Habari za Shughuli Mh. Michuzi.
Baada ya salamu,naomba nichukue nafasi hii kutoa ushauri wangu kwa ndugu jamaa na rafiki zetu waishio ughaibuni
Kwa miaka ya karibuni kumekuwepo na matukio ya vifo mbalimbali vya ndugu zetu waishio huku nje na hivyo kulazimu kuomba msaada wa jinsi ya kusafirisha miili ya marehemu hao, na blog hii imekuwa ikitumika sana katika kutoa taarifa hizo za misiba na kuomba misaada hiyo.
Kwanza tunakushukuru kwa kutoa msaada wa kutoa taarifa za haraka kuhusu misiba hiyo
Pili niombe ndugu zetu waliopo nje waanjishe umoja wao katika nchi mbaimbali wanzoishi ambapo watakuwa na akaunti zao maalumu kwa ajili ya matatizo wanayoyapata huko ikiwepo ya misiba ili kuepusha ombaomba tukio linapotoea kwani tunaamini wenzetu waliopo huko wananafasi nzuri zaidi ya kukusanya fedha kwa maendeleo hivyo watumie fulsa hiyohiyo kuanzisha akaunti za misiba
Waige kwetu sisi tuliopo huku nyumbani, mathalani utaona sisi wa Iringa tuishio Arusha tuna umoja wetu wakusaidiana wakati wa matatizo hivyo kutokuwa na tatizo la kuomba msaada zaidi tukio la aina hiyo linapotokea.
Waimarishe umoja wao huko waliko
Asante
Mdau Frank
Arusha
Baada ya salamu,naomba nichukue nafasi hii kutoa ushauri wangu kwa ndugu jamaa na rafiki zetu waishio ughaibuni
Kwa miaka ya karibuni kumekuwepo na matukio ya vifo mbalimbali vya ndugu zetu waishio huku nje na hivyo kulazimu kuomba msaada wa jinsi ya kusafirisha miili ya marehemu hao, na blog hii imekuwa ikitumika sana katika kutoa taarifa hizo za misiba na kuomba misaada hiyo.
Kwanza tunakushukuru kwa kutoa msaada wa kutoa taarifa za haraka kuhusu misiba hiyo
Pili niombe ndugu zetu waliopo nje waanjishe umoja wao katika nchi mbaimbali wanzoishi ambapo watakuwa na akaunti zao maalumu kwa ajili ya matatizo wanayoyapata huko ikiwepo ya misiba ili kuepusha ombaomba tukio linapotoea kwani tunaamini wenzetu waliopo huko wananafasi nzuri zaidi ya kukusanya fedha kwa maendeleo hivyo watumie fulsa hiyohiyo kuanzisha akaunti za misiba
Waige kwetu sisi tuliopo huku nyumbani, mathalani utaona sisi wa Iringa tuishio Arusha tuna umoja wetu wakusaidiana wakati wa matatizo hivyo kutokuwa na tatizo la kuomba msaada zaidi tukio la aina hiyo linapotokea.
Waimarishe umoja wao huko waliko
Asante
Mdau Frank
Arusha
Mdau Frank wa Arusha, nakumiminia tano (5). Umesema kweli. Ni ukweli ulio wazi kuwa tulioko nje ya inji tuna nafasi nzuri kimshiko! Tunajitahidi kwa kila namna ya kuonyesha jinsi tunavyoishi maisha yaliyotangulia kulinganisha na Bongo kwetu.
ReplyDeleteKila kukicha hatuko nyuma kumtumia ankal mapicha yetu ya matanuuz ughaibuni. Lakini pia hatuko nyuma katika kumtumia maombi ya ombaomba kama ulivyosema bwa Frank. Hii haijakaa vizuri ati.
Tunaweza kuyafanya hayo yote kimoyomoyo tu (yaani kimyakimya) bila ku goo public. Ni fedheha kuchangishana mitandaoni. Lazima tuonyeshe upevu wa fikra na akili.
Ahsante Frank
Chiaaz Mchiiiz
wanajua tu kufungua matawi ya ccm na kuparty, mambo nyeti hayapewi kipaumbele!
ReplyDeleteKWANI WAKATI WANAOMBA OMBA WANAOMBA NYINYI WA ARUSHA ,MBEYA AU TZ KWA UJUMLA???? UNAJUWAJE KAMA WAKATI WANATOWA MATANGAZO YA VIFO NA KUOMBA MISAADA UNAJUWAJE KAMA WALENGWA WAO NI WATU WA UGAIBUNI????WEWE KAKUAMBIA NANI WANAOMBA WATU WA ARUSHA NA MBEYA????HII BLOG NI MPAKA UGAIBUNI WEWE MLOPOKAJI.
ReplyDeleteMichu naomba usiibanie hii comment ina mambo ya maana....
ReplyDeletemie nina mambo mawili. kwanza, watu wanatakiwa kununua life insurance, for USA it cost less than $10 a month kwa walio wengi.
pili utakuta mtu akifa na ana life insurance watu bado wanaendelea kuchangisha na ile hela ya life insurance ndugu na jamaa wanagawana. life insurance kazi yake ni ku-cover costs zote za funeral including kusafirisha mwili na zinazobaki wanapewa beneficiaries na hiyo hela inatosha kabisa na kubaki. kwa hiyo before kuanza kuchangisha tunahitaji kuhakikisha kama marehemu ana life insurance. hii itapunguza michango ya kila siku
Kwa wale hawafahamu amounts ambazo hutajwa kama mchango kwenye shughuli hizi basi naomba niwape habari hii, UK £50, US $100 na kuendelea, sasa ndugu zangu, mwezi ukikaaa pabaya na wapendwa wengi wakakutangulia ujue kuwa mahesabu yako mwenyewe kujikimu hayatatimia. Kuna comment niliisoma kwenye blog ya jirani zetu wakenya, pendekezo lilikuwa paanzishwe mfuko wa hizi dharura, lakini contributors waliona kuwa huyu jamaa anatafuta capital aanze, sasa jamani wazo hapa pafanyike nini? wana-diaspora tupo wangapi? na suggestion hapo juu inaweza kutimizwa? Contributor hapo juu amesema kuhusu insurance, ndio watu tunalipa, na katika mazingira ya hapa kweli asilimia kubwa huwa wanalipa, lakini, sijawahi kusikia hata siku moja kwenye maombolezi kuwa mpendwa wetu alisha-sort-out hii ishu, (ukumbuke, insurance zingine hu-cover whole family and named dependents, lakini kimyaa!) watu mbio kuchangisha hii michango na kwa kweli si vizuri kabisa.
ReplyDeletekwa hiyo watu tusi-party eti sababu mtu atakufa. hata bongo mbona watu wana-party tena kwa michango hadi birthday na ubatizo watu wanachangasha, na kwenye misiba rambirambi siku hizi wanaweka ndoo kabisa siyo tena sahani....ponda mali kufa kwaja
ReplyDeleteAsante kwa ushauri ndugu. Wana ughaibuni tuna uwezo mzuri to wa kufikiri, usikondeshwe na michango yetu. To ushauri endelevu kwa watanganyika wanaotaabika kwa umasikini kila leo.
ReplyDeleteJust so so you know, since it sound like you do, NSSF inaanzisha mfuko wa insurance za magonjwa na vifo kwa wana ughaibuni in the next few months, stay tuned or you can visit NSSF website for details. Pia tunahimizana kuchukua life insurance.
Thanks for caring, if you really do (or maybe you're just bothered). In short we're working on it. Cheers!
Wote hao walioandika na wanaoongelea haya mambo utazania wanachangaga hata siku moja. Hebu waachieni wenyewe. Utajuaje walishafungua maumoja hayo na kujikuta hela zinapotea tu na siku ikitokea kitu hakuna tena heklla na hamna anayetaka kuchanga kwa vile wanajua kuna hela? Huwezi jua ya watu ni heri kuwa na hii michango mara kitu kinapotokea kuliko kuwa na makamati na watu kujikuta kula hela za umoja tu.
ReplyDeleteWakitangaza kama hutoi kitu sijui inakuuma nini kuona hilo tangazo na huko uliko?
Jamani kabla hujaguswa na kitu usifungue mdomo.
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza Life insurance hazikavi gharama za watu wengine ambao watachukua muda wao kufuatilia mambo yote.. Siku za kazi watakazo kaa nyumbani ujue kuna bills zinawangojea. Bills za huku hazijali kuwa ulikua kwenye msiba au ulikua umesafiri sasa kama watu wakisaidiana wakikutwa na mambo haya sijui ni nini nyie kina wauma...Think before you say something
Ndugu zangu watanganyika naona tunapenda kuongea au tuna computer mtu unapenda kubonyeza let me tell you something there are people make alot of money to sit down and push the button ok point iko hivi mtu akishafariki kwa sisi waislam tunasema inna lillah wa inalillah rajiun maana yake ni hakika sisi ni wa mwenyezi mungu na kwa hakika kwake ni sisi wenye kurejea hii pekee yake inatafsiri yake ukichambua pale unaposikia swala la msiba ni wito kwa kila mtu kulifahamu labda unamjua au humjui kama upo karibu hudhuria mazishi labda kuwe kuna masharti ndio usiende moja ambalo nashindwa kuelewa kuna mtu hapo juu anasema diaspoora something like that sidhani anauelevu mzuri kuhusu life insurance huyo wa tanzania namsamehe kwa sababu hajui alisemalo life insurance haitoki hapo hapo mtu akifa pili ndio maana hata hivi vyama wanavyofungua havifiki mbali kutokana na watu kama hao inakuwa ngumu sana kuendelea life insurance ni kama mirathi kwa sababu ni hela ya marehemu ambayo amefungua akaunti akifariki iwasaidie wale waliomtegemea husan mke au mtoto sasa basi ina maana nyie watanzania huko mtu akifa inauzwa nyumba ili ipatikane hela mtu akazikwe au inakuwaje mie nipo us watu wanachanga na wala hawaulizi hela ya insurance wala nn sina mengi
ReplyDeletethis goes to mdau anon wa october 4 10:21:00 PM - ina maana watu tunachanga kwa ajili ya kulipa bills za watu siyo kusafirisha maiti tena? na huo muda wanaochukua kufuatilia ni siku ngapi? basi kama ndo hivyo kila mtu akiumwa akakaa home siku kadhaa aombe mchango.
ReplyDeleteimekuwa kama ni wajibu kuchanga wakati wa misafiba. nakubali watu tunatakiwa kutoa rambirambi kama pole kwa familia, lakini hii ya kuwekeana viwango sidhani kama ni nzuri. mtu anajikuna pale anapoweza. myself i can't afford kutoa $100 na nikitoa chini ya hapo watanisimanga, so nimeamua sitatoa kabisa
tunashukuru mdau uliyetuma sisi ni wanadamu wakati mwingine watu tunakosa mawasiliano mimi nahitaji umoja huo kama upo e mail yangu makoyehayes@yahoo.com-washington dc naomba mawasiliano kwa wanabongo wenzangu,ila kupart ni sehemu ya life jamani kupunguza frasturation ok
ReplyDeleteTafadhalini kila mtu ukisoma hii habari hakikisha una Life insuarance ni pesa kidogo tu kwa mwezi ukilinganisha na matatizo yote. Tuwe tayari jamani hakuna atakae ishi milele. Mweleze na jirani yako na ndugu zako.
ReplyDeleteTafadhalini kila mtu ukisoma hii habari hakikisha una Life insuarance ni pesa kidogo tu kwa mwezi ukilinganisha na matatizo yote. Tuwe tayari jamani hakuna atakae ishi milele. Mweleze na jirani yako na ndugu zako.
ReplyDeleteTATIZO SI MICHANGO NI WATU FULANI KUJIFANYA WA MAANA KULIKO WENGINE UTAKUTA WAO WAKIFIWA WANATAKA MJI MZIMA USHIRIKI KWENYE MISIBA YAO UTADHANI ALIYEKUFA ANATUHUSU WAKATI WAKIFIWA JAMAA WENGINE WAO HAWATOKEI KABISA ILA UTAWAKUTA USIKU WAMECHOMEKEA KWENDA DISCO
ReplyDeleteUSHAURI WANGU NI KWAMBA KOMENI NA TABIA ZENU ZISIZO ZA MAANA HAKUNA MSIBA WA MAANA KULIKO MWINGINE VIKUNDI VYENU VYA KUCHOMA NYAMA MSICHANGANYE NA MISIBA LA SIVYO MGEOMBANA MICHANGO WENYEWE SI KUTUCHANGISHA KWA MATANGAZO YA EMAILS NA TEXTS WAKATI MISIBA MINGINE HAMFANYI HIVYO MNAKAA KIMYA KANA KWAMBA HAKUNA JAMBO LIMETOKEA.
SWALI LA KIZUSHI KWA WANA COLUMBUS JE HAWA WALIOKUFA WIKI HII NI WA MAANA KULIKO WALIOKUFA WA JAMAA WENGINE? KUMBUKENI HAKUNA MSIBA WA MAANA KULIKO MWINGINE LA SIVYO MUWE MNAJICHANGISHA WENYEWE NAFIKIRI MTAKUWA MMEJIFUNZA ENDELEENI KUHESABU SIKU MISIBA MINGINE INAKUJA
Mimi nafikiri wazo la mdau ni jema tu, wala hakuna haja ya kumsemea vibaya kwa waliofanya hivyo. Mara ngapi tumeona matangazo kuwa gharama ya kusafirisha mwili ni $ 15,000 (kwingine up to $ 25,000). Nafikiri si kazi ndogo kuchanga pesa hiyo kwa kudunduliza, nashauri mchukue ushauri huo au wowote unaofanana na huo...
ReplyDeleteKWELI TUPU FRANK ni aibu na fedheha kubwa sana kuchangisha michango ya misiba na kadhalika..
ReplyDeleteme pia nilikua najiuliza ivi kweli imeshindikana kabisa adi matangazo haya yabandikwe kutwa kuchwa michuzi blog???
big no n shame
ujumbe umefika
mjibebe
ReplyDeletembona hamzisemi balozi zenu zilizo ughaibuni.
ReplyDeletewanawajibika asilimia 100 kuangalia na kujali masilahi ya watanzania walio ughaibuni mbona mmewafumbia macho wakati wao ndo hasa waliatakiwa wawe msatari wa mbele kwa matukio kama hayo.
Mdau aliyosema kuhusu Life Insurance ana pointi kubwa sana.
ReplyDeleteLazima binadamu uone mbali sio tu kufanya kazi, kujenga nyumbani na kutanua. Kuna kifo pia. Wenzetu wananunua insurance na inalipa mahitaji yote ya gharama za kusafirisha maiti na kadhalika. Kama wanavyosema, si ghali sana, sana sana ni sawa na kreti moja la Bia ya Heineken (24 pack) kwa mwezi. Lakini utakuta mtu anajisahau na starehe halafu ndugu wanaombaomba akiondoka dunia ili azikwe nyumbani.
Mimi binafsi, sioni faida ya kuzikwa nyumbani japokuwa nina uwezo wa kuupeleka mwili wangu nyumbani katika insurance yangu ya maisha na dafrau.
Mimi nataka nichomwe Los Angeles. Hamna haja ya kuleta vilio eapoti na kuburuzwa nikiwa nimeshaoza na sipo tena duniani.
Maraha ni Pesa
USA (Karibu na Mungu)
waambie ukweli hao. kazi yao kutuma maoni ya matusi kama wavuta bangi. wenzenu tunajenga tz. nyie mnasubiri tuwachangie ili mrudishwe kwenye majeneza.
ReplyDeleteumesema kweli mdau. anzisheni vyama vya kuleta majeneza yenu home. hamtaki kuja kujenga nyumbani mnatujazia makaburi tu shenzi.
ReplyDeletenyie mnaotoa matusi ni wapumbavu. chukueni ushauri huo. tumechoka kuona matangazo ya kusafirisha majeneza. si mzikwe huko huko.
ReplyDeletemimi nawashangaa sana ndugu zangu miloko nje ya tanzania kila siku mnafungua matawi mapya ya ccm kama mnataka kuwa wana siasa basi rudini tu tz huko waacheni labour party ya akina tony brail tena nasikia kwenye party mnavaa nguo za bei kali kweli hadi $900 mbona mmejisahau mambo ya maana ni bora msi party mkawa na chama cha maafa ok
ReplyDeleteNa mkome kutuma matangazo ya kuombaomba toeni taarifa za msiba tu, na sio muanze kutembeza vibakuli dunia nzima sijui paypal nini, michango ya hali na mali, kwani wakati wa kujirusha hamjui kuna kufa mjiandae? mtatia akili na hatuchangi tena, starehe mle wenyewe shida zenu mtushirikishe, mtajiju
ReplyDeleteFYI - LIFE INSURANCE INA-COVER HADI SANDA NA MAZISHI KILA KITU. ILA WATU HUWA WANAJARIBU KU-MINIMIZE HIZO COSTS ILI HELA ZIBAKI NYINGI ZA MTAJI. MBONA HUSIKII HATA SIKU MOJA M-MAREKANI AKIFA WANACHANGISHA? WAMAREKANI HATA KWENYE MISIBA HAWALII MAANA NI WANATAJIRIKA MTU AKIFA.....KUFA KUFAANA OHOOO! BY THE WAY, COST YA KUSAFIRISHA MWILI SIYO ZAIDI YA $12,000 HIYO INAINCLUDE FUNERAL HOME ETC. SASA MIE HUWA NASHANGAA $25,000 INATOKAGA WAPI?
ReplyDeleteKaka Michuzi hii kitu ya "USHAURI WA BURE KWA WADAU WAISHIO UGHAIBUNI" iweke tena juu ili watu waijadili kuna watu wengi sana wenye dukuduku zao moyoni wanataka kutoa maoni yatakayo tusaidia kuondoa uombaji wa pesa pindi tupatwapo na matatizo
ReplyDeleteThanks Mdau
koments nyingi zimejaa chuki za moyoni mbona wabongo mnachuki kiasi hicho kunaubaya gani mtu kuchangisha kwa mtandao mbona huko bongo mnachangisha si ni yaleyale tu acheni chuki hazitowapeleka popote.
ReplyDeletechuku chuki mpaka mmekuwa vipofu hamjistukii
nawaona ni kama wachawi tu,
walosi ,wanga, vigagula hamna tofauti nao.
msifikili huku ugaibuni sisi tumeukata tunatafuta maisha tsikumoja wewe au mwanao atakuja kusoma au kufanya kazi kama wewe hauko huku.
chuki chuki chuki tuuuuu
kalaga bahoo mtalost mkiendekeza chuki kiasi hicho.