WAKILI MKUU WA SERIKALI KUTOKA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI, DONALD CHIDOWU(KATIKATI) AKIFUATILIA MAJADILIANO KUHUSU MKAKATI WA JUMUIYA YA KIMATAIFA WA KUKABILIANA NA UGAIDI. MKUTANO HUO AMBAO UMEANDALIWA NA KAMATI YA SITA INAYOHUSIKA NA SHERIA ZA KIMATAIFA KATIKA BARAZA KUU LA UMOJA WA MATAIFA, UMEWAKUTANISHA WATAALAM WA MASUALA YA SHERIA KUTOKA MATAIFA WANACHAMA WA UMOJA WA MATAIFA NA UNAFANYIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA HUO JIJINI NEW YORK.

NA MWANDISHI MAALUM

NEW YORK

Tanzania imesisitiza kwamba inayo nia na dhamira ya dhati ya kushirikiana na jirani zake na jumuia ya kimataifa, katika kupambana na vitendo vya ugaidi ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wanajiohusisha vitendo hivyo.

Msisitizo huo umetolewa na Wakili Mkuu wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Bw. Donald Chidowu, wakati wataalam wa sheria wa Kamati ya Sita ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, walipokuwa wakijadili juhudi na mikakati ya Jumuia ya Kimataifa na kitaifa katika kukabiliana na kupambana na ugaidi.

“Kama nchi ambayo imeoja ukatili wa matukio ya kigaidi, dhamira na nia yetu iko wazi kabisa nayo ni kushirikiana na jumuia ya kimataifa na majirani zetu dhidi ya ugaidi”.

Bw. Chodowu anayeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo, akasema Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine inalaani kwa nguvu zote tukio la kigaidi lililotokea jijini kampala, Uganda mwezi julai. na kwamba inaugana na serikali ya Uganda katika kuwatafuta na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria yeyote atakayepatikana kuhusika na tukio hilo.

Akasema ugaidi hauna rangi, dini, haujali mipaka na wala hauchagui nchi. Na akaongeza.” Kila mtu ni mhanga wa ugaidi, hakuna mwenyewe uhakika wa kutoguswa na matukio au tukio la kigaidi. Na kwa sababu ya unyeti wa matukio yenyewe, ni ukweli usiopingika kwamba tunahitajika kama jumuia ya kimataifa, kuunganisha nguvu zetu na mikakati ya pamoja kuukabili ”.

Akabainisha kuwa wakati jumuia ya kimataifa ikiendelea kuvutana na kubishana juu ya tafsiri ya ugaidi, ucheleweshaji wa ukamilishwaji wa rasmu kuhusu mkataba wa ugaidi, ndivyo ugaidi unavyojikita na kuibuka na mbinu na mikakati ya hali ya juu.

Akatoa wito wa jumuia ya kimataifa kumaliza tofauti zao, kuonyesha utashi wa kisiasa na ushirikiano ili rasmu hiyo iweze kukamilika.

Kuhusu juhudi zinazofanywa na serikali ya Tanzania katika kukabiliana na kudhibiti ugaidi, pamoja na mambo mengine, Wakili Mkuu wa serikali ameuleza mkutano huo kwamba, Tanzania kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa imekuwa ikiandaa mafuzo kwa maafisa wa ngazi za juu kutoka mamlaka za utekelezaji wa sheria.

Akasema mafunzo wanayopewa yanahusu namna ya kuukabili ugaidi na uhalifu wa kimataifa .

Aidha akasema Tanzania katika kuunga mkono mkakati wa kimataifa wa kupambana na ugaidi, inaandaa mkakati wa kitaifa na akatumia nafasi hiyo kuziomba jumuia ya kimataifa kuipatia Tanzania msaada wa kiufundi ili kusaidia mpango wa utekelezaji.

Karibu kila mjumbe aliyezungumza katika mkutano huo, alitoa wito wa kutaka kumalizwa kwa mkanganyiko kuhusu tafsiri sahihi ya ugaidi na kusisitiza kwamba rasmi inayoandaliwa lazima ije na tafsiri itakayokubalika.

Aidha licha ya kila mjumbe kueleza nchi yake inafanya nini katika kukabiliana na ugaidi, baadhi ya wajumbe wamesisitiza kwamba juhudi za kukabiliana na ugaidi lazima ziheshimu haki za binadamu na mipaka ya nchi nyingine na kwamba kinyume na hayo, juhudi hizo zitakuwa kazi bure.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. UGAIDI MKUBWA TULIO NAONI:
    ELIMU;
    UKIMWI;
    HUDUMA DUNI ZA AFYA:
    KILIMO DUNI:
    TUUKABILI HUU KWANZA:

    ReplyDelete
  2. Ni swa tukishirikiana sote ni rahisi kumkamata aliyeshukiwa kuwa ni gaidi! Lakini kesho ataibuka mwingine, keshokutwa mwingine, mara wanaongezeka na kuwa `magaidi'!
    Tatizo ni kuwa hatutazami chanzo cha ugaidi' kwanini kutokee huu ugaidi. Nafikiri hali halisi inaaznia kwenye `haki' kwenye `hali za kimaisha' !
    Sijui lakini mimi naona tutakuwa tunakata matawi wakati mti na shina bado lipo, na mti na shina la namna hii huchipua haraka sana, sasa tutakata weeeeee., mwisho wa siku limti litakuwa kama mbuyu, hata kuupanda kukata hayo matawi itakuwa shida!

    ReplyDelete
  3. Chidowu bila shaka umesoma gazeti la New York Times la Leo (October 7, 2010)Page 1 & Page 4; Kuna habari zinazohusu nchi yetu, na mfungwa yanetuhumiwa kuhusika na Ugaidi. najua New York inakuwa na pilika pilika nyingi hivyo unaweza usipate nafasi ya kupitia habri zake; na Bila shaka mlikuwepo Jana kwenye Federal Court, manhattan jana.

    ReplyDelete
  4. USHINDI UTAKUJA KWA KUJUA CHANZO NA KUTUMIA MBINU SAHIHI

    Katika vita dhidi ya ugaidi, Rais Bushi alikosea kutumia neno "Crusade against evil" japo alikuwa sahihi ni "vita dhidi ya uovu."

    Kama wakristo wachukuliavyo neno "Jihadi" kama vita dhidi ya wasio waislamu, waislamu nao huelewa neno "crusade" kama vita vya msalaba na hulenga wasio wakristo. Pia wakaingia wachochezi wengi ikiwemo wahubiri wa dini kwa kusema Uislamu ndo ugaidi.

    Matokeo yake vita imechukua muda mrefu zaidi ya ilivyotarajiwa. Kwani baadhi ya wailamu (chini ya 0.0001%) huona kama wanalengwa kuuliwa au kukandamizwa. Kila gaidi mmoja akiuliwa vitani magaidi wawili wapya huingia kundini kutokana na hisia ya mauwaji na huruma (kama yule wa chupi-bomu).

    Nakubaliana na Emu-three kwa 100%, chanzo kitafutwe na njia sahihi ya kutokomeza ugaidi. Ugaidi hautaisha ikiwa kila mwisilamu anaona aitwa gaidi. Lazima lugha ya ustaarabu iwepo na watu wajuwe kuwa 99.9999% ni watu wa amani na huielewa dini yao vizuri.

    Pia kama kuna uwezekano wa kuweka mtutu chini na kutumia njia nyingine za ki-aidiolojia itakuwa bora zaidi. Nadhani nusu ya fedha itumikayo kuendesha vita inaweza kutokomeza ugaidi kwa njia nyengine nyingi tuu.

    Waislamu lazima washiriki kikamilifu na waongoze vita dhidi ya ugaidi na ugaidi ukiisha lugha iwe nzuri. Isije kuwa "jamaa wameuwa watu wa dini yao kwa kusema ni magaidi, msiifuate dini hii watawauwa na ninyi baadaye." Naona hata bongo mitaani ukiwa mwisilamu ukasema we ccm watu wanaganga wanasema lazima utakuwa cuf kwa siri. Haya maswala ya kutiliana mashaka na kutokuaminiana ndo hata raisi Obama anapingana nayo kila siku.

    Vita imekuwa ngumu, imebidi Raisi Obama awaambie watu kuwa vita si dhidi ya Uislamu bali waislamu wachahe mno ambao hawajaelewa dini hii na kuanza kuuwa watu wasio na hatia. Huko Kabul Karizai naye anafanya mapatano na talibani ili waungane kumwondoa alikaida. Lakini kwa sababu watalibani waliwekwa kundi moja na alikaida (ambao wenyewe waliwakumbatia kijinga) wanaweza kusema "wakiwamaliza alikaida watatufuata sisi."

    Mwisho, nimependa saana wazo la M-3.

    ReplyDelete
  5. TUSITENGENEZE MAGAIDI

    Anko Michuzi, ikiwa maneno haya ni makali saana au yanashambulia na kuamsha hisia, usitundike. Lengo ni ufahamu kwa amani.


    Sina data ila kuna kauli mitaani kuwa osama kafundishwa ugaidi US. Na kwamba kwa ugaidi huo ndo Afghan iliweza kupata uhuru kutoka kwa Urusi. Inafana na stori za kina mkwawa, bwana heri na kinjikitile. Wapigania uhuru!!!.

    Ukitengeneza gaidi mmoja magaidi wengine watazaliwa na madhara yatawafikia hata wasio walengwa. Sasa leo dunia nzima tuko tunamwinda jamaa huyu ambaye utaalamu wake ulisababishwa na uhasama kati ya mataifa makubwa mawili.

    Hata tanzania na kenya tumekuwa waathirika bila hatia kwa sababu tu hatuna ulinzi wa kutosha kwa wageni wetu.

    Swali:Ikiwa chanzo cha ugaidi ni wapinga ugaidi wenyewe itakuwaje? Wako tayari kubadilika? Nikimaanisha: kama vitendo vya serikali zetu huamsha hisia na hamasa za ugaidi itakuwaje?

    Obama: Ugaidi umeuwa waislamu wengi zaidi ya watu wengine (hotuba ya kairo).

    Leo gaidi yuko radhi kuuwa waislamu 10000 japo kwa kumpata mmarekani mmoja sokoni. Watu nao washambulia Uislamu kwa lawama za ugaidi. Hapa mwisilamu kazingirwa kila kona. Sasa itakuwaje? Maana mwisilamu huyu kama ananyimwa nafasi ya kupigana dhidi ya ugaidi na anwekwa (kimazingira) katika hali ya kutetea dini yake dhiti ya tuhuma, ambapo magaidi wanaweza kumchota pia kirahisi.

    Osama: magharibi wanataka kuuwa waislamu woote kwa vita na serikali.

    Hata vita za marekani dhidi ya ugaidi zinafanya osama aonekane mkweli kwa vita na kambi za kijeshi zilizoko arabuni. Hapa huyu osama au sadamu alitakiwa atafutwe na kukamatwa kijasusi kuliko vita ya nchi nzima. Au kuna sababu za siri (mafuta ya iraki na lithiamu ya afghani)?

    Hakuna kisingizio cha ugaidi lakini lazima ifahamike kuwa cheche moja huunguza numba nzima. Kuwa na lugha zisizo na tuhuma za jinai ni bora. Mmoja kati ya 1.5 bilioni akihisi anaitwa gaidi bure halafu akaamuwa kuwa kweli unadhani wangapi watakufa? (Mfano wa kiswahili ukimtuhumu mpezio katembea nje naye anatembea kweli ili kukukomoa kwa tuhuma zako za uongo). Ukimuua gaidi huyu mmoja unazalisha 10 wengine.

    Lazima tutambue kuwa ugaidi ni jinai na mjinai pekee ndo awajibike na sio watu 1.5 bilioni.

    Wahubiri lazima wajuwe kuwa kuleta lawama za ugaidi kwa waislamu hakuwafanyi wabadili dini bali kunazusha uwezekano wa ukinzani na kupata magaidi zaidi.

    Mawazo mazuri kama demokrasia n.k. lazima yaenezwe taratibu na kwa hiari.

    Maswala yasiyo ya lazima yazuwiliwe. Sawa waislamu wamekosea kwa kupinga katuni, Lakini kulikuwa na ulazima gani wa kuchora katuni. Tena mchoraji akijuwa kabisa kuwa patakuwa na tafrani.

    Ugaidi ni dhana iliyo MZUNGUKO amabo watu woote wanauchochea. Sioni kama watu 1.5 bilioni wanaweza kubadili tabia ya 'kumpokea ajavyo [yaani njoo kwa heri upate heri, njoo kwa shari urudi kwa shari]" ndani ya siku moja [iliyojengeka kwa miaka 1500]. Naona watu wastaarabu wa magharibi wanaweza kujizuia kuamsha hisia zisizo za lazima, kama katuni n.k. Tunayapenda maisha jamani.

    Watu wameacha mafundisho nyeti ya dini zao hasa wakristo. Mafundisho yanasema mpende adui wako [mshinde adui kwa njia ya upendo, akishika silaha mpe chakula na maji ya kunywa]lakini leo adui awindwa zaidi ya simba [wasema ukimpa chakula atarudi kesho tena.] wanapinga mafundisho bila habari. Pia kutii serikali, angalia hata wachungaji waanzisha vyama vya kupinga serikali. Hakuna mtu hata mmoja anageuza shavu la kulia tena, kila mtu ukimpiga kibao ye akupiga viwili na ngwala juu ili ukome hasa.

    UKUMBUSHO: Hapa uislamu na ukristo havilaumiwi bali wafuasi wavyo kwa kushindwa kufuata na kufuata matamanio yao.

    ReplyDelete
  6. Nauliza nani gaidi? Manake hata Mzee Nelson Mandela wakati anapigania uhuru aliitwa gaidi. Inategemea unatumia tafsiri ipi na kwa masilahi ya nani. Mtu anaweza kuwa 'gaidi' kwako akawa 'shujaa' kwa mwingine. Tusifuate mkumbo tu ili mradi "Bwana Mkubwa" kasema fulani ni gaidi nasi tunaimba wimbo bila kujua maana yake!

    ReplyDelete
  7. Jamaa mmoja aliniambia "hata ukijidai una amani wenyewe wanajua sisi wote magaidi tuu, ikifika saa watatulamba."

    ReplyDelete
  8. Watu woote ambao katika kupigani uhuru palihusika na vurugu wallitwa magaidi.

    Hata mkwawa, bwana heri, kinjekitile, samora macheli, savimbi, mandela, n.k. ni magaidi kwa tafsiri hizo.

    Mandela haruhusiwi kuingia marekani kwani ni gaidi.


    Lehi (kikundi cha kupigania uhuru israeli) kiliitwa cha kigaidi.

    Hamas (kikundi cha uhuru wa palestina) kinaitwa cha kigaidi.

    TAFSIRI YA UGAIDI HAIJULIKANI!!!!!

    ReplyDelete
  9. For the first time in this Globu...comment zooote zimeenda shule. Yangu macho, wenye vichwa changieni.

    ReplyDelete
  10. UOVU HUWAGHARIMU WEMA ZAIDI YA WAOVU

    1. Gharama ya kwanza ni kuwa watu wema ndo waatjirika wa jinai,

    2. Watu wema ndo hulipa gharama za kuwaadhibu wajinai kupitia kodi (swali: uwiano gani kati ya watu wema na wajinai utafanya mahakama na magereza zishindwe kuendeshwa kutokana na kodi ndogo? ukiongeza kodi watu watashindwa kulipa au watapinga)

    3. Adhabu kali huongeza uovu zaidi na kuwaathiri zaidi wema (kama kuuwa magaidi au kuwatesa huko gtmo kunazaa magaidi zaidi)

    4. Vita dhidi ya magaidi huathiri raia wema zaidi ya magaidi na kuzaa magaidi zaidi (watu wangapi wamekuwa wakimbizi na kupoteza utu wao huko iraki, magaidi wangapi wameongezeka tangu vita ianze?)

    5. Sijawahi kusikia eti mahakama imemsamehe mjinai mahakamani, naona tu eti raisi husamehe wafungwa tena sanasana wale wa kesi nzito kama mauwaji. Kwa nini wauwaji wasmehewe na wezi wa kuku watumikie vifungo? Kwa nini hatutumii msamaha kama njia ya kuondoa jinai? Kwa nini kufungwa ndo njia pekee, mbona hamna kwa mfano adhabu ya kulipia jinai, kama mtu kaiba kuku alipe kuku na usumbufu?




    MBINU ZA KWELI ZINAHITAJIKA HAPA
    pendekezeni


    hivi kwanza hao viongozi hata wanapata mawzo haya au ni kujifurahisha (ngoja tujifurahishe, ni fani)

    ReplyDelete
  11. Governor among 20 killed in Afghan mosque blast

    Comment:"Terrorist on terrorist crime is ok in my book."

    Kwa nini ugaidi uishe wakati kila mtu aitwa gaidi? Je nipigane kuondoa ugaidi au nijitee mimi sio gaidi na kukuachia upambane nao peke yako?

    ReplyDelete
  12. ONE MAN TERRORIST IS ANOTHER MAN FREEDOM FIGHTER

    ReplyDelete
  13. Do we fight for freedom in the oppressor's way or the way of the oppressed.

    For sure oppressors dont like violance against them. They want you a friend when you have freedom. Why did they oppress in the first place?

    Appatheid, occupations, invasions, terrorism, crimes, where are we going?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...