Pichani kati ni Mwisho Mwampamba akiwa na Meneja Masoko Multichoice Furaha Samalu pamoja na (kulia) Meneja Mahusiano Multichoice Barbara Kambogi.Mwisho amezungumza na vyombo vya habari mbalimbali leo asubuhi ndani ya hoteli ya Holiday Inn jijini Dar kuhusiana na mambo mballimbali yaliokuwa yakijiri kwenye jumba hilo la shindano la BB Africa Allstars ambalo limefikia tamati hivi karibuni.

Mwisho pia aligusia suala la maandalizi ya harusi yao na Merry mara baada ya yeye kumvisha pete ya uchumba mrembo huyo ndani ya jumba la BigBrother. Mwisho amesema kuwa kwa sasa hawezi kuzungumzia lolote juu ya hilo,kwani jambo hilo linawahusu wote wawili (Yeye na Mchumba wake) ,hivyo si vyema kulizungumza ama kulitolea maamuzi akiwa peke yake,anasema na kuongeza kuwa kama angekuwepo Merry angeweza kujibu chochote juu ya hilo wote wakiwa pamoja,hivyo hawezi kusema lolote juu ya mipango yao ya ndoo kwa sasa..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mh kashamwaga huyo, ile ilikuwa zuga tu ili apate ushindi. Mwisho rudi zako Moro kauze viatu tu. si tulisikia ulimuoa Ray C kwa siri sasa talaka ulimpa au? Jamaa unapenda sana attention wewe, sikufagilii wala nini.

    ReplyDelete
  2. jamani zungumzia kuhusu ulivyoona mambo yalivyokwenda acha uzushi vitakuridia baadae watu hawsahau.

    ReplyDelete
  3. Jamani acheni wivu ndugu yetu afadhali katutangazia jina la tz sio kama vile mlivyomfanyia hashim thabit, hata hajashinda mmemkaribisha kila pahali ona sasa alivyotuangusha...............

    kaka mwisho achana na watu hawa wenye majiba ya roho, do you.

    ReplyDelete
  4. Hivi hilo jina la mwisho ni lake la kweli au? na anatoka wapi huyu mkwamis? mi niko ugaibuni nataka kumwalika, kama kuna yoyote ana data zake tafadhali chapa.

    NB: mi ni wakili na niko singo hehehe

    ReplyDelete
  5. we mwisho ulevi ndio unakuponza... ukiacha pombe with those looks utafika mbali..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...