Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mkurugenzi wa kampuni ya Labiofam, Dk. Jose Carlos wakitia saini mkataba wa utekelezaji wa mpango wa kudhibiti mazalia ya mbu wenye thamani ya Tsh bilioni 2.9, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kutokomeza ugonjwa wa malaria katika jiji la Dar es Salaam. Mpango huo ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha dawa ya kudhibiti mazalia ya mbu kinachotarajiwa kujengwa Kibaha, mkoa wa Pwani. Picha na mdau Magreth Kinabo- Maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi na wadau kuna hii mpya ambayo bado haijapenya kwa wengi. Ni hivi kuhusu Malaria Afrika au Tanzania tunajisumbua tu kwani wapo watu wanaendesha maisha yao kwa kukubali ugonjwa huo uendelee kuwapo nchini. Kuna wazungu walikuja nchini na dawa zao za kunyunyiza angani kwa Helkopta lakini ilikataliwa na wahusika. Hiyo dawa ilikuwa inaua kabisa mayai ya mbu hote nchini na utafiti uliwahi kufanyika huko Mahenge (kunakosemekana kuna mbu sugu) na hata kwa wale mbu wa kupandikizwa pale Muhimbili wote walikufa na mayai yao yote (waliwekwa mahabara). Wazungu hao walipotakiwa kuhalalisha madhara ya dawa hiyo walijieleza hadi wakailamba ili kuthibitisha kama aina madhara kwa wanadamu. Dawa hiyo ingekua inanyunyizwa angani na ndege au helkopta ili kuua makazi ya mbu kote nchini na hakika Malaria ingeisha nchini. Ajabu wazungu hao wakaambiwa eti wataje 'formula' ya kutengeza dawa hiyo jamaa wakachomoa maana walitaka kuchezewa chezo la mwaka. Jamaa ikabidi waondoke kimya kimya nchini na kurudi kwao. Sasa kuna maslahi yaliingia hasa kwa watengenezaji wa dawa za Malaria na vyandarua. Wadau wengine wenye data wanaweza kuzimwaga hapa. Muhimu hakuna mtu aliyemakini kuhakikisha Malaria inakwisha nchini. NAWASILISHA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...