

Picha zote na Mohammed Mhina.
Wizara ya Katiba na Sheria leo imetiliana saini na kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Company Ltd kutoka China kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST).
Ujenzi huo wenye thamani ya aidi ya shilingi bilioni 16 unafanyika jijini Dar es Salaam kupitia Programu ya Maboresho ya Sekta ya Sheria (LSRP) kwa thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 16.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Oliver Mhaiki alisema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika baada ya miezi 15.
Katibu Mkuu huyo aliitaka kampuni hiyo kuhakikisha kuwa ujenzi huo unakamilika kwa wakati na kiwango kama ilivyokusudiwa ili kuondokana na changamoto zinazoikumba Taasisi hiyo kutokana na kutokuwa na majengo ya kudumu.
Kwa sasa Taasisi hiyo inaendesha mafunzo yake kwa kutumia majengo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati ikisubiri ujenzi wa majengo yake ukamilike.
Akiongea katika hafla hiyo fupi, Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Gerald Ndika alisema ujenzi huo unatarajiwa kujumuisha majengo ya kisasa vikiwemo vyumba vya madarasa, maktaba, nyumba za watumishi, hosteli na vyumba vya mahakama vya mazoezi.
“Hii itaifanya taasisi kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria sheria kwa ufanisi zaidi na hivyo kutimiza ile azma ya kutoa mafunzo sahihi ya vitendo,” alisema Dkt. Ndika.
“Baada ya kukamilika, wanafunzi wetu wataruhusiwa kutoa huduma za kisheria Mahakamani kwa wateja chini ya usimamizi wa wanasheria wazoefu,” alisema za Dkt. Ndika na kuongeza kuwa udahili wa wanafunzi unatarajiwa kuongezeka kutoka wastani wa 300 wa sasa hadi 1,000 kwa mwaka, alisema.
Kwa mujibu wa Dkt. Ndika, Taasisi hiyo pia inatarajia kujenga kituo cha kutoa elimu ya sheria kwa watendaji wakiwemo Mawakili, Mahakimu na Maafisa Sheria kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wao.
Akizungumza kabla ya utiaji saini wa mkataba huo, Mratibu wa LSRP Bw. Juvenalis Motete, alisema taratibu zote za kisheria zilifuatwa katika mchakato wa kumpata mkandarasi ikiwemo makataba huo kupitiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aliongeza kuwa mchakato wa kumpata mkandarasi huyo ulianza mwezi Mei mwaka huu na jumla ya wakandarasi 17 kutoka ndani na nje ya nchi waliomba kazi hiyo kabla ya kuchujwa na kufikia sita na baadaye kupatikana kampuni ya BCEG.
LST ilianzishwa mwaka 2007 ili, pamoja na mambo mengine, kutoa mafunzo ya mwaka mmoja ya uanasheria kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya sheria wanaotarajia kuwa Mawakili binafsi au watumishi wa umma wanaotarajia kufanya kazi za kisheria.
DO WE REALLY NEED TO CONTRACT A CHINESE COMPANY TO DO SUCH A JOB. DON'T WE HAVE COMPETENT TANZANIAN COMPANIES THAT COULD UNDERTAKE SUCH A SIMPLE ASSIGNMENT?? I WONDER WHAT IS WRONG WITH OUR SYSTEM OF GOVERNANCE? UNLESS WE UNDERTAKE SUCH JOBS, OUR PEOPLE WILL CONTINUE LIVING IN ABJECT POVERTY
ReplyDeletejengo litakuwa wapi? ili kupunguza msongamano wa magari ilibidi liwe nje kidogo ya city center..
ReplyDeleteWell tupo na tumefanya kazi kubwa kujenge magorofa pande zote za bahari ya atilantic na kwinineko, lakini huwezi kupata kazi hata moja kwenye nchi yetu. Inasikitisha sana kwani ni mpaka ujumue mtu na siyo kwamba unafanya kwa proud ya kuwa unajenga nchi yako. Na ukimjuwa huyo mtu ni mapaka mgawane nusu kwanusu. Sasa sisi watoto wa wakulima ambao hatuna connection huwezi hata kupata kazi ya kujenge banda la kuku. Na kama hizo kazi zipo kweli tunaomba zitangazwe kila mahali ili watanzania tuojuwa tunauwezo wa kujenge majumba ya kisasa tuzifanya hizo kazi. Sasa tulipata shule ya bure kuanzia msingi mapaka chuo, leo hii huwezi kupata kazi ya kulijenge Taifa lako na ujuzi unao na utaishia kwenda kaburini na ujuzi wako wa Technologia ya sasa. Sasa kwa nini bado unapeleka watu shule serikali inalipa mamilioni na wakati huohuo unaagiza wachina waje waje wajenge. Kumbuka hao ni wachina wa sasa hawaji kujenge tu wankuja na mambo yao ya zaidi. Akiwa pale najenga ameashatumwa kufanya mamabo mengine. Michuzi usinanie hii.
ReplyDeleteJana nilikutana na mtu anaelekea uturuki akawa ananieleza kwamba ukienda kuchukua viza ya uturuki unaambiwa lazima ulete booking ya turkish airlines, yaani wanakulazimisha kupanda ndege ya kwao. sisi tuendelee tu kuwanufaisha wengine tukijifanya champions of free market economy.
ReplyDeleteWee mtoa maoni wa kwanza sio kupenda kupinga kila kitu na kuleta uzawa wako uchwara,hao wachina ndo wameonekana wana uwezo ndo maana wamepewa hiyo kazi na sio siri hakuna asiye jua kazi za mchina zilivyo bomba ,angalia uwanja wa taifa ,ambao mnashindwa hata kutumia vifaa walivyoweka na mnavunja viti na kukojolea kwenye masinki badala ya chooni,umeambiwa kampuni zilizoomba zilikuwa kumi na saba zikachujwa zikabaki sita na kati ya hao sita akapatikana huyo mchina sasa wewe unapiga domo tu,unalalamika nini ilihali nafasi ya hao ndugu zako kuomba ilikuwepo? tatizo la wabongo sasa tunapenda sana kulaumu kuliko kutafakari na kujishughulisha, hao makandarasi wa kibongo ni mda mrefu sasa toka john Magufuli awashauri kwamba wawe wanaungana zinapotokea kazi kubwa ili waweze kuunganisha nguvu na wapewe tenda na wajenge taifa lao wenyewe lakini sidhani kama walishafanyia kazi ushauri huo, kwani aliwaambia mitaji yao ni midogo lakini wakiunganisha nguvu na ujuzi wataweza kupata kazi kiurahisi kwani watakuwa na uwezo wa kushindana na kampuni za nje zenye mitaji mikubwa na ujuzi wa kazi kuliko kwenda mmoja mmoja hiyo itakuwa ngumu kwao kushindana na kampuni za nje kwani zina ujuzi mkubwa uzoefu na pesa nyingi, tuamke wabongo tusiishie kulaumu na kulalamika ushauri tulishapewa je? tumeufanyia kazi kiasi gani? kwani makandarasi wetu wakishirikiana pamoja hata benki zitakuwa tayari kutoa mikopo kwa mradi mikubwa kama hiyo.
ReplyDeleteam sooo angry kwa kuona hivi..Tanzania we never learn,as long as kuna cha juu watu hao!hivi barabara ya sam nujoma si wachina..this is bogus!!..kuna kampuni nyingi tu za first class Tanzania ambazo zinaweza fanya one hell of a good job...TANZANIA ITS TIME TO WAKE UP!!!...
ReplyDeleteDear Sir,
ReplyDeleteDo you know that we don’t have one Tanzanian contractor abroad? Kuna mama mmoja aliniambia kwamba yeye ni mkandarasi huko Ulaya nikajagundua alikuwa anashona foronya.
We don’t have any known Tanzania contactor in China.
That is the reason I would wish for such jobs even if you think 16bn is a bit big for our people, the works be divided into 4pcs of 4bn each and be given to four or five local contractors with stringent controls.
We don’t Need Chinese Companies for these sorts of Jobs. We Have Competent Tanzanian Companies That Can Undertake Such works. At least a few are good.
Mheshimiwa Katibu mkuu, Huu siyo ubaguzi ni uzalendo tu.
Mkuu wa kazi, kiongozi...heshima yako
ReplyDeleteishu hapa ni law school,siyo jengo!!!ingawa step moja mbele,but bado mambo ya kuwatumia watu wa nje,wachina ni upumbavu wetu,na kama hakuna ulaji hapo nitashangaa sana...
ReplyDeleteSasa nyie wadau mna lia nini. nyie mna peza hizo za kujenga , pesa za wachina mnakopeshwa na mnaambiwa mtumie kwa makampuni yao. tulizeni ball watu wamesha katiwa chao ,msione watu wanakenua meno tu kwenye picha wanayao moyoni
ReplyDeleteits pity!
ReplyDeleteJamaa wa pili kauliza jengo litakuwa wapi...tumeambiwa litakuwa barabara ya Sam Nujoma, nyuma ya jengo la TCRA...nadhani foleni itapungua kama alivyosema. Kuna mshkaji pia kadai kuna issue ya uzalendo inatakiwa kusukumwa...tatizo letu longolongo na kutojifunza, Magufuli alishawashauri, tunajidai tunajua...haya tuendeleaa na kiburi na umimi. Pili, nafahamu hizo fedha kama zinatoka LSRP, hii ni programu ambapo fedha zake zipo katika kapu a.k.a wadu mbalimbali wakiwemo Banki ya Dunia na Serikali inaweka fedha ili kuboresha sekta ya sheria...kama ni hivyo, WB haiwezi kukubali apewe mshenzi tu eti kwa sababu ni mweusi, vigezo vinawekwa na kazi inatangazwa kitaifa na kimataifa including katika mtandao wa WB...sasa Wachina wamejipanga wakawapiga chini kampuni nyingine 15 na kukamata kazi tunaanza longolongo tena hata bila ushahidi...cha msingi wahandisi wa Bongo wakubali kuunganisha nguvu na wafanye kazi ya viwango...ukitaka kujua hawa jamaa waliopata kazi ni wazuri uliza wameshawahi kufanya kazi gani na sasa hivi wanafanya kazi gani...tufanye utafiti kabla ya kuongea..
ReplyDeleteCheck progress hapa:
ReplyDeletehttp://www.dullonet.com/2012/03/06/law-school-wajenga-jengo-lao/
http://lukwangule.blogspot.com/2012/03/wajumbe-bodi-ya-zabuni-wizara-ya-sheria.html