ANKAL NAOMBA KUWASILISHA KERO YANGU KUHUSU USAFI WA JIJI LA ARUSHA, JIJI HILI HUITWA GENEVA OF AFRICA LAKINI KIUKWELI HALI YAKE YA USAFI HAIRIDHISHI HATA KIDOGO SIJUI WAHUSIKA WANACHUKUA HATUA GANI KUONDOA HALI HII.
UKIPITA MITAA YA KATIKATI KAMA VILE ENEO LA OFISI YA CCM MKOA, KUZUNGUKA AMRI ABEID STADIUM NA SEHEMU NYINGINE MITARO IMEJAA UCHAFU MAKOPO YA MAJI NA MIFUKO YA PLASTIC IMEZAGAA, MAJANI NA TAKA ZA MAHINDI YA KUCHOMA USISEME KWAKWELI TUNATIA AIBU, NAOMBA VIONGOZI WA JIJI HILI WACHUKUE HATUA ZIFUATAZO.
1. WAAJILI WAFANYA USAFI WA KUTOSHA KUSAFISHA ENEO LOTE LA JIJI KWANI WALIOPO HAWATOSHELEZI
2. WAENDE MANISPAA YA MOSHI WAKAJIFUNZE JINSI WENZAO WANAVYOMUDU KUWEKA MJI WA MOSHI SAFI
3. WAACHANE SASA NA MAMBO YA SIASA NA KUSHUGHULIKIA KERO ZA JIJI IKIWEPO HII YA UCHAFU ULIOKITHIRI
4. WAPITISHE MATANGAZO YA KUBANDIKA NA KUTANGAZA KWA MAGARI KUWAHAMASISHA WANAARUSHA WOTE KUWA NA TABIA YA USAFI KWA KUTO TUPA TAKA OVYO MITAANI
WENGINE WENYE MAONI YA KUBORESHA MJI HUU WAYATOE TAFADHALI KWANI TUNATIA AIBU HATA UKIKARIBIA LANGO LA AICC UPANDE WA MAUNT MERU HOSP NYASI HADI BARABARANI NI AIBU KWA WAGENI WETU.
NAOMBA KUWASILISHA HOJA HII NA KAMA UNAWEZA KUIFIKISHA KWA MKURUGENZI WA JIJI NITASHUKURU.
MDAU FRANK
ARUSHA

Naungana na mdau Frank wa Arusha, kushinikiza manispaa na watendaji wake kuangalia suala hili la uchafu uliokithiri Arusha kwa umakini,mfano kuhusu Moshi ni hali halisi ambayo inaweza kuigwa kwa manispaa nyingine yeyote.Manispaa kupitia kwa mgambo na wafanyakazi wengine huwa inapita mara kwa mara kukusanya bidhaa za machinga na wamama wa sokoni ambao wako katika harakati za kujitafutia riziki, je kwanini kusijengwe soko jingine kubwa kuweza kuwahifadhi wajasiriamali hao?
ReplyDeleteMgambo hao kwa nini wasitumike kukamata watu wanaotupa taka ovyo ikiwemo chupa za maji toka kwenye magari?kwa nini tunang'ang'ania vitu vingine kama wrong parking?
Arusha ni mji unaoendeshwa kibabe sana, Manispaa is still asleep.
Ukiingia soko la Arusha upande wanaouza matunda na kuku utatamani urudi tu maana hutakuwa na uhakika ukitoka ndani ya soko sio unapeleka mazalia ya wadudu nyumbani. Wake up manispaa....
Nina mengi sana ya kuongea kuhusu Ausha lakini waangalie kwa hili ambalo mkoa uliopo dakika 45 toka hapa wamefanya mengi na ni mfano wa kuigwa kwa mji msafi.
Ningekuwa namshauri raisi, mkurugenzi wa mji wa moshi aje arusha wakati wa arusha anastaafiswa kwa manufaa ya umaa, mbaya nini kwani?
asante.
Mdau mkereketwa wa Uchafu A-TOWN.
kweli hata mimi naungana na frank sijui wahusika wako wapi mpaka jiji la arusha linakuwa chafu kiasi hichi mgambo wako tu kwakushughulika na watu wanao tafuta riziki zao inatia aibu sana watalii wanakuja kutembelea arusha wanashangazwa sana uchafu uliokidhiri niaibu sana wahusika wamekaa kimya wanakula mishahara ya bure tu. inaudhi asna wangeanzisha dizaini ya mtu akitupa taka atozwe faini na atakaye mkamata mtu akitupa taka awapeleke kwa wahusika na huyo aliye mpeleka anapewa silimia flani nafikiri hiyo itasaidia mji wa .Arusha unakuwa ni aibu uchafu kukidhiri pls wahusika amkeni asas acheni kulala nafikiri mnaelewa wajibu weni sio msubiri mpaka kipindupindu kimalize watu
ReplyDeleteTukiongea hapa inaweza kuonekana tunaleta siasa, lakini ukweli ni ukweli. Hawapo watu wenye dhati kuwatumikia wanaArusha. Ni siasa zaidi kuliko kazi yenyewe. Inahitaji commitment. Watu hao hawapo. Kwa Moshi wanawajibika. iko mifano mengi
ReplyDelete