JK na mwenyeji wake Rais Hosni Mubarak wa Misri katika ikulu ya Cairo wakati nyimbo za mataifa hayo mawili zikipigwa kwa heshima ya marais hao wakati Rais Kikwete aliposimama kwa muda nchini misri akiwa njiani kuelekea jijini Brussels Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa maendeleo ya kiuchumi
JK akikagua gwaride la heshima liliandaliwa na vikosi vya ulinzi vya Misri wakati Rais Kikwete aliposimama kwa muda jijini Cairo na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Hosni Mubarak akiwa njiani kuelekea Brussels Ubelgiji kuhudhuria mkutnao wa Maendeleo ya Uchumi
JK akizungumza na mwenyeji wake Rais Hosni Mubarak wa Misri ikulu ya jijini Cairo, wakati Rais Kikwete aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea mjini Brussels Ubelgiji kuhudhuria mkutano wa maendeleo ya Uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Staff Sajenti NzabomanaDecember 06, 2010

    Nimevutiwa sana na hilo jeshi la Misri. Askari wote wanaonekana kuwa ni wakakamavu. Urefu sana. Vitambi hakuna, yaani hadi raha.
    Ziko wapi zile enzi za Tanganyika ambapo kuingia jeshi ilikuwa mpaka uwe mrefu wa kutosha na ukakamavu wa ziada. Siku hizi jeshini hata ukiwa na futi 4 twende tuu. Jeshi limepungua ladha yake kwa kweli.

    ReplyDelete
  2. Du, mdau wa kwanza una macho, ni kweli majamaa wameenda hewani wamenyooka, tamu zaidi ni mahandsome kweli, wana mvutoo!!

    ReplyDelete
  3. safi sana jk umetua misri kunywa chai then uingie ubelgiji ukafanye mambo.

    ReplyDelete
  4. Suala nyeti linaloifanya Misri angalau kutusikiliza sisi wabantu ni maji ya ziwa victoria kama mojawapo ya vyanzo vya Nile, tishio la East Africa kuvunja mkataba wa maji na kujibiwa na tishio la kijeshi kwa nchi yeyote itakayodhubutu ni suala nyeti kweli. JK kuwa ng'ang'ari na sulala hilo. Waache vigeugeu kama Museveni kusita kutia saini. AlexBura

    ReplyDelete
  5. Mdau e Mon Dec 06, 02:14:00 PM umesema kweli kabisa Haya jamaa wana nyodo kichizi nilishawahi kutana na mmoja wao Japani yeye salaam zake kwa kila mtu zilikuwa " I have never been to Africa" Wanadharau hakuna. Wanaita kila mtu mweusi ZANZIBARYA nasikia siyo neno zuri. Sasa kuhu maji hakuna kulala, Kama alivyosema Idd Amin kuweka meter pale owen falls nao walipe.

    HIvi kama mwingereza angesema Mafuta 90% ya Africa hawa wangekubali hata kidogo waache hizo

    ReplyDelete
  6. Kweni lake victoria maji kiasi gani kina enda misri? Asilimia 90 ya Nile inatoka Ethiopia na asilimia 5 Uganda. Victoria ni asilimia 3 pekeyake. wabongo kwa kulalamika....maju nyingi bado mnakufa na kiu alafu mnalalamikia river Nile kama vile kiasi kikubwa kina toka kwenu. Waethiopia wata semaje

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...