Mama Salma Kikwete.

==== ==== ==== =====

NA MWANDISHI MAALUM, IRINGA

MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete, amewataka wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), kuzingatia elimu inayotolewa kuhusu upigaji kura katika uchaguzi mkuu Oktoba 31, mwaka huu.

Alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekuwa ikitoa elimu hiyo ili kila mpigakura afahamu anachopaswa kufanya wakati wa kupiga kura hivyo wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na UWT wanapaswa kuzingatia maelekezo hayo.

Alisema hayo Oktoba 26, 2010 alipozungumza na wanachama wa UWT katika mikutano ya ndani ya kuwahamasisha kina mama kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Katika mikutano hiyo iliyofanyika katika majimbo ya Njombe Magharibi, Njombe Kaskazini, Njombe Kusini, Kalenga, Mufindi Kusini na Iringa Mjini, Mama Salma Kikwete alisema kura ina thamani na kila mpiga kura anapaswa kuipiga kwa usahihi.

“Zimebaki siku chache tupige kura tafadhali tuzingatie maelezo yanayotolewa ya namna tunavyotakiwa kupiga kura. Kura ni kitu cha thamani usikubali kupoteza kura yako kwa kusababisha iharibike,” alisema Mama Salma.

Katika hatua nyingine aliwataka kina mama wasihadaiwe na kuwapa watu wengine shahada zao za kupigia kura, pia ni kinyume cha sheria kwa mtu kumnyang’anya mwenzake kitambulisho hicho.

Alisema hivyo kufuatia taarifa kwamba kuna baadhi ya kina mama wamekuwa wakinyang’anywa shahada hizo ili wasishiriki kupiga kura katika uchaguzi mkuu.

Mama Salma ambaye amekuwa akizunguka nchini kote kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi, alisema ana uhakika CCM itashinda katika uchaguzi huo, ila kinachotakiwa ni ushindi wa kishindo.

“Tunataka kura zetu zijae mpaka zimwagike, sina wasiwasi wa ushindi hata kidogo,” alisema na kupigiwa kofi na kina mama hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Upinzani, jifingangeni vizuri ili mshike hatamu mwaka 2060!

    ReplyDelete
  2. Hiyo ndiyo picha ya First Lady wa Ikulu ya sasa na baada ya Jumapili; sio huyo kimada, Josie!

    ReplyDelete
  3. Heshima ni kitu cha bure. Mama anapendeza sana tusimkosee heshima. Ongelea siasa ya kuendeleza nchi sio chuki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...