Na Catherine Sungura,MOSHI

Baraza la madaktari nchini,limetakiwa kuhakikisha wananchi wanahudumiwa na wanataaluma kwa kuzingatia ubora na usalama,kwakuwa mgonjwa ndio kitovu cha kazi ya taaluma ya udaktari.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa afya na ustawi wa jamii Dkt. Hadji Mpinda alipokuwa akizindua baraza jipya la madaktari Tanganyika nchini.

Dkt. Mponda alisema wajibu wa wanataaluma wa udaktari ni kuweka wazi haki na usalama wa mgonjwa ili kuondoa malalamiko ambayo yanaongezeka siku hadi siku.”ni imani yangu kwamba baraza jipya litasimama imara na kuhakikisha mahusiano ya mgonjwa na daktari yanakuwa ya kuaminiana na litakuwa jambo la kusononesha ikiwa jamii itashindwa kuwaamini wanataaluma wa udaktari.

Aidha aliwataka wanataaluma kuwa makini na kutekeleza majukumu yake kwa uaminifu wa juu na kuheshimika na mteja”hayo yanawezekana kwa daktari kuwa mkweli ,kuheshimu taarifa za siri zinazomhusu mgonjwa ambazo amezifahamu kwa mujibu wa mahusiano ya kuaminiwa baina yake na mgonjwa huyo atakuwa mwaminifu na mwajibikaji”alisisitiza.

Hatahivyo waziri alilitaka baraza hilo kuhakikisha wanataaluma wanapitia katika vyuo vinavyotambulika na wanapata elimu sahihi itakayomwezesha kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyokubalika,hivyo kushirikiana na mamlaka nyingine za taaluma kutengeneza miongozo ya vigezo vya aina ya elimu inayotakiwa, utaratibu wa kuipata itakayojumisha miundombinu ya chuo husika inayokidhi sifa zinazokubalika kutoa elimu na ngazi hiyo.

Kwa upande wa kada ya matabibu ambao wengi wao wanatoa huduma za tiba vijijini,lakini hawajawekewa mfumo wa kusajiliwa na baraza hilo,Dkt. Mponda alilitaka baraza liweke utaratibu wa kuwatambua kisheria ili waweze kuongozwa na kusimamiwa na baraza hilo kwani matabibu ndio kada muhimu katika mpango wa afya ya msingi vijijini(MMAM) na wanapaswa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma.

Baraza hilo jipya litakalodumu kwa mika mitatu linaongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mganga mkuu wa Serikari Dkt.Deo Mtasiwa,wajumbe wengine ni Profesa David Ngasapa, Dkt. Gabriel Upunda, Dkt. Ramaiya Kaushik, wengine ni Dkt. Rosemary Kigadye, Profesa Phillip Hiza na Kasmir Kyuki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. "waweze kuongozwa na kusimamiwa na baraza hilo kwani matabibu ndio kada muhimu katika mpango wa afya ya msingi vijijini(MMAM) na wanapaswa kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma." HILI NALIUNGA MKONO SANA ESPECIALLY NINAPOSIKIA WAZEE WANGU KULE MWANGA KILA MARA WANAVYOLALAMIKA JUU YA MATABIBU KUSHINDWA KUWAHUDUMIA IPASAVYO; NADHANI WENGI WANASAHAU KUWA WANAPOHUDUMIA WAZEE INATAKIWA UNYENYEKEVU NA MUDA ZAIDI WA KUMUELEWESHA MZEE JUU YA DAWA UNAZOMPA NA/AU TATIZO ALILO NALO. KUONYESHA DHARAU NA ROHO MBAYA WAKATI WA TIBA NI KUTOKUJUA WAJIBU WAKO KAMA TABIBU!

    ReplyDelete
  2. Sasa nafikiri inabidi kufuatilia nini haswa sababu za hao watu kulalamika kuwa huduma ni mbaya na kama ni kweli matabibu wanakuwa na dharau pia roho mbaya basi tuangalie kwa kina nini kinasababisha hii tatizo kwani kulalalamika tu siku zote hakusaidii kitu....
    Maana kwa tz hakuna ofisi ya umma yenye huduma nzuri kote ni kero tu labda mdau unambie huduma gani za umma zinapatikana bila kero kama hizo ulizoainisha juu hili ni janga la kitaifa.....katika srkta zote..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...