Askofu wa KKKT kanda ya Kaskazini kati Thomasi Laizer wakibadilishana mawazo na Katibu Mkuu CHADEMA katika uwanja wa NMC kwa ajili ya kuaga miili ya wananchi waliouwawa katika vurugu la kisiasa jijini Arusha wiki iliyopita
Home
Unlabelled
Mazishi ya waliokufa katika vurugu za kisiasa arusha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hii kitu mimi inaniuma sana na inakera. Kulikuwa hakuna sababu ya kuzuia maandamano ya amani kama yale. Polisi wangesubiri kwanza hadi mwisho wa mkutano waone kama wafuasi wa CHADEMA wangeleta vurugu. Sisi wengine hata kadi za vyama hatuna lakini inakera kuona watanzania wenzetu wakiondolewa maisha yao hivi hivi tu ,fikiria juu ya wake zao na watoto wao. Jamani Polisi jifunze kufanya kazi zenu kitaaluma, hizo hisia zenu za KINTELIJISIA na kuanza kufyatua risasi za moto zinalifikisha Taifa letu pabaya.
ReplyDeleteMbona hakuna fujo zozote zilizotokea? Wananchi wasio na hatia wameuwa bure. Mungu awalazie mahala pema peponi.
ReplyDeleteWadau Serikali haikuona umuhimu wowote ule wa kutuma wawakilishi?
ReplyDeleteSerikali inabidi ijifunze kwa hilo lililotokea
ReplyDeleteInasikitisha kuona wanasiasa wanachochea fujo kwa kuwashawishi wananchi waandamane kwa maslahi yao binasfi...
ReplyDeleteyote haya ni kwa ajili ya uchu wa madaraka...kugharamia mazishi si kitu swali linakuja Je mtaweza kuzihudumia familia za hawa watu walioathirika! Kila mtu anajaribu kukwepa kulaumiwa..
Dola hata siku moja haitafutwi kwa kumwaga damu za watu wasio na hatia...kama bado hawajaridhika na matokeo ya uchanguzi kwa nini wasijipange uchanguzi ujao? maandamano na ghasia havitaweza kuwasaidia kwa maana kama sheria ikifuatwa hakunu atakayewatetea.
Inauma sana...hivi kweli huyu Mbowe na mwenzie Silaha wanajiona ndo manabihi na wenye uchungu na hii nchi peke yao...mbona historia zao wote hazinifanyi nishawishike na dhamira yao ya kweli...bado nawaona kama ni wanafiki tu ambao hawajui walitendalo..damu za watu hawa zitawatafuna mpaka waendapo kaburini.
Time will Tell.
Mitoso.
Poleni sana wafiwa. Hii hali hatujazoea. Pia tuwe tunatii matakwa au matangazo ya wenye dola ili kudumisha amani
ReplyDeleteHili Jeshi letu ni lakulinda raia au kuua raia? nadhani hapo kuna ukinzani wa maamuzi na hili swala tunataka liundiwe tume na watu wawajibishwe. Nasikitika kwanini hawa viongozi wa juu wa jeshi la polisi hawajajiuzulu. Ukombozi wa Mtanzania sasa hvi hauji bila incha ya upanga, lazima tudai haki kwa hali yeyote ile. Watanzania tumechoka na mambo yanayofanywa na hii Serikali ya CCM. Kila kukicha vi vituko. Iko siku yatatokea mambo mabaya, badilikeni tuijenge nchi yetu. Acheni ubinafsi na ulafi nyie viongozi wa CCM.
ReplyDeleteHuyo anayejiita Mitoso hapo juu naona hana kabisa hoja. Waliokuwa wanaandamana walikuwa wanadai haki yao waliyonyang'anywa na wala sio madaraka.. Halafu unazungumza kama kwamba walioandamana ndio walioua... shame on you!
ReplyDeletePole kwa wafiwa, inasikitisha sana kuona anaeandaa vurugu hakujeruhiwa,hii risasi ingempata mchochezi mkuu ambae ni Slaa anaetafuta umaarufu kwa kuwatoa kafara vijana wa watu. Damu zao zitamhukumu!
ReplyDeleteWewe Mitoso, hapo hakuna cha uchu wa madaraka. Yalikuwa ni maandamano ya amani lakini kiburi cha jeshi la polisi ndiyo iliyosabisha yote haya. Na serikali kupitia kwa waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje imekiri jambo hili kuwa ni kosa la polisi. Sasa sijui wewe ndugu yangu unaishi katika dunia gani kusema ni uchu wa madaraka. Mgomo wowote ambao ni wa amani ni haki ya msingi kikatiba kwa raia yeyote wa Tanzania bila kujali itikatidi za kisiasa, kidini, kikabila nk.
ReplyDelete... NA "MHESHIMIWA" RAIS WA JAMUHURI ANASEMAJE KWA HAYA YALIYOTOKEA?! AU MIMI NIMEPITWA NA SPEECH YAKE?
ReplyDeleteHaya mazishi Chadema wanayatumia kwa ajili ya faida ya kisiasa na hii inatia kinyaa. Yote hii ni kwa ajili ya kupata picha na kuonyesha ulimwengu kwamba wanatetea wanyonge. Hata mtoto mdogo anaweza kuona hii ni PR stunt ambayo inapunguza heshima na kuwadhalilisha waliofariki na wafiwa. Tanzania ujuha mtupu. Kama hawa jamaa ndio wanataka kuja kuongoza nchi mimi nahama.
ReplyDeleteNajua hutapost hii lakini ujembe utaupata...Ni aibu kw ajambo kama hili serikali kuu haijaongea chochote kuhusu hili tukio na licha ya yote hata kutuma mtu kwenye hayo mazishi. Mhhhhh huko tunakokwenda sio salama...Na watu wameshapata picha kuwa kama wewe sio CCM basi serikali haikutilii maanani kabisa. wewe ni kama mdudu tu. Ina maana kwa vile ni watu wa chama kingine ndio maana hakuna kiongozi wa serikali kabisa? Waambie hao wmamoss wako twasira wanayoionyesha kwa wananchi sio nzuri kabisa....
ReplyDeleteMtanzania halisi
Mitoso mimi naona Uka karne ya16. Sasa kama mtu hakubaliani nakitu ndiya anyamaze asidai haki yake? Basi inge kuwa hivyo mkoloni Mjerumani ange kuwapo Mpaka leo. Nafikiri Mtoso unahitaji kuelewa wakati Ukuta na hiyo amani na utulivu unayo ifikiria ni ujinga kwa sababu siku hizi watu wengi wamesoma.
ReplyDeleteHaya mambo huwa yana time. Kila siku hukumbusha kuwa itakuja siku mambo yatafika shingoni, na wanyonge wataamua kuwa liwalo na liwe. Wataadvansi tu hata kama risasi za sisiyemu zitaendelea kumiminwa.
ReplyDeleteTunisia ni mfano wa nchi ambazo wananchi wake wamekuwa wakipewa kibano katika sekta mbali mbali. No kuandamana, limited freedom of press, no freedom of participation when it comes to multipartism, rushwa, uzembe wa serikali, ulimbikizaji wa utajiri wa nchi unaofanywa na viongozi waliopo madarakani, na mambo mengine kedekede.
Wananchi wamevumilia weee mpaka wakaona si kweli. Wameng'amua kuwa wanapigwa changa la macho. Rushwa na dili chafu kubwa zimekuwa halali, na vimambo vidogodogo ambavyo wananchi wamelazimika kufanya ili kuzuia wasife na njaa kama vile kuuza ndizi etc. vimekuwa sosi ya vijipolisi uchwara kujipatia rushwa. Hilo likazuwa tafrani, bila shaka kila mmoja ajua! Uprising inaendelea kupamba moto na kushika kasi ya ajabu. Polisi na askari wote pamoja na vifaa vyao hawajaona ndani.
Hali kama hii yaweza kutokea pia huko kwetu. Mambo mengi ambayo tumekuwa tukiyaona kwa wenzetu wa jirani au hata mbali sasa naona yanatokea kwetu, na kwa kasi ya ajabu. Tulikuwa tukiwabeza nchi nyingine duniani juu ya swala la udini, ukabila na rangi; mambo ambayo yameshachungulia na kujipatia nafasi nzuri tu katika jamii yetu. Mengi pia tuyaonayo yaja, tena kwa kasi. Hala hala mti na macho JK!! Ahsante kwa kutuandikia historia mpyaa. Tunakupenda, tena sana.
Kama walivyosema wengine, yaonekana wazi kuwa maisha ya watanzania (eti kwa sababu ni wachagga, wakristo, au kosa kubwa hata kama mtu anatoka katika kabila zuri, basi kutokuwa mwana sisyemu) hayana thamani zaidi ya ulaji wa viongozi.
Waweza kutoipublish hii ndude, lakini hata usipoitoa haitasaidia kuzuia ukweli uliopo ndani yake kubaki kuwa kweli.
Inasikitisha sana kuona Watanzania tulipofikishwa na sisiem, Viongozi kutokujali UTU na badala yake wana anagalia maslahi ya kijinga, Hivi Majambazi wamejaa wamewashinda polisi wanakuja kupiga watu mchana kweupe wakiwa hawana hata mshale mikononi? Inaingia akilini mtu anatetea kitendo hiki kilichofanywa na hao wanaodhani Nchi yetu imebinafsishwa kwao? Siku zao zinahesabika.
ReplyDeleteMitoso unasikitisha sana na maneno yako hayo.
Pole sana wafiwa..... Hii inaonyesha kuwa polisi wote wa TZ HAWANA ELIMUndio maana wanatumia nguvu bila kufikiria. Pia ni woga sana hawajiamini. Kama si woga wangesubiri kuona ni nini kingetokea ktk hayo maanadamano. Lakini si polisi tu wasio na elimu ni karibu watu ewngi kwenye dola. Angalieni Dr wa magonjwa anapelekwa kuwa waziri wa ulinzi.... kweli hapo hakuna elimu ya ulizi ni vurugu tupu... sasa hata mapolisi utakuta albda alifukuzwa ualimu, ndugu yake ambaye ni kigogo akamkabidhi bunduki awe askari bila hata kwenda kozi.....hapo tunategemea nini? Siku hizi vigogo wanapeana nyazifa hata kama ntu hajaenda shule husika. Kwa hiyo wa TZ TUTEGEMEE VURUGU ZA NAMNA HIYO...Lakini inauma sana poleni wahanga wa uongozi wa kileo
ReplyDeleteMtoso nakuonea huruma sana .... mtazamo wako si wa lizalendo....waliokufa pale wangekuwa kaka zako ungesikitika lakini kwa kuwa ni watu baki unaona sawa......Pole sana mtoso.unatia huruma kuliko.
ReplyDeleteNdugu zangu si kwamba mimi napingana na mabadiliko, ni kweli mabadiliko yanahitajika nchini kwetu ili basi kila mtu aweze kufaidi rasilimali zilizopo na si kama ilivyo sasa watu wanafanya maamuzi kiholela kana kwamba nchi imepoteza uelekeo.
ReplyDeleteKinachonikera mimi ni kuona baadhi ya hawa ambao nyinyi mnadhani ni manabii wanatuingiza kiini macho kwa kutumia mapungufu ya mfumo wa utawala uliopo na kuwashawishi watu wafanye fujo kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Angalia jinsi mazishi yalivyofanywa inaonyesha wazi kwamba wanachokitaka ni jumuiya za kimataifa wawaonee huruma...sasa mabadiliko hayaji hivi kwa sababu dhamira ya hawa kina Mbowe na mwenize Silaha mimi nilishagundua tangu muda sana kwamba si ya kweli..na uwezo wa kuleta hayo mageuzi ya kiuchumi hawana.
Uwezo wa mtanzania wa kawaida kuchanganua mambo ni mdogo sana hivyo ni rahisi kufuata mkumbo...ukijumuisha na mzigo wa matatizo yanayomkabili ni rahisi kushawishika kuchafua amani iliyopo..
Kushindwa kwetu kutambua mapema kwamba hili kundi la kina Silaha ni wanafiki ..ama kwa hakika nawambieni wengi wataumia na hakuta kuwa na mtu wa kulaumiwa.
Ni mimi Mitoso.
myonge mnyongeeni lakini haki yake mpeni, watu waruhusiwe kuandama kama katiba inavyosema. watu wameshika vitambaa vyeupe mnawapiga mabomu nini maana yake
ReplyDeleteHahahahahah...nimefurahi sana kuwa HAKUNA kurudia uchaguzi wa meya Arusha mjini. Pia kauli ya polisi jana kuwa uongozi wa nchi uliopo madarakani kihalali HAUTADHALILISHWA. Safi sana. Hizo ndio kauli tulizokuwa tunazisubiri kutoka kwenye serikali yetu tukufu. MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDelete