Mwenyekiti wa bodi ya Benki ya KCB Tanzania Dr.Edmund Mndolwa(kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Hai Dr.Norman Sigalla mfano wa hundi ya shilingi Milioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lyasikika ya wilayani humo. Wa pili toka kushoto ni Mkurugenzi wa masoko na uhusiano wa benki hiyo Christina Manyenye,Mkuu wa kitengo cha mikopo Ronald Kitti. Hafla hii ilifanyika katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Dares Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ankal hii ni changamoto kwa Benki zetu, Sina uhakika kama tuna tawi lolote la benki nje ya mipaka ya nchi yetu. Hongera sana KCB kwa kujali Elimu na Jamii kwa ujumla. CRDB na Benki zingine mko wapi msifungue matawi nje ya nchi jamani. Nchi hii miaka takribani 50 ya uhuru hatujawa na tawi la benki nje ya nchi????,,,,Aibu hii!!!!

    ReplyDelete
  2. Tatizo la Tanzania ni kujisahau sana, na kuwa nyuma kwa kila jambo nashangaa wenzetu wakenya,waganda ,wanaijeria wana matawi ya benki zao nje ya nchi zao,sisi ni uswahili mtupu,sijui ni kwa nini??Swala hili lipo hata katika kutangaza utalii !!Kenya inajulikana sana ki utalii kushinda Tanzania
    maana inajitangaza sana kiasi cha kwamba kitu kama mlima Kilimanjarao
    unaonekana ni wa Kenya !!!hadi baadhi ya watalii waje east africa
    ndipo wanashangaa kuona mlima huu upo Tanzania !!!Mimi kama mtanzania niishie nje ya nchi kwa siku nyingi nimeshuhudia mara kwa mara kuona Kenya iko juu kwa kutangaza utalii,na sasa hata mabenki yetu yajitahidi kufungua matawi nje ya nchi na siyo kujisahau na kubweteka tu.Watanzania inafaa tubadilike sana ili tujikomboe kifikra na kiuchumi pia.mtoa maoni.
    Washington Dc.Usa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...