Ubalozi wa China nchini utaadhimisha mwaka mpya wa Kichina (Spring Festival) hapa Dar es salaam kwa siku mbili kuanzia tarehe 29/01/2011.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo viongozi mbalimbali wa serikali watahudhuria sherehe hizo kuanzia saa 10 jioni.

Aidha tarehe 30/01/2011 Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Fenella Mukangara atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za urushaji wa tiara (Kite Flying) ambazo zitafanyika eneo la wazi karibu na Hotel ya Golden Tulip kuanzia saa 10 jioni.

Sherehe hizo ni sehemu ya mila na utamaduni wa watu wa China ambapo hujumuika kwa pamoja sehemu mbalimbali duniani kusherehekea mwaka mpya.

Mwaka mpya wa Kichina huadhimishwa kila mwaka nchini China kwa kufuata utaratibu wa Kalenda ya Mwezi(Lunar Year) ambapo utaanza February 2,2011.

Imetolewa na :-
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo

ANGALIZO: Habari kuhusu sherehe hiyo
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. aaah, kumbe wa kichina basi utakuwa feki.......tih,tih,tih

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...