Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza (kushoto) akiwasisitiza jambo baadhi ya wanafunzi ambao shule zao zilikabidhiwa msaada wa madawati wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 300 yenye thamani ya milioni 18.2 kwa shule 12 ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya jamii inayoandaliwa na benki hiyo kila mwaka kwa lengo la kuisaidia jamii inayowazunguka. Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania Christina Manyenye (kushoto) akiwasisitiza baadhi ya wanafunzi ambao shule zao zimekabidhiwa madawati kuyatunza ili yadumu mara wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 300 yenye thamani ya milioni 18.2 kwa shule 12 ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya jamii inayoandaliwa na benki hiyo kila mwaka kwa lengo la kuisaidia jamii inayowazunguka.

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mwantumu Mahiza amekabidhi madawati 300 yenye thamani ya milioni 18.2/- yaliyotolewa na benki ya KCB Tanzania kwa shule 12 nchini na kusema anaondoka akijua bado shule nyingi zinakabiliwa na changamoto hiyo.

Shule saba zilizopatiwa msaada huo kwa awamu ya kwanza ni shule za msingi Mwanambaya madawati (15), Makuburi (30), Ruvuma(15) na Ali Hassan Mwinyi(15), shule za sekondari Hekima(30) na Msangani (30) pamoja na shule ya chekechea na msingi ya Bibi Jane (15). Awamu ya pili itakuwa kwa mikoa ya Arusha, Mwanza, Morogoro na Zanzibar.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Naibu waziri huyo alisema upungufu wa madawati ni tatizo linazozikabili manispaa nyingi nchini na serikali kwa ujumla hivyo kuzitaka kuongeza juhudi katika kulimaliza tatizo hilo ambalo linawezekana hata kwa kuwahusisha wazazi wa wanafunzi.

Akifafanua alibainisha kwamba ikiwa KCB Tanzania imeweza kutengeneza madawati kumi kwa kiasi cha milioni 1.5 iweke manispaa zishindwe wakati zikiwa na rasilimali tofauti ikiwemo rasilimali watu, miradi na mali.

“Kwa hili lililofikiwa leo nazishauri manispaa kujifunza na kuiga mfano huu wa KCB Tanzania wakati wakitumia changamoto hoi kujiuliza kwa nini taasisi hoi ya kifedha imeweza nao wanashindwa jambo litakalozibadilisha kifikra na kuleta maendeleo kwa jamii,” alisema Mahiza.

Mbali na hayo akizungumzia umuhimu wa msaada huo alisema ni urithi mzuri kwani utaweza kutumiwa kwa vizazi na vizazi tofauti Kama wangetoa madaftari ambayo yangeweza kutumiwa na mtoto mmojawapo peke yake.

Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwaasa walimu kuitangaza benki hiyo kwa wazazi wa wanafunzi na jamii kwa ujumla pia kuyatunza madawati hayo ili kuwapa moya wahisani wengine kuendelea kuzichangia shule hizo. Ambapo kwa upande wa wanafunzi aliwataka kuyatumia kwa kujiletea maendeleo katika masomo yao.

Awali Mwenyekiti wa Bodi wa KCB Tanzania Dk Edmund Mndolwa alisema kuwa katika kuadhimisha wiki ya jamii wametoa msaada huo kwenye sekta ya elimu ikiwa ni kawaida yao na kwamba kwa mwaka jana waliichagua sekta ya mazingira na mwakani wamependekeza kuwekeza kwenye sekta ya afya.

Dk Mndolwa alisema wanaendesha shughuli zao kwa umakini na kwa kuzingatia wajibu wao wa kusaidia jamii inayowazunguka. Aidha mbali ya shughuli za kibenki wanatoa misaada mbalimbali ili kupunguza umaskini hususani kwenye sekta ya elimu, afya, mazingira na maafa mbalimbali.

Kwa sasa benki hiyo ndiyo kubwa zaidi Afrika Mashariki ikiwa na matawi 200 na rasilimali. Ina mashine za kutolea fedha (ATM) zaidi ya 400 na mtandao unaozifikia nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mi nadhani kipau mbele cha haya madawati kingekuwa kwenye shule za vijijini kwani ndiko kwenye shida ya ukweli. Kwa shule za Dar nafikiri kinachofanyika ni kubadilisha madawati yaliyochafuka kwa mapya wakati kuna shule hata hayo madawati yaliyochafuka hawana.
    Hao watoa misaada waangalie shule zilizopo vijijini ili misaada yao iwe na manufaa zaidi.

    Ingawa wanasema hii ni awamu ya kwanza sidhani kama watarudi hivi karibuni kutoa tena huo msaada. Wangeanza na vijijini hawa wa Dar es Salaam wakasubiri.

    ReplyDelete
  2. Dk.Mndolwa kwwanza Shikamoo na hongera kwa msaada kwa jamii.
    Mimi nawaomba kwa dhati ya moyo wangu mjenge jina lenu Tanzania kwa kuibadilisha manzese...manzese tu ikawa kamji ka mfano kenye mitaa ya kisawasawa na barabara za uhakiak. Najua ni gharama na mradi wa muda mrefu lakini nina hakika Prof Tibaijuka atawasaidia vijisenti kutoka UNHABITAT..walau tukiwa angani tuone kamji kalikopangiliwa hata mkikapa jina la KCB haijalishi

    ReplyDelete
  3. Mambo haya hushangaza sana! Waziri wa elimu na watoa misaada mawazo yote yako Dar tu, tena utakuta shule iliyopewa msaada ina madawati kibao eti yanatolewa ya zamani yanawekwa hayo mapya. Mkumbuke kuna watoto vijijini hawajui hata dawati linaonekanaje. Viongozi wetu muwe na upeo wa kitaifa zaifa ninyi sio mawaziri wa Dar es Salaam ni wa nchi ya Tanzania. Ndiyo maana kiongozi wa nchi anaulizwa swali la afya linalohusu nchi nzima yeye anaongelea kuboreshwa kwa Muhimbili! je ni wananchi wangapi wanaweza kusafiri kutoka pembezoni mwa nchi kuja kupata matibabu Muhimbili?
    Ni kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  4. Mzee....CSR(Corporate Social Responsibility)....depiction....
    Mdau(John)UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...