
Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa akiongea na vyombo vya habari wakati wa kuonyesha magari 30 kati ya magari 100 yanayotolewa kwa washindi wanaoshiriki shindano la shinda Mkoko linaloendeshwa na kampuni hiyo tangia tarehe 2 mwezi wa nane na mpaka sasa magari yamebaki 15 yakiwa tayari kwa kunyakuliwa na mteja yeyote Yule wa Vodacom Tanzania.

Askari wa Usalama Barabarani akielekeza magari hayo kuingia katika eneo la kuegesha lililopo kwenye ofisi za Kampuni ya kuuza magari ya FK Motors jijini Dar es salaam leo.

Magari aina ya Hyundai I10 yanayotolewa na kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania katika shindano lake la kila siku la Shinda Mkoko yakiwa katika msururu wakati yalipokuwa yakipelekwa katika maegesho yaliyopo kwenye kampuni ya kuuza magari ya FK Motors iliyopo barabara ya Nyerere.
hii ni kufuru sasa... kipindi cha miaka mitano ya mkwere waliofaidi ni mashostito , naona voda inavyopeta , rostam nawasilisha mada
ReplyDeleteKwa foleni za magari zilizopo tanzania hasa dar, bado makampuni yanazidi kuleta magari nchini. Hii inasaidia nini katika kuondoa tatizo la foleni barabarani? pia kuna suali la mazingira. Anyway hapa tanzania bwana!
ReplyDeleteMmmmmmh!
ReplyDelete"Baby Walkers!"
Khaah!
Naomba personal email/simu ya Rukia Mtingwa
ReplyDeleteJamani Voda mkoje....hata mimi naitaka hyundai I10 lakini kwa nini sina bahati?
ReplyDeletenimejaribu wee lakini wapi...hola..yaani zitaisha hivhivi bila mimi kupata?
VODA WANGETOA PIA NA ZAWADI ZA MABASI MAKUBWA YANGEWANUFAISHA WASHINDI KWA KUPATA KIPATO HATA CHA KUWEZA KUNUNUA USAFIRI MDOGOMDOGO BINAFSI NA MABASI HAYO KUNUFAISHA ABIRIA WA JIJI LA DAR NA KWINGINEKO MIKOANI WANAOTAABIKA KUTOKANA NA SHIDA ZA USAFIRI WA PUBLIC HAPA TZ.
ReplyDeleteJamani Voda, mie nimecheza mpaka sasa nina pointi milioni tisa na nusu. Je, ni nini kinanifanya nikose? Na kila siku lazima niziamshe pointi zangu, ikifika saa nne na nusu usiku nakaa macho nikisubiria simu yangu labda leo itaita lakini wapi. Ningetoa ushauri wa bure tu kwa Voda, wajaribu kuwafikiria na wachezaji ambao walicheza tokea mwanzo hadi mwisho na wana pointi nyingi kama mimi lakini bahati ya kushinda hawana.
ReplyDeleteJamani Voda mimi mpaka sasa nina pointi milioni tisa na nusu lakini kila siku nasubiria kupigiwa simu bila mafanikio. Ushauri wangu ni kuwa mngeangalia wale walio na pointi nyingi tufutwe machozi. Kila siku najibu maswali siku nyingine natumia hata shilingi elfu ishirini na tano. Nioneeni huruma jamani.
ReplyDelete