Fuvu la kichwa la marehemu Martine Kiyeyeu mkazi wa kijiji cha Mlolo kata ya Mseke wilaya ya Iringa vijijini likitolewa kaburini
Mabaki ya mwili wa Kiyeyeu yakiwekwa katika jeneza tayari kwa kwenda kuzikwa upya baada ya eneo la awali kuchimbwa kaburi lake ili kupisha upanuzi wa barabara kuu ya Iringa -Mbeya
Jumla ya makaburi nane ndio ambayo yameondolewa katika eneo hilo na hakuna tukio lolote la ajabu lililopata kujitokeza pamoja na kuwepo kwa maneno mengi toka eneo hilo. Picha na mdau Francis Godwin.

Ankal alitembelea eneo hili mwezi wa Septemba,
kabla ya makaburi kuhamishwa.
BOFYA HAPA




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mizimu ya Chifu Kiyeyeu imeamua kula kobis!!!

    ReplyDelete
  2. watanzania kweli ni majabari wa aina yake, wanafukua makaburi kwa kuvaa gloves tu! hakuna kujifunika pua kupunguza harufu na kujilinda ma madhara yeyote yasiyotegemewa ambayo huenda maiti imesababisha, halafu i bet watu wameondoka hapo direct wamekwenda kupiga sembe bila wasi wasi wowote!

    ReplyDelete
  3. Ankal, asante sana kwa kutuletea tena hii habari. Ama kwa hakika utata ulio kuwepo juu ya mazingaombwe hayo umetoweka. Mie pia nilikuwa njia panda kwani nilikuwa sijui ukweli ni upi.
    Kuwezekana kuhamishwa kwa makaburi hayo inaonekana kweli ulikuwa ni uongo tupu. Na kama baadhhi ya wadau walivo comment sababu kuu ni ulipaji wa fidia na si vinginevyo. Hakuna cha mizimu imeamua kula kobisi au la nguvu zime expire wadau watuambie hayo makaburi yameishi hapo kwa miaka mingapi?
    Napenda kuwakilisha.

    ReplyDelete
  4. suali tu, je hakuwezekana kuwekwa tent sehemu hiyo ya ufukuzi kama stara ya marehemu na pia kupunguza maumivu ya ndugu wa marehemu kumuona ndugu yao katika hali kama hiyo! ni nani atakaependa kuona maiti ya jamaa yake ikiwa katika hali kama hiyo tena isitoshwe ipigwe picha na kuwekwa mtandaoni? Uungwana ni vitendo sio maneno watanzania wenzangu!

    Michuzi usiniweke kikapuni!!! Hii inauma mno!!!

    ReplyDelete
  5. Next time ankal kwa manufaa na privacy ya wana familia inabidi usiweke jina la marehemu kwani itaweza ibua simanzi na msiba upya!
    Ni maoni tu.

    ReplyDelete
  6. Abiola Jr. New Albany OhioDecember 31, 2010

    Ni mapema mno kusema kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa sasa, tusubiri angalau wikik mbili tatu hivi huku tukifuatilia kwa karibu afya na maisha ya walioshiriki kuhamisha makaburi hayo na hata hawa wanaoshiriki kutoatoa habari zinazomhusu KIYEYEU.

    ReplyDelete
  7. Bora wamehamisha hayo makaburi kiungwana. Tabora nilishuhudia makaburi yakifukuliwa na mifupa kutupa ovyo kando kando ya barabara ili watu wajenge majumba! Ila na mimi nina wasiwasi pia, mbona hao waliofukua hawakuvaa masks? Mmewahi kusikia Curse of King Tut?

    ReplyDelete
  8. Ankala Nakupa five kwa kutupa news motomoto. Lakini leo umetufungia mwaka kwa style ya kipekee. Hata kama marehemu alikufa miaka 40-50 iliyopita.Mabaki yake bado yanastaili heshima.Sidhani kama ni busara kuyatundika hadharani kana kwamba yameokotwa mtaani.

    ReplyDelete
  9. Watanzania tunalilia katiba lakini kuna mambo mengi yanahitaji kuwepo, katika hili naona Tanroad hawana mtu wa Health and Safety na Risk Management kama hawa wangekuwepo husingekuta haya, watu kufukua maiti bila kuwa wataalamu na kazi hiyo na bila kupewa mafunzo maalum, hii yote ni njaa inayosababishwa na shule ya darasa la saba hizi ndizo kazi zao kwani hawana kazi nyingine za kufanya, ndiyo maana tunataka mfumo wa elimu ubadirike.
    Mdau uk

    ReplyDelete
  10. watu wanaoishi ughaibuni bwana...utawajua tuu. Mara oooh health and safety..., tent..., mask...., forensic expert...;

    huku bongo hakuna mambo hayo, tuna mambo muhimu zaidi ya kufanya kabla hatujaanza kufikiria mambo haya.

    ReplyDelete
  11. Jamani kumbe yale tuliyokuwa tunaelezwa ohh watu wamejaribu kuhamisha kaburi lakini wameshindwa ilkuwa stori za vijiweni tuu. Naomba serikali iwachukulie hatua kali hao makandarasi waliotumwa kufanya hiyo kazi miaka ya nyuma na kuleta stori za vijiweni badala ya kufanya kazi. Umeme umepitishwa kwingine kiholela kwa sababu mkandarasi alitunga tuu story ohh umeme umeshindwa kupita juu ya kaburi...jamni hizi stori zetu tutaacha lini? Hadi kwenye mambo ya maendeleo tunaleta mchezo. Hii bara bara ingeshakuwa imepanuliwa tokea 1989.Sababu za story za vijiweni tumengojea miaka 21 kufanya kazi hii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...