Umati Mkubwa wa watu uliofurika katika Viwanja vya NMC Arusha jana ukisikiliza Sera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA zilizokuwa zinatolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa (hayupo pichani) Bw, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Hai alipokuwa amelitembelea Jimbo la Arusha Mjini ili kuhamasisha kampeni za Chama chake wakati huu ambapo zimebakia siku chache kabla ya kupigwa kura za Uraisi, Ubunge na Udiwani Nchi nzima hapo Oktoba 31. katika Mkutano huo Mgombea wa nafasi ya Ubunge kwa Jimbo la Arusha Mjini Bw, Godbless Lema pamoja na Madiwani wote wa Chama hicho walipata nafasi ya kunadi Sera na kuomba kura
Wananchi wengi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Pamoja wa Mgombea Ubunge Jimbo la Hai na Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini wanaonekana wakiitikia Sera za Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wakisikiliza hutuba iliyokuwa inatolewa na Mwenyekiti wa Chama hichoTaifa Bw, Freeman Mbowe
Umati mkubwa wa watu ukiwasindikiza wagombea Ubunge kwa Majimbo ya Hai na Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wakati walipokuwa wanaondoka katika Viwanja vya NMC Arusha jana baada ya kumaliza kuhutubia - Picha zote kwa Hisani ya Arusha Mambo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Ukweli ni kuwa Chadema Arusha mjini ni chama cha Wachagga. 99% ya waliokuwa na Mbowe ni "wenzake". Kwa hivyo uchaguzi wa mwaka huu Arusha mjini ni Wachagga versus Non-Chaggas. Msemakweli mpenzi wa Mungu.

    ReplyDelete
  2. He!

    Mbona NYOMI imeanza kuPUNGUA sasa?

    Mweeh!

    ReplyDelete
  3. Tatizo watanzania wanajifanya hawaoni wala kusikia, na hata wanasahau hata kujiuliza, maana kiukweli, hata Padri nimuonavyo mie amezungukwa sana na hao watu, sasa sijui kama kutakuwa na kitu chenye kheri hapo,ila kwa sababu sie ni wadanganyika kazi kwenu, tujiangalie watanzania, lile ni kundi si demokrasia kama jina lilivyo.

    ReplyDelete
  4. Kwani Wachagga si Watanzania? tukisema Dr Batilda ni Muislam Mzanzibari mtapiga kelele ya udini na ubaguzi kwa Wazanzibari? mwageni sera na muache longolongo....

    ReplyDelete
  5. acha kuongea vitu usivyovijua,dr batilda ni muarusha,sio mzanzibar,mume wake ndo mzanzibar,na alikuwa mkiristo ndo akabadilisha dini bada ya kuolewa.so familia nzima ya batilda ni wakiristo,acheni kutuletea siasa za chuki nyie wachaga,arusha mjini hamuwezi kushinda kwa sababu dr batilda ana nguvu kubwa ya kinamama.imekula kwenu

    ReplyDelete
  6. wachaga bwana,alivyokuwa mrema mbunge wa arusha kisa mchaga walimsapoti,mwaka huu kaekwa batilda,wote wamekuwa chadema,hawa jamaa wanakatabia cha kule kenya,wahako kama watanzania hata kidogo,kila serikali iliwekeza kaskazini kwa sababu ya kulalamika sana,lakini stil wanalia tu,angalieni kaskazini na kusini ndo mtajua wachaga hawafai

    ReplyDelete
  7. Na hilo ndo kosa watanzania wanpokuwa hawajui makusudio ya kundi flani, na ndo maana wachaga kwa chadema ndo ma spear wakaubwa na ndo maana hata wateule wengi walitoka huko na watatoka huko pia.
    Any way kwa sababu watz wanazani kuna mkombozi wa kweli basi wasubiri wataona, maana lile nikundi la watu waliokataliwa na Mwalimu na Mtei ukweli huo anaujua,subirini watz mkizanimtakombolewa na kundi kutoka Kaskazini, hapo mtakuwa mmeliwa.

    ReplyDelete
  8. Nilidhani mngeongelea sera zao na mipango yao kutatua shida ya maji, elimu bora, miundo mbinu mmebaki kuongelea udini na ukabila.upuuzi mtupu. kwani shida za maji, elimu mbovu, barabara mbovu zinawagusa wachaga pekee.tuache kuongelea mambo yasiyo na msingi tuwapime wagombea kwa sera..ndio maana twapata viongozi wabovu.

    ReplyDelete
  9. Wewe Anonymous wa Thu Oct 28, 02:48:00 PM

    Acha ukabila wewe. Nenda ukapigi kura kuwa faida ya yako na vizazi vyako vijavyo. Angalia sera za vyama sio kabila la mtu. Kama unataka Afya, Elimu, na nafuu ya ujenzi, matumizi mazuri ya mali ya umma unajua chama cha kuchagua. Kama unataka maisha bora kwa kila mtanzania kwenye sera unajua pia chama cha kuchagua hapo Jumapili. Achana na ukabila

    ReplyDelete
  10. ......Ankal naona unajitahidi kweli kuchakachua maoni! yaani naamini kabisa mshikaji atakupa SALAMA yule Daktari wa meno. Kwani hakuna zawadi nyingine! au SALAMA kaolewa? kuna kale kengine ka SAma sijui kanaitwaje .....jitahidi mzee!

    ReplyDelete
  11. Jamani hakuna habari ya Uchagga wala Uislamu wala Ukaskazini na Ukusini, watu wengi wanaochangia mambo hayo matatu niliyoyataja ni vibaraka wa Chama fulani, ikubalike tu mkutano ulikuwa na watu wengi na walikuja kusikiliza sera na sio kwa sababu ya uchagga wao, udini wao au ukabila wao na ninaamini kuwa hata makada wa CCM walikuwepo kwenye mkutano huu.

    Watanzania tubadilike, tusiendelee kunywa dawa za kienyeji.

    ReplyDelete
  12. Jamanijamani mbona mnatusimanga hivyo wachaga? Mbona ndugu zetu wahaya hamuwasemi wao ndio wamezidi kuliko hata huyo mchaga mnakataa? Lakini ndugu zangu wewe utaanzaje kujenga kwamwenzako wakati nyumbani kwako huna pa kulala unaanza kujenga kwako kwanza ndio uende kwa mwingine kumsaidia tuacheni wachaga jamani tunaona mbali ndio maana kuna tofauti ya kusini na kaskazini na sisi ni Watanzania halisi tunaoipenda nchi yetu

    ReplyDelete
  13. Inasikitisha kuona mawazo ya watu wenye access ya computer tunaoamini kuwa wamepata japo elimu ndogo wanaanza kuzungumzia ukabila, sasa wanataka kutuambia arusha ina wachagga wengi namna hiyo? Mbona kikwete kajaza watu wa dini yake hatusemi ni mdini tangu mgombea mwenza, kampeni meneja, mke na mtoto makamba. Huku wale wa dini zingine kama msekwa na pinda wakiwekwa kando kama hawapo ccm

    ReplyDelete
  14. Ninyi wachaga na CHADEMA yenu hiyo mwaka huu hizo pesa mlizomchangia huyo Dr. Slaa zote inakula kwenu. Hakuna kitu. Urais hapati na wabunge hata 10 hawatafika. Ndiyo mtakuwa mmeula wa chuya!! Halafu mtaingia mitaani muanze kufanya fujo ya kuibiwa kura. Nadhani mnakumbuka jeshi na polisi, magereza na JWTZ limeshawaonya. Atayethubutu ataiona Segerea ikoje!!

    ReplyDelete
  15. ANON WA 12:39:00 PM, BATILDA SI MZANZIBARI. BATILDA NI MWARUSHA NA MMASAI KWA KABILA. AMEZALIWA DARAJA MBILI ARUSHA. AMESOMA ARUSHA MPAKA RORM IV. MPINZANI WAKE GODBLESS LEMA HAKUZALIWA ARUSHA HAKUSOMA ARUSHA NA UKWELI NI KUWA HAPA ARUSHA SUPPORTERS WAKE KARIBU WOTE NI WACHAGA. WAO NDIO WAMEANZA UKABILA. SIO SISI. PIA COMMENTS ZAKO ZINAONYESHA WAZI KUWA SILAHA KUBWA ZA CHADEMA NI MATUSI NA UONGO. j. LUKUMAY (ONCE A MORANI ALWAYS A MORANI).

    ReplyDelete
  16. Wewe muongo mkubwa unayesema eti Batilda Muungaja hujui kitu. Batilda ni Mwarusha/Mmasai kwa baba na mama. Anatokana na koo mbili maarufu sana hapa kwetu, namely, Laiser na Mollel. Uliza kabla hujaropoka.

    ReplyDelete
  17. Ndugu yangu anon wa Thu Oct 28, 06:52:oo PM, Unayosema ni kweli lakini ni lazima nieleze ukweli. Wakati Dr Batilda Buriani alipombwaga Felix Mrema vibaya sana katika kura ya maoni CCM, Wachaga waliokuwa wakimsapoti Felix walianza kumsapoti Godbless Lema wa Chadema. Hicho ndicho chanzo cha hali ya sasa Arusha. Matokeo yake ni kuwa wazawa na wenyeji wengi wa Arusha wameamua kuwaiga wachaga na kulipiza kisasi kwa kumuunga mkono binti yao mwenyeji, mzawa wa Arusha na msomi. Usianzishe kitu bila kufikiria matokeo yake. Morani7.

    ReplyDelete
  18. Batilda ni MMasai, amezaliwa Arusha, amesoma Arusha, mama na ndugu zake wanaishi Arusha ana nyumba Arusha na atakuwa mbunge wa Arusha kuanzia mwaka huu. Copy and paste that non-Arushans!!!!! "Muhoshya" Sing'ati. A-Taun (proudly native).

    ReplyDelete
  19. Ama kweli sasa yatasemwa mengi. Inawezekana Batilda akawa wa Arusha. Inawezekana pia akawa amesoma Primary Arusha. Lakini huyo aliyesema kuwa Batilda kasoma mpaka Form IV Arusha ni muongo. Mimi nimesoma na Batilda Kibosho Girls Secondary School kuanzia mwaka 1977 mpaka 1980. Kibosho Girls iko Moshi na siyo Arusha.

    ReplyDelete
  20. Mmmh nimeamini wachaga tuko juu na ndio maana kwetu kunamaendeleo lami mpaka kwenye vitongoji, umeme umesambaa kila kijijia. sasa nyie waosha vinywa nimegundua ni kwanini hamuendelei, mna wivu tena wa kijinga si ule wa maendeleo, hata tusipoenda ikulu bado umeme upo nyumban, maji, gari yangu haikwami lami mpaka home so nyie endeleeni na ujinga, nasema ujinga kwa sababu sera za chadema ni kwa ajili ya nchi nzima na kama mtachagua chadema naapa kweli hizo nyumba za nyasi karibu tanzania nzima zitakwisha. mtu anakuja kuona nyumba ya bati mjini wajameni wapeni chadema hicho chama cha wachaga "kama mnavyoita ila sio mimi" nchi muone kama maendeleo hayatakuwepo.

    Nilipoanza kutembea kwenye mikoa ya watu nilikuwa najiuliza maswali mengi sana, sasa majibu nayapata hapa, jealous, ndio inawazuia kuwa na maendeleo poleni sana. mkikataa kuchagua eti wachaga, ni kijiji gani au mji gani au nchi gani utaenda umkose mchaga??? Nauliza jamani ka mikoa mingine wao wameshatawa so bado tumewatala whether you like or not kwani hata maduka makubwa, hotels, sheli n.k. ni wachaga/wahindi so acheni wivu wa kijinga tafuteni maendeleo huwezi fananisha mji wa wachaga (moshi) kimazingira na mji wowote tanzania.

    ReplyDelete
  21. Watanzania wenzangu, tuwe na fikra pevu, CHADEMA sio chama cha wachaga Arusha Mjini, napenda kutaja Viongozi wa Chadema ambao sio wa Chaga, ambao ndio viongozi waandamizi wa Chadema.
    Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha Samson Mwigamba (Mkurya)
    Katibu wa Mkoa Aman Golugwa (Anatoka Kanda ya kati)
    Mratibu wa Wazee Mkoa Chifu Fundikira (Mnyamwezi)
    Mratibu wa Vijana Mkoa Ephata Nanyaro (Mmeru)

    WIYAYA YA ARUSHA MJINI.
    Mwenyekiti wa wilaya Derick Magoma (sijui ni mtu wa wapi, kuna watu wanasema ni mwarabu na wengine wanasema ni Mjerumani sasa sijui lipi ni sahihi)
    Katibu wa Wilaya Bakari Kasembe (Mmakonde)
    Katibu Mwenezi wa wilaya Gabriel Lucas (Mmasai)

    ReplyDelete
  22. Aaah Amani Golugwa namjua, huyu mshikaji mnyisanzu wa singida. Hapo hamna ukabila na Amani nimesoma nae ni kichwa kama wapo na huyo Mbunge Lema kuna kazi itafanyika.

    ReplyDelete
  23. HAO JAMAA NAWAJUA NI KWELI HATI YAO HAKUNA MCHAGGA, WATANZANIA ACHENI UNGONGANISHI USIO NA TIJA.
    FANYENI KAZI TUJENGE TAIFA LETU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...