Habari Ankal Michuzi,

Katika pita pita zangu huko mikoani,nilibahatika kukutana na hii njiani kuelekea Songe Kilindi Tanga ni kilometa zaidi ya mia moja kutoka makao makuu ya wilaya ya handeni, imenifurahisha sana maana yake dish ni kubwa kuliko paa ya nyumba, na tv wanaangalia kwa kutumia battery ya Gari .

hebu wape wadau wapate kuosha vinywa vyao kidogo.

Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. bongo sasa tunaendelea kwa tekelinakujia nyie wabeba rudini pia, tunapata net kwa satelaiti dish sie. speed ni soft toch.

    ReplyDelete
  2. Kwa wapenda maendeleo ta teknohama, sio ajabu wanamfahamu mchambuzi wa mambo ya jamii, Alvin Toffler (m-Ameika), ambaye aliwahi kubainisha maendeleo ya kuwasiliana kwa kutumia lugha ya "mawimbi matatu” katika kitabu chake kinachozingatia Wimbi la Tatu (The Third Wave, 1980), kama ifuatavyo:

    (a) Orality (mdomo na symbols) utegemezi wa nguvu zetu na za wanyama, moto, jua, maji na upepo, kama zilivyo nchi nyingi zinazoendelea. (b) Print/photo na simu ya upepo/telephone utegemezi uliotokana na viwanda (kusoma na kuandika). (c) Digital or instatenenous communication utegemezi wa teknohama: radio, luninga na komputa) .

    Alvin anaamini kuwa nchi zinazoendelea, kwa mfano, Tanzania, hazina haja ya kugundua gurudumu la mapinduzi ya kuwasiliana. Zinaweza kabisa kuvuka wimbi la b na kuingia wimbi la c, kama hiyo picha inavyoonyesha hapo juu – kama si la kukoga tu (samahani).

    Alvin anatoa mfano wa Ghadhi and Satellite: Nchi zinazoendelea zinaweza kujiunga na nchi zilizoendelea katika njanja ya mawasialiano bila wasiwasi. (Ghandi ni fano tu wa maisha ya kutotaka sana kukoga na vya usasa).

    (“The illiterate of the 21st century will not be those who cannot read and write, but those who cannot learn, unlearn, and relearn.) – Alvin Toffler.

    ReplyDelete
  3. ama anakinga nvua pindi zinaponyesha au ni paa la nyumba na kama sivyo anaonyesha kuwa la angekuwa na uwezo pia angependa kuwa na ungoz.nasuuza kinywa teh teh teh

    ReplyDelete
  4. .....Hii ni ya "kuzuia kabisa" watu hawa wataanza ubishi na kuhoji hoji kama watu wa mjini,......wanaweza kuhatarisha hata maisha ya mbunge wao! (sijui nimesomeka?)

    ReplyDelete
  5. huyu mtu ana akili sana,taswira ya kijiji inaonesha wapo out of touch with the real world,Hilo dish litawafunza mengi sana kuhusu dunia na kids hawatakuwa na one ambition ya ku own a lots of cattles and many many wifes,ila watakuwa na variety ambitions ambazo zitasaidia kuleta maendeleo.Well done.

    ReplyDelete
  6. masikini akipata matako hulia bwata!

    Mbuzi wa masikini hazai!

    Masikini akipata husingiziwa kaiba!

    ReplyDelete
  7. MPANGO MZIMA....

    ReplyDelete
  8. SAFI SANA
    HUYO ANAYESEMA WABEBA MABOX WARUDI KWANI ULIWAPELEKA WEWE?

    GO ON WITH YOUR LIFE, TUNATAFUTA MAISHA YETU KWA FAMILIA ZETU. HATUKUHUSU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...