JK akiingia kwenye uwanja wa michezo Karatu Mjini tayari kuanza mkutano wa kampeni Karatu leo
Waziri mkuu mstaafu Mh. Frederick Sumaye alikuwepo Karatu kimpigia chapuo JK na wagombea wengine wa CCM nafasi za ubunge na udiwani leo.

kwa picha zaidi
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. JK anataka vunja ngome ya adui mkubwa! Naona half a budget imemwagwa huku!

    ReplyDelete
  2. atleast kwa shingo upande sumaye ameingia ulingoni dakika za mwisho kwa aibu ila atakuja wajibika kwa kanisa kwa kumpigia debe mtoto wa saigoni.

    Michuzi usibane ntakupiga albadir.

    ZAUNUNU-AMSTERDAM

    ReplyDelete
  3. Lazima CCM na mafisadi wote wang'oke tarehe 31.
    Slaa oye!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete, jana alilazimika kukusanya watu kwa mabasi kutoka Arusha mjini kwenda wilayani Karatu kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wake wa kampeni.

    http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=20484

    ReplyDelete
  5. Kuna watu wanafikiri kuwa eti Slaa ndiye mfalme Karatu. Si kweli! Yeye hajatuwakilisha hata kidogo katika miaka 10 alipokuwa mbunge wetu. Ametaka tu kututumia sisi kama ngazi yake ya kufikia malengo yake ya uchu wa madaraka. Sishangai wananchi hapa Karatu kutomuamini Slaa.

    ReplyDelete
  6. CCM imara; wanaotukana waendelee kutukana. Mwamuzi ni mpiga kura. Mungu ibariki Tanzania! Mungu ibariki CCM na msimamo wako wa umoja wa Watanzania woooooote!

    ReplyDelete
  7. Wala usihofu. Watu unaowaona hapo ni wale wale uliowaona Arusha mjini, Moshi, Singida, Dar kuna malori yanasomba watu usiku na mchana na wengine wanaenda kuwaona akina masanja na joti.

    ReplyDelete
  8. nani asiyejua mabus matatu yalijazwa watu wa kwenda kumsikiliza kutoka arusha na ndio wanavyofanya kila mahali so hamna uhalisia .michu dont b bias usibanie tafdhali sana

    ReplyDelete
  9. KWANINI MHESHIMIWA HATAKI MASWALI TOKA KWA WAPIGA KURA WAKE? anawaogopa nini?

    ReplyDelete
  10. Bura TluwayOctober 26, 2010

    Nyie watu JK alienda Mangola na Karatu mjini. Na kote watu walifurika. Kwa taarifa yenu Kata ziko 14 ambako kote kuna binadamu wanaopiga kura. Ukiacha Kata ya Karatu mjini kama inavyoitwa kata zilizobakia JK mambo yake ni mazuri sana. Ninawaambieni subirini kupigwa na mshangao baada ya 31 Oktoba kwa jinsi JK atakavyombamiza Slaa. Sisi watu wa KAratu miaka yote CCM hushinda kwa sababu CCM inakubalika ila mle ndani ya chumba cha kuhesabia kura hujuma hufanyika. Safari hii tutawabana kisawasawa. Nyinyi subirini tu.

    ReplyDelete
  11. hesabu rahisi sana coaster 3 mara 25 ni 75 je watu hao ni sabini na tano ? lakini pia arusha kwenyewe hakujai namna hiyo ukweli ni kwamba karatu wamemchoka slaa walichotaka ni chaguo lao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...