Kuna mwamko mkubwa sana wa wananchi kutumia huduma mbalimbali za benki badala ya kuweka pesa mchagoni. raha ni pale inapokuja swala la kuchukua ngawira hasa kwa ATM. Foleni ni za kufa mtu na inatoa changamoto kwa mabenki sio tu kuongeza huduma hii bali pia kusambaza mashine hizo kwa wingi kila sehemu ili kupunguza ama kuondoa kabisa raha hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hizo ATM zisambazwe nchi nzima ndio zitakidhi mahitaji ya wateja.Bongo kweli tambarare....
    Mdau-KIWANJA!!!

    ReplyDelete
  2. Kitimtim kinakuja ukute kwenye foleni kama hiyo kuna walugaluaga wana tumia mda mreeefu kuchukua elfu 5 tu, yani mtadoda hapo weee, wakati atm zimewekwa kurahisisha mambo.

    ReplyDelete
  3. NI KWAMBA HIZO ATM NI CHACHE AMA WAUDUMU NI MWENGI. HATA INDIA KWENYE WATU WENGI SIJAWAHI ONE FOLENI KAMA HII . HAPO MJOMBA NDO UMEPANGA FOLENI KWA MA SAA THEN UNAKUTA ACCOUNT HAIJATENA DAH , NOMA

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  4. Idadi kubwa ya ATM pekee haitoshi kupunguza tatizo kwa ujumla.Nchi lazima ijaribu ku-adopt malipo kwa njia ya kadi.At least sehemu nyingi za biashara zikiwa zina-accept malipo kwa njia ya Debit cards basi watu hawatalazimika kubeba cash kila wakati ila kwa hali ya sasa ATM bado zitaendelea kuwa ni kimbilio maana bila cash mtu hawezi ku-survive!

    ReplyDelete
  5. Pamoja na kuongeza ATM kuna sual lingine inabidi mabenki yajitahidi.Mabenki yaanze kutumia teknolojia ya debit card katika ATM card ili wananchi waweze kununua bidhaa kupitia card badala ya cash.

    Kwa kuanzia tu baada ya kuanza kutumia teknolojia ya DEBIT card katika ATM Card mabenki yakutane na wafanyabiashara mbali mbali na KUWAELIMISHA waweze kuwa na mashine za kufanya malipo kwa kutumia debit card katika biashara zao.

    Hii haitowalazimu wananchi kutembea na pesa nyingi na wakati mwingine haitowalazimu wananchi kukaa foleni katika ATM machine kwa kuwa wataweza kutumia card zao katika manunuzi yao na vile vile Usalama wa fedha za wananchi utakuwa mkubwa.

    Namba kuwasilisha.

    Daniel
    The Netherlands

    ReplyDelete
  6. tatizo hii bank imepewa mzigo mkubwa na serikali mishahara ya waalimu,masoja basi kitimtimu.

    daa kwakweli bora rxim,baroda nk kuliko nmb

    ReplyDelete
  7. Tatizo Bank nyingi zimesambaza Machine za ATM ambazo ni mitumba, so far nyingi zimeshakufa. Zinazofanya kazi ni zile ambazo zipo kwenye bank branch. Mfano ATM machine nyingi za CRDB na NMB ambazo zipo mbali na Bank branch hasa Dar hazifanyi kazi.Ukikuta moja inayofanya kazi foleni ndio kama izo.

    ReplyDelete
  8. Haya mabenki hayana mshindani (competitor). Serikali pamoja na vyama vya ushirika (credit unions)vianzishe benki zao ili kuyapa haya mabenki yaliyopo ushindani na matokeo utayaona. Na kuhusu swali la kutumia debit cards, kwanza hakuna umeme, pili biashara nyingi hazijafika huko.

    ReplyDelete
  9. WATU WANAZUNGUMZIE ZIWEKWE KILA MAHALI. MBONA HAMZUNGUMZI SECURITY AU HIZO ZITAJILINDA KIVYAKE.

    HAKUNA USALAMA. NA MAMBO HAYA YANAENDANA NA MAZINGIRA SIO KILA SEHEMU KUWE NA ATM.

    ikiwa kama uingereza au part ya EU wanapigizwa iwe tz

    ReplyDelete
  10. Kulipa kwa kadi ni vizuri lakini UK kuna maduka wanakukata pesa kwa kutumia huduma hiyo, na pia wengine utumie si chini ya pound 10. Sasa kama mbongo ukikatwa paundi moja ni 2500 hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...