Miili ya vichanga 10 vilivyokutwa vimetupwa katika jalala kwenye nyumba moja iliyo jirani na makaburi ya Mwananyamala, na wanawake watatu wako mikononi mwa polisi kusaidia uchunguzi wa tukio hili la aina yake ambalo Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Afande Charles Kenyela amethibitisha.

Pia Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Jordan Rugimbana naye amethibitisha tukio hilo na kuahidi kulitolea ufafanuzi ofisini kwake kesho saa sita kamili mchana. Pichani juu ni sehemu ya miili ya vichanga hao ambayo haikuweza kuoneshwa yote kwa sababu za kimaadili


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Na hamu ya kukoment lakini sina cha kukoment kwa mshangao! nimeshtuka

    ReplyDelete
  2. Itabidi tufafanue upya 'AMANI' na 'UPENDO' tuliyonayo WaTanzania ni ipi. Maana hii imekaa 'kishirikina'
    Kuna video kule MichuziJr kuna mchizi anasimulia.. tembelea..

    ReplyDelete
  3. nimeumwa na tumbo la uzazi kwa hili jambo. eeh Mungu, ni nini hiki jamani binadamu wako wanafanya??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...