Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe akiendesha harambee ya kumchangia fedha za kuweka mawakala wa mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Mwalimu Norbart Yamsebo (chadema) ,katiba harambee hiyo zaidi ya shilingi 800,000 zilipatikana huku yeye Kabwe akiuza kwa manadi kombati yake iliyonunuliwa kwa shilingi 200,000
Bw Zitto Kabwe akiendesha harambee ya kumchangia fedha za kuweka mawakala wa mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini Mwalimu Norbart Yamsebo (chadema)
Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe( kulia) akisaidia kuhesabu fedha zilizochangwa jana katika viwanja vya mkutano wa kapeni vya Sumbawanga mjini wakati wa kampeni zake
Maelfu ya wananchi wa jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa wakimsikiliza naiu katibu mkuu Taifa wa Chadema Zitto kabwe wakati akimnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo Mwalimu Norbart Yamsebo ( Chadema) katika kampeni zake mkoani Rukwa jana
Askari polisi ,magereza na mgambo wakilinda mkutano wa kampeni za Chadema ambao alikuwa akihutubia naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe jana viwanja vya Sumbawanga mjini
Naibu katibu kuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema)Taifa Bw Zitto Kabwe (kulia) akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini mkoani Rukwa Mwalimu Norbart Yamsebo jana wakati wa kampeni za Chadema mjini Sumbawanga. Picha zote na Francis Godwin






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Uncle, nakupa hongera leo umeweka picha za kutosha nadhani sasa umeanza kuyakubali mambo.Asante sana na mbona picha za akina Dovotwa, Rungwe, Peter Mziray na Mutamwega hutuwekei.

    ReplyDelete
  2. Kazi nzuri Zitto unaupendo wa mshumaa vipi jimbo lakao

    ReplyDelete
  3. Oh my God! Kama mzee Yamsebo amegombea ubunge Sumbawanga, basi CCM wasahahu hicho kiti. Na hivi mzee Kimiti amestaafu, basi jimbo ni la CHADEMA. Mzee Yamsebo ni mtu mwadilifu, amekuwa mkuu wa shule za Mazwi, Kantalamba high school, na mwenyekiti wa Wakuu wa shule za sekondari Tanzania wakai fulani. Nimefanya naye kazi nikiwa Teaching Practice shuleni kwake, nikajifunza uadilifu alio nao huyu mzee. Ni mtu asiyejua kujidai kwa madaraka aliyonayo, na anajua kupanga mambo. Sumbawanga wakimkosa huyu mzee, watajutia.

    Mungu ibariki Tanzania.
    Tuchague kiongozi bora, na siyo chama.
    Mdau,
    USA.

    ReplyDelete
  4. Picha za chadema unapiga close up (kwa ukaribu) ili tusione idadi kubwa ya watu waliohudhuria, mwaka huu kaka umetia aibu sana...Ndo uhandishi wa habari sahihi kwa nchi yetu huu, jitahidi zaidi na zaidi, Slaa akiingia madarakani imekula kwako...

    ReplyDelete
  5. Wingi wa hizo jero jero (500/=) unaonyesha kuwa wa-TZ wengi ni wa hali ya chini. Hapo ndio wamejitolea mpaka mwisho wa uwezo wao!!!

    ReplyDelete
  6. Wanachadema akili zao hazina akili picha za Chadema mkiwekewa mnapinga msispowekewa mnalalamika nyie hamnazo kweli ila wee Mithupu mbona unabania picha za CUF na TLP?n.k

    ReplyDelete
  7. Yamsebo hupiti ng'oo, hata akiwanga usiku hatumchagui. Fipason.

    ReplyDelete
  8. Hivi nyie CHADEMA vipi? Unamtoa mzee Kimiti halafu mnamleta mzee mwingine? Vijana wa Sumbawanga hatumpi huyo. CCM OYEE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...