakao binafsi ila hawa ndio chaguo la Mungu hata kanisa Katoliki liliwahi kuzungumza hivyo chaguo la Mungu siku zote halipingiki n amwenye kulipinga atalaaniwa.

    Wee Michuzi kama kawaida yako bania hii ila nishakuzoea.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  5. He is so cool...namzimia sana dr Shein ol the best on sunday!

    ReplyDelete
  6. KUBANIA COMMENT ZA WACHANGIA MADA KTK BLOG YA JAMII NI UFISADI MWINGINE HAPA NCHINI.

    KWA AMA KUOGOPA AU KULINDA MASLAHI YA WENGINE UNABANIA COMMENT ZA KIUKWELI ZINAZOTOLEWA NA WADAU.COMMENT ZOTE UNAZOTOA NI ZILE ZA WAOGA AU ZA UNYENYEKEVU KWA MTU FULANI ILA ZILE ZENYE UKWELI UNAZIFICHA.KWANINI?WHY?

    UTALAANIWA NA MUNGU KWA KUANZISHA BLOG SAFI NA YENYE KUELIMISHA WATU KWA HARAKA NA WATU WANAPOTAKA KUITUMIA BLOG KWA FAIDA YA WOTE UNABANIA.

    ADUMU JK,ADUMU DK SHEIN ADUMU MR.SUGU,ADUMU DK HUSEIN MWINYI ADUMU ZITO KABWE ALAANIWE DK SLAA NA KANISA.

    BANIA TENA HII.

    Z.A

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...