
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Mh Joel Bendera akimkabidhi nahodha wa timu ya taifa Sophia Mwasikile bendela ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na cd ya wimbo wa Taifa ,Timu hiyo inaondoka kesho kwenda Gaborone Botswana kucheza mechi ya kirafiki na botswana na baadae kuelekea nchini Afrika kusini kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika ya wanawake yanayoanza mwezi ujao mwaka huu.

Meneja bidhaa wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Dada Nandi Mwiyombela akiwakabidhi viongozi wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Twiga Stars mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni
97,13,500 ambazo zimetolewa na kampun hiyo kwa ajili ya maandalizi pamoja na vifaa mbalimbali vya michezo zikiwemo jezi.

Meneja bidhaa wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Dada Nandi Mwiyombela akikabidhi vifaa vya michezo kwa nahodha wa timu ya Taifa ya Twiga Stars,Sophia Mwasikile huku Naibu Waziri wa Michezo habari na utamaduni Mh Joel Bendera pamoja na Kaimu katibu mkuu wa TFF na Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya TFF,Sunday Kayuni wakishuhudia.Picha zaidi
Bofya Hapa
Sielwi hili: "...thamani ya shilingi milioni 97,13,500..."
ReplyDeleteUbaya wa habari za kwenye internet nyingi hazina mhariri!
Mmh Dada Nandiimekuwa kitambo..tokea Bunge. Endeleza libenek zuri la wana Bunge.
ReplyDeleteClass of '91 Bunge Primary School.
hizo posho muwapatie na hao watoto wa watu, siyo mnatafuna mpunga wote wenyewe .
ReplyDelete