Home
Unlabelled
Prof. Ndullu presents new Tanzanian bank notes to President Kikwete
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
naomba wadau mnieleweshe maana ya kutoa noti mpya mbona nikiangalia nchi za wenzetu fedha zao hazi chapishwi mara kwa mara faida gani tunaipata kubadilisha fedha na hasara gani tunapata,kama zipo hasara kwanini hawazifikirii au nikila rais anakuja na matoleo yake?
ReplyDeletetueleimishwe juu ya hizo security features au ni siri kwa general public??
ReplyDeletehii itasaidia sana kudhibiti note fakes kuingia kwa kasi nchini. na mara nyingi mahajangili hutumia lop hole mwanzoni kabisa ya matumizi ya pesa. serekali inajukumu ya kutoa elimu kupitia vyombo vya habari
Yaani bongo hatuwezi kujakuendelea.. yaanini juzi tu gavana ameelezea sababu za kuwa na noti mpya leo hii mdau wa kwanza kasha sahau... duh kazi kweli.
ReplyDeleteHivi si kule kwenye forum ya wasema hovyohovyo wamesema Dr. JK yuko NY? Sijui ni wivu au ni roho mbaya tu waliyonanyo.
ReplyDeleteHasara ni the value of money ina decrease. Faida sijui kwa kweli....Dola ni ileile toka elfu lela ulela...siye kila siku zabadilika na nadhari cost ya kutengeneza noti ya shilling moja ni kubwa kuliko hiyo shilling moja yenyewe....
ReplyDeleteUlieomba kuelimishwa nakumbuka juzi kwenye saa moja jioni kuna station moja ya TV walikuwa na kipindi kirefu tu wakielezea hizo security features mpaka ukiweka kwenye mwanga maalum inakuwa na rangi gani mambo mengi tu walieleza. Sema ndio hivyo inaweza kuwa bahati mbaya pale wanapoonyesha au kuelezea kwenye redio mtu unakuwa hujui kama kutakuwa na kipindi kama hicho.
ReplyDeleteDr Mkulo????
ReplyDeletekuna watu wengine hata kufikiria kunawashinda mtu ameomba aelimishwe juu ya faida na hasara ya kuchapisha noti mpya kila mara,kama unajua kwanini humwambii..eti juzi juzi gavana kasema wewe unafikiri kila mtu ana time na michuzi au blog nyingine kila mara?mjinga mwingine anadai walitoa kwenye tv hahahahah hivi mnajua wote wanaishi bongo na kuangalia hizo tv zenu eeeh!!!!kabla hujaandika jaribu kufikiria kwanza na wewe uliyeuliza swali je umeshajaribu kupekenyea kwenye internet na vyanzo vingine vya habari ili ujue faida na hasara ya kuchapisha noti kila kukicha? haaaaaa,watanzania ni wajinga kweli na mtaendelea kufanywa wajinga mpaka mfe shenzi zenu!!!
ReplyDeleteSerikali iko bz kufyatua noti mpya wakati wananchi wateseka kwa kukosa umeme...Duh Mungu ibariki Tanzania..
ReplyDeleteJamni ninyi mko mbali sana, hivi hamjui nini madhumuni ya kuchapisha pesa mpya kila mara.Sasa nawapa somo:
ReplyDeletePesa mpya zikichapishwa huwa ni siri hatuambiwi ni kiasi gani cha pesa nchi yetu imechapisha huwa inabaki siri kati ya serikali(siri kali) na kampuni ya utengenezaji hayo mapesa.Sasa kama hatujui na hata tukiambiwa hatuna uwezo wa kujua ni kweli hicho kiasi kilichotengenezwa ni cha kweli,kwa maana hiyo uchapishaji wa pesa mpya ni utajiri kwa baadhi ya watu, na ndiyo maana wanakuwa wakali sana wakisikia kuna pesa "bandia" mitaani.kwa nini ziitwe bandia na za kwao walizotengeneza ziwe ndiyo halali tu? Hivi ni mara ngapi tumeshabadili hizo pesa? hatuoni hata aibu jamani? Tujifunzeni kutokana na makosa.mimi nasubiri tu kusikia hiyo tenda iliendaje na akina nani wameshakula cha juu..
mimi nataka niambiwe idadi ya fedha mpya iliyotengenezwa,nina maana ni matrilioni mangapi? na wenyewe wamekula ngapi?
ReplyDeleteMbona idadi hatuambiwi eeeee!!!!!!
Shem Michuzi
ReplyDeletenaomba nifikishie barua hii kwa mheshimiwa Rais Kikwete.
Ndugu Rais
kwanza nataka kukupa hongera kwa kuchaguliwa tena na pia hongera kwa mafanikio na kazi kubwa unayofanya.
mimi sioni umuhimu wa kuchapisha noti mpya wakati kuna vitu kibao utawala wako unatakiwa kufanya. mimi naitwa Rukia Malipula ni mkazi wa Marekani kwa muda mrefu lakini nina mpango wa kurudi nyumbani hivi karibuni.Kwa hiyo nimeaanza kufanya investments fulani, kitu kinachonisikitisha ni kwamba wafanyakazi hawana mafunzo ya customer service.ukienda ofisi nyingi za serikali ni wajeuri sana.
imenichukua kama miezi minne kuandikisha kampuni wakati huku Marekani kuandikisha kampuni inachukua dakika tano.
swala lingine linalosikitisha ni hizo kodi zenu ambazo saa nyingine zinatisha kwa mfano wiki hii nimepeleka mzigo wa vifuniko kwa ajili ya chupa za kuwekea sabuni custom duty wamenichaji shilingi laki moja na thelathini na saba,vifuniko viko 1800 kama sample bei yake ni kama dola 20, kwa hiyo nimechajiwa custom duty zaidi ya asilimia hamsini, ukumbuke hivi vizibo ni mali ghafi.Je tutafika ?
mzigo imebidi tuuache posta manake it doesnot make no sense.Halafu muhudumu anajibu kwa hasira nyie si mnaenda kufanya biashara itabidi mlipe. Tatizo si kulipa inabidi serikali yako ianze kusupport viwanda vipya na vidogo ili vitoe ajira na pia watanzania tuweze kununua bidhaa bei ya chini.Marekani inasupport sana biashara ndogo na kodi zinazoeleweka, kwa nini tusifuate mfano wa wenzetu walioendelea ? swala lingine tunaomba barabara za jijini Dar ulitilie mkazo, foleni sio ya kawaida nilisikiliza hotuba yako ya kufunga bunge mwezi wa kumi, nilikuwa Dar,ilikuwa nzuri tafadhali timiza ahadi zako. kuhusu hizo kodi kwa nini zisikusanywe na wilaya kwa ajili ya wilaya, na wilaya zipileke fungu lao serikali kuu? kama wanafanya wenzetu, huoni kwamba itakuwa rahisi kuzikusanya na kuzitumia wilayani humo humo kuliko kusubiri peasa kutoka serikali kuu, la mwisho ni swala la maji,kule kwetu Tabata maji yanatoka mara moja kwa wiki, hivi ni haki pamoja na wachina kuchukua mabilioni ya pesa kufunga mabomba yasiyotoa maji, aliowaambia tabata tulikuwa hatuna mabomba ni nani?
Ndugu Rais tafadhali usisahahu wannachi waliokuweka madarani.
Rukia Malipula
Hivi kwa nini kuchapishwe noti za design mpya kila siku kwa nini tusiwe na standard moja ya pesa hii sheria ya kuwa BOT kila baada miaka 5-7 wanaweza kubadilishwa inatumika vibaya.UK,USA nk noti zao miaka nenda miaka rudi iko vile vile .
ReplyDeleteJengine sikuona twiga kuweka mara hii ambaye ndio national animal, TZ ni nchi pekee inamtumia twiga na ni mnyama mzuri kwa kivutio na fahari ya nchi. Tusisahau tunapoteka kufika tunapokwenda
Wadau hapo juu jaribu kujielimisha kabla ujauliza swali. Nchi zote zinachapisha pesa. Nchi kama marekani inachapisha pesa (paper dollar)kila miaka fulani kulingana na jinsi inavyochakaa. Pia paper money inaweza kuchapishwa kwa sababu ya kuongeza usalama. paper dollar in circulation ni $800 billion. Marekani inataka kuchapisha zaidi ya $600 billion juu ya za sasa ambayo itasababisha kushuka kwa thamani. Paper dollar zinatengenezwa Fort Worth, Texas.
ReplyDeleteNchi ya dunia ya tatu kama Tanzania mara nyingi zinachapisha pesa kwa sababu zilizoelzwa hapo juu au baada ya uchaguzi na kusababish kushuka kwa thamani.
Anony Fri Dec 24, 04:32:00 PM naona kimekuuma sana. Kama uko nje ya nje na hujui faida na hasara za kuchapisha noti nafuu tu urudi bongo. Nchi yetu haiwezi kuendelea kama tutaendekeza huu ujinga kila siku tunaongelea mambo yale yale ambayo hayana mbele wala nyuma. Kama huna time na blog au vyombo vya habari vya bongo nyamaza tu. maelezo ya gavana yalitolewa kwenye kila chombo cha habari cha bongo hata kule kwenye forum ya wasema hovyohovyo waliongelea sana na limtu linakuja kuuliza swali lile lile.
ReplyDeleteNa nyie mnaosema eti Marekani hawabadilishi hela zao akili zenu hazina akili kaka michuzi tubandikie hii link http://www.newmoney.gov/currency/history.htm
hapa USA wamechapisha not za dola mia kunatatizo la langi kwenye hizo noti mpya kwaiyo nilizuiwa kutoka sasa kasheshe ni kua noti zilikua ni dola billioni kuzitengeneza kulicost zaidi ya billion 10 kwaiyo kutengeneza pesa kunacost mala 10 ya kiwango cha pesa unazo tengeneza
ReplyDeletesina muda wakuangalia tv kujua hizo security features.si unajua tanesco hawajatuanganishia umeme huu ni mwezi wa nne na mimi nimewambia sitoi rushwa. sasa ndugu yangu utanilauumu kwakutokuwa na tv.pili na imani kubwa kuna ufisadi unapita kila kukitolewa note mpya.unajuwa hawa viongozi wanadhani watu wajinga lakini iko siku watatuharibia amani.
ReplyDelete