Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Kingereza kinamsumbua sana,hapo nimegundua tofauti ya kingereza cha mtanzania msomi na kingereza cha mazoea.

    ReplyDelete
  2. hahahaha....ulaya kweli kugumu.....kama disco basi mtu hachagui wimbo wa kwenda kucheza.....blue, reggae, chacha, salsa, bolingo.......zote unacheza...

    ukichagua chagua shauri yako....utaondoka bila kucheza wimbo hata mmoja..maana wimbo unaoutaka unaweza usipigwe na dj mwanzo hadi mwisho.

    Kwahiyo mpira basi kwishne....

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa kanivunja mbavu sana, eti white people singing bushman song ;) lol

    ReplyDelete
  4. JAMANI KAMA HAUWEZI KUIMBA SI UACHE TUUU!!! UNATUAIBISHA WATANZANIA...NA UNANYONGA MIZIKI YA WENGINE!

    ReplyDelete
  5. mbwegelembwegeleDecember 31, 2010

    Kwa Mtoa maoni wa kwanza.KAMA VILE ILIVYOTOFAUTI YA MZUNGU ALIYESOMEA SWAHILI USA, NA YA MZAWA FULANI KARIAKOO,IGUNGA,TUKUYU AU MACHAME.

    Wazawa mara nyingi hawaongei lugha kisanifu, so ukijifunza kwao unarithi makosa yao, kwa upande mwingine shule haiwezi kukufunza sanaa ya lugha yoyote duniani.

    GO YOU TUBE,Jaribu kusikiliza jamie carragher, au mtu asilia toka liverpool kisha uchambue makosa. Mfano; ....this is me shoes, badala ya these are my shoes .

    ReplyDelete
  6. Any reason why Wabongo tunazimudu lugha nyingine zote ila Kingereza kinatupa taabu?

    ReplyDelete
  7. Babu Kaju miaka zaidi ya 20 hapa unyamwezini, bado anaongea english kama ndio kwanza anaingia. Kweli kazi ipo!
    For your info guys, don't get me wrong when i say that they're a lot of Tanzanians here in US, and in other english speaking countries who speak this language fluently.

    ReplyDelete
  8. Huyu jamaa Kajimulo ni mlala hoi ambaye kaangukia USA. Sasa anatumia muziki ili apate kula. Wenzetu wazungu huwa hawana cha kufanya basi hutafuta hobby ya kupotezea muda. Kuhusu kiingereza ni kuwa kuna viingereza vingi duniani na hapa kwao UK pia kuna vingi. Lakini kwa wasomi kipo kimoja tu chenye kukubalika cha kuandikia "thesis". Kuna sehemu chache ambazo UK na USA wanatofautiana kama vile spelling, pronounciation and past-participle. Sasa wabongo kwa sababu walimu wetu wabofu, nyumbani hatuzungumzi kiingereza na pia wepesi wa kutumia kiswahili kuweza kuwasiliana na kila kabila ndio tumeishia na kiingereza kibovu. Lakini msishituki maana wanageria wanaongea sana kiingereza lakini ukikichambua ni broken tupu.

    ReplyDelete
  9. Yale yale...watu washaanza kuchambua Kiingereza cha Nshomile wa watu, jamani lengo la lugha ni kuwasiliana...kama anaowasiliana nao wanamwelewa ni vyema. Masuala ya umilisi na utendi wa lugha si kila mtu anayaweza!! Tuchambue ubora wa kazi yake ni si usanifu wa lugha yake!

    ReplyDelete
  10. simple kajukulo acha kuimba ni aibu tubu!!

    ReplyDelete
  11. Wadau ngojeni na mie nichangie. Kajumulo mwacheni aimbe kwa sababu anapenda kuimba. Kwani Alivyokuwa anacheza mpira ni nyie mlimshauri afanye hivyo? Siyo lazima watu wapende wimbo wake lakini kuna watu wanaupenda hivyo mwacheni afurahie muziki wake. Kunawaimbaji wazuri lakini hata albamu moja hawajatoa kwa sababu ya kukatishwa tamaa na kusikiliza watu. Kwa kifupi ujasiri wa Kajumulo ni wa kuigwa kwa watu wote wapenda maendeleo na siyo tu kuponda, kuponda bila maendeleo. Aka!

    ReplyDelete
  12. Wadau acheni kumponda Kajumulo na kujifanya nyie ndio wajuaji wa lugha wakati wengine hata lugha yetu ya Kiswahili hamuijui kwa ufasaha mfano mdau wa Dec31 08:55:00 ameandika walimu wetu wabofu= wabovu na msishituki= msishituke na wadau wengine kujidai kuandika na kuchanga kiingereza na kiswahili kama nyie wajuzi wa lugha kwa nini msiandike lugha moja inayoeleweka?. nyie endeleeni kumponda wakati mwenzenu yake yanamuendea na anapata mkate wake wa kila siku.wabongo ndio maana hatuendelei kwa majungu sasa akijua hicho kiingereza au asipojua nyie wazee wa majungu itakusaidieni nini?
    mdau Paka la Jikoni.

    ReplyDelete
  13. nyie mnaoponda english yake, hebu muacheni, sio lugha yake kwa nini asichapie? hebu njooni msikilize wapolish wanavyoongea huku, au wahindi haswa wapakistani,me naishi na wapakistani hakuna maelewano kila siku. kukaa ulaya muda mrefu sio kujua lunga.

    ReplyDelete
  14. Ndugu zangu kazi yenu kuponda na kubeza, lakini nyie wote hakuna mtu aliyefanya kitu huyu jamaa anatafuta hela, na ndiyo maana hujasikia kajumulo kafungwa ulaya au usa, yeye ni kazi, kwanza jiulize ni $ ngapi analipa studio? na akitengeneza hii video ya malaria ikauzwa amazoni, itune, spotify ni shilingi ngapi atapata? Miaka iliyopita wakati tunaingia na trein kutoka Bukoba kuja Dar, tulivyokuwa tunafika Buguruni wazaramo wasema wALETE HAO WASHAMBA WA BARA, lakini miaka michake tukikaa tulirudi kwetu na maendeleo makubwa sana na tumewaacha hapo hapo mjini na wengine ndo nyie mnaandika pumba humu, nimegundua kitu kimoja kwamba watu wengi mnaochangia humu mnakuwa hamnakazi ya kufanya, hii blog siyo ya kukashifu wala matusi, kama huna la kuandika wacha na kaa kimya, ndugu zangu watanzania subiri vyandarua kupitia video hiyo hili ndo suala la msingi.
    Mdau uk

    ReplyDelete
  15. Wewe Anony wa Sat Jan 01, 03:04:00 AM
    usitudharau,na usidhani tunaoingia humu hatuna shughuli za kufanya.Hii blogu inatembelewa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa,mabalozi,maprofesa na watu wengi tu wenye hadhi zao.

    Unajitambulisha mdau uk,mbona hata mimi niko hapa Amsterdam ,Holland.Mimi huwa napenda kuchangia ukweli,Unataka tukitoa maoni basi tutoe CV zetu,kama mtu hajui ni kweli lazima tuseme ukweli maendeleo hayaji bila kusema ukweli.Wenzetu wazungu hawana haya ukikosea anakuambia straight na hii inawasaidia kuendelea hakuna kuficha kuficha

    Siku zote tambua kwamba mtu yeyote anapokukosoa basi usimfanye adui bali rafiki,anayekukosoa anakusaidia ili uende katika njia iliyonyooka.Tabia ya kukaa kimya na kutoelezana makosa ndiyo iliyoipelekea chi ya TZ kuwa maskini.Tuelezane ukweli ili tupate mafanikio.

    ReplyDelete
  16. Baba kanyaga twende...kilichobaki ni kugombea Ubunge Muleba South hapo 2015!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...