Na Mohammed Mhiona, wa Jeshi la Polisi

Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Dar es Salaam wamesema watawatumia Askari Mgambo katika kusaidiana na Jeshi la Polisi katika kulinda Usalama wa vituo wakati wa zoezi la upigaji kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Wakurugenzi hao waliyasema hayo wakati wa mkutano wa pamoja na Makamanda wa Polisi wa Mikoa mitatu ya Kanda ya Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo wametoa wito kwa kila askari mgambo kupiga ripoti kwa mshauri mgambo wa wilaya yake.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ilala Bw. Gbriel Fuime, na Mkurugenzi wa wilaya ya Temeke Bw. Stephen Kongwa, wamesema kuwa mgambo hao watakuwa sehemu ya walinzi wa vituo na watalipwa posho kama ilivyotagazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wamesema Mgambo hao watahakikiwa na kupangiwa kazi na baadaye kutawanywa katika vituo watakavyopangiwa na wakurugenzi katika halmashauri husika.

Awali Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Naibu Kamishna (DCP) Suleimani Kova, Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Absalom Mwakyoma, na Msaidizi wake ACP Charles Kenyela, walisema ni vema kila kukijitokeza jambo la muhimu, kuvitumia vyombo vya habari katika kutoa ufafanuzi ili kuwaondolea wananchi shaka katika mambo ya kuhiisi.

Mkutano huo pia umewashirikisha maafisa waandaamizi kutoka mikoa hiyo pamoja na wakuu wa Upelelezi wa mikoa hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sasa tutajuaje kama ni wagambo,
    au wafuasi wa chama fulani.
    maana nguo zao zina fanana.
    Wasije waka tupiga yebo yebo tuka
    kosa hata kupiga kura au kula kabisa

    ReplyDelete
  2. ndio inakubalika mgambo kusaidia ulinzi,lakini akina ras makunja na kofia za nyekundu na magitaa yao lazima wawepo hili ulinzi ushamili zaidi

    ReplyDelete
  3. Hizo ndio haswaaa kazi zao badala ya kufukuzana na wamachinga kuuutwaaaa.

    ReplyDelete
  4. WASIWASI WANGU NI JEE WAMEPEWA ELIMU YA KUTOSHA JINSI YA KULINDA SIKU YA UCHAGUZI... MAANA HAWA WATU HAWANA USTAARABU WALA ELIMU WALIJE LINDA KAMA WANAVYOWALINDA WAMACHINGA MTU AKIPITA TU NA MZIGO WAO WANAUNGANGANIA NA MABEGI YAO MGONGONI WANAENDA PEMBENI KUGAWANA.!!!!! WAPENI ELIMU TAFADHALI WANAWEZA KUJA KUWA WAANZILISHI WA VURUGU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...