SHARIFFA ABDARAHMAN ABDALLAH (MAMA KIMARIO)

Leo ni mwaka mmoja tangu ulipotutoka tarehe 21/01/2010
saa moja na nusu asubuhi pale Mwaisela, Muhimbili Hospital tukiwa tunakuangalia na kukosa la kufanya zaidi ya kumuachia Mwenyezi Mungu afanye analotaka kwa kiumbe wake kwa kuwa ndio alitulea na kaamua kukuchukua.


Sisi watoto wako Fatuma, Neema, Kashenge, Abdulrahman na Mfaume, wajukuu zako Cossy, Nurdin na Nyota (Star) bila kusahau Familia ya Maj General M. Kimario (Rtd) umetuachia ukiwa kwa mapenzi, upendo na mwongozo wako kwetu.

Tutakukumbuka daima katika maisha yetu ukizingatia kupata mbadala wa wewe (mama) ni kitu kisichowezekana, hatuchoki kukuombea kila siku kwenye sala zetu, tunamuomba mwenyezi mungu aiweke roho yako peponi.

"INNA LILLAHI WAINA ILLAIHI RAJIUUN"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nawapa pole Mzee Kimario na watoto wako wote. Mola aiweke roho ya dada yetu peponi. Amin.

    ReplyDelete
  2. REST IN PEACE AUNT SHARIFFA.AMEN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...