Marehemu Fatuma Kihombo
(kulia mwenye kofia ) akikagua timu

Na Francis Godwin
Aliyekuwa katibu wa madiwani wa chama cha mapinduzi (CCM) na mjumbe wa kamati ya utendaji wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa (IRFA) Fatuma Kihombo(51) amefariki dunia.

Pamoja na kifo cha kiongozi huyo wa soka kuacha pigo kubwa ndani ya chama cha soka mkoa wa Iringa ila bado kimeendelea kuwa ni kubwa ndani ya CCM jimbo la Iringa mjini .

Katibu mtendaji wa IRFA Eliud Mvela alisema kuwa Kihombo alikuwa ni mdau mkubwa wa soka katika mkoa wa Iringa na enzi za uhai wake alipata kuwa mjumbe wakamati ya utendaji akiwakilisha wanawake katika chama nafasi hiyo.

Pia moja kati ya kazi ambayo amepata kuifanya ni kuhamasisha soka la wanawake ndani ya mkoa wa Iringa na kuwa pamoja na nafasi yake kutafutiwa mtu wa kujaza ila bado pengo lake halitazibika.

Kifo cha diwani huyo kimeendelea kuwa pigo kubwa ndani ya CCM jimbo la Iringa mjini ukiacha pigo kubwa lililotokea Octoba 31 baada ya kupoteza jimbo hilo na kuangukia mikononi mwa chama cha Demokrasia na maendeleo (chadema).

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa mjini Abed Kiponza alimweleza wandishi wa habari hizi kuwa CCM wilaya ya Iringa mjini imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha diwani huyo na kada maarufu wa CCM mkoa na wilaya hiyo.

Alisema kuwa kabla ya kifo chake Kihombo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Maralia na kulazwa kwa muda wa siku tatu katika Hospitali ya mkoa wa Iringa kabla ya jana usiku kufariki dunia .

Pia alisema nafasi nyingi alizopata kuzitumikia ni pamoja na mjumbe wa baraza la utekelezaji wilaya na nafasi nyingi ndani ya CCM kata na wilaya.

Kiponza alisema kuwa CCM imempoteza kada maarufa katika siasa za ndani ya chama huku kwa upande wake aliyekuwa mstahiki meya katika baraza la madiwani lililopita na diwani wa kata ya Mlandege Aman Mwamwindi ameeleza kusikitishwa na kifo cha diwani huyo na katibu huyu wa madiwani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nimesikitishwa sana na msiba huu. Ikumbukwe pia kuwa FAtuma alikuwa mchezaji mahiri sana wa netiboli alipokuwa msichana. Miaka ya 70 Alikuwa akichezea timu ya Nyanda za juu Kusini, moja ya timu bora sana enzi hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...