====================
Ubalozi wa Marekani nchini umemteua mwandishi wa habari wa gazeti la The Guardian Bw. Lusekelo Philemon, kushiriki katika Programu ya kufuatilia na kuandika habari kuhusu uchaguzi wa muhula wa kati wa mwaka 2010 kuchagua Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Marekani iliyoandaliwa na Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Marekani (U.S. Foreign Press Center).
Katika ziara hiyo ya siku nane Bw. Philemon atatembelea miji ya Florida, Nevada na Washington D.C. ili kujionea kinyang'anyiro cha uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wajumbe wa Seneti na Magavana. Ziara hii itaanza tarehe 28 Oktoba hadi tarehe 5 Novemba 2010.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Ubalozi wa Marekani Bw. Roberto Quiroz II, "chaguzi za haki na zenye uwazi ni msingi wa demokrasia katika nchi yoyote. Vyombo huru vya habari vinajukumu muhimu la kulinda haki ya watu ya kuchagua viongozi wao katika ngazi zote za serikali. Bw. Philemon atapata fursa ya kuripoti kutoka Marekani masuala muhimu mbalimbali yanayogusa nchi zetu akiyaangalia kwa kupitia mboni ya hali ya kisiasa ya Marekani."
Akiwa huko Florida na Nevada, Bw. Lusekelo atashuhudia masuala yanayoangaziwa sana kwa sasa katika mijadala na midahalo ya kisiasa nchini Marekani na kuweza kutathmini mchakato wa kisiasa wa Marekani na nafasi ya makundi mengine kama vile Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Vyama vya Wafanyakazi na makundi ya washawishi katika uchaguzi.
Huko Florida, masuala yanayoweza kujitokeza katika kampeni ni pamoja na deni la serikali, nishati zisizoharibu mazingira, utafutaji wa mafuta na gesi, marekebisho ya sheria za uhamiaji na elimu. Huko Nevada, masuala yatakayojitokeza katika kampeni ni pamoja na namna ya kushughulikia takataka za nyuklia, mabadiliko katika sera za utoaji huduma za afya na haki ya matumizi ya maji.
Bw. Philemon atakutana na kufanya mahojiano na maafisa wa kampeni, waangalizi wa uchaguzi na wadau wengine wa uchaguzi katika majimbo ya Florida na Nevada jambo litakalomuwezesha kupata habari na kutayarisha taarifa ya kina kuhusu uchaguzi huo wa wajumbe wa Seneti katika majimbo hayo.
Ziara hii itamalizikia katika jiji la Washington, D.C. kwa kuangalia shughuli zinatakazofanyika baada uchaguzi na uchambuzi wa mwenendo mzima wa uchaguzi huo. Hapa Bw. Philemon atakutana na wanasiasa kutoka katika vyama vya siasa na wadau wengine wa siasa na kutoa taarifa yake kuhusu umuhimu wa matokeo ya uchaguzi huo kitaifa.
Kwa kuwa hivi sasa Tanzania, kama ilivyo Marekani ipo katika kipindi cha kampeni za uchaguzi, ziara hii ya kiuandishi imekuja wakati mwafaka, kwani itampatia Bw. Philemon fursa ya kulinganisha mikakati ya kampeni, masuala yanayozungumziwa katika kampeni hizo na hali ya kisiasa katika nchi hizi mbili.
Aidha, akiwa ni mwandishi wa habari pekee wa Kitanzania aliyepewa nafasi ya kuripoti uchaguzi huu, Bw. Philemon atakuwa katika nafasi nzuri ya kutoa taarifa za maendeleo ya mchakato mzima wa uchaguzi kwa kadri utakavyokuwa ukiendelea na kuelezea wajibu muhimu wa vyombo vya habari katika mchakato huo.
Katika mkutano mfupi wa kuagana uliofanyika katika Ubalozi wa Marekani hapo tarehe 25 Oktoba, Bw. Philemon aliwashukuru watu wa Marekani na Kituo cha Habari cha Kimataifa cha Marekani kwa kudhamini ziara hii, akisema kuwa, "ni matumaini yangu kuwa ziara hii itaongeza uelewa wangu kuhusu Marekani na kuboresha ujuzi wangu katika kuandika habari na makala kuhusu masuala ya uchaguzi.
Hii ni fursa muhimu itakayonikutanisha na waandishi wa habari wa Marekani n kujionea jinsi waandishi wenzangu wa nchi hiyo wanavyoripoti masuala ya uchaguzi."

Bradha mstue Mkubwa mwenzako KITIME anavyofanya sio vizuri.
ReplyDeleteKama hawezi kuendesha Bulogi afunge.
We mwezi mzima hakuna apdets wangu? Tunatuma koments mpaka zinaozea huko ndani kwa ndani!?!
Khaah!