Beki wa timu ya Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza akijaribu kuondoa hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake katika mechi iliyochezwa jioni hii dhidi timu ya Simba ya jijini Dar,ndani ya uwanja wa Taifa.hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa ni Simba 1-1 Atletico Paranaense.
Mshambuliaji wa timu ya Atletico Paranaense,Gabriel Lima De Oliveira akijaribu kumtoka Rashid Gumbo wa Simba katika mpambano uliomalizika jioni katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Mshambuliaji wa timu ya Atletico Paranaense,Gabriel Lima De Oliveira akitafuta namna ya kutoka kipa wa Simba,Juma Kaseja.
Beki wa Atletico Paranaense,Bruno Costa De Souza akiondoa hatari langoni mwake.
Kiungo wa timu ya Simba,Patrick Ochen akiwatoka mabeki wa timu ya Atletico Paranaense katika mchezo uliochezwa jioni hii ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar.
mbilinge mbilinge langoni mwa timu ya Simba huku mshambuliaji wa timu ya Atletico Paranaense akigaa gaa chini mara baada ya kukutana na kijiji cha timu hiyo.hadi mwisho wa mchezo matokeni ni Simba 1 na Atletico Paranaence 1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hii mechi imechezwa siku 2 tofauti au ni vipi? mbona naona jezi tofauti tofauti timu ya atletiko!!!

    ReplyDelete
  2. Dah! kweli Simba ni kiboko yaani Yebo yebo walikung'utwa goli mbili bila lakini mfalme wa porini a.k.a wekundu wa msimbazi wamekomaa na kutoka droo.

    Kweli Simba ni wanaume,Yanga mdebwedo kudadadekiiii Simba oyeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  3. uncle..mambo vipi?? tunashukuru kwa kutuletea habari mbali mbali kutoka hapo nyumbani..kwa sisi tulioko mbali na nyumbani..tunafurahi tunaposoma habari za nyumbani kupitia global yako..!!sasa kwanini hutuandikii kwa kirefu na list za wachezaji wa timu zote walizocheza..!

    Ni hayo tu kwa leo..usiku mwema
    double d

    ReplyDelete
  4. Yanga walifungwa 3-2 sio 2-0.

    ReplyDelete
  5. ilikuwaje jana mbona naona kama jezi za wabrazil mara nyekundu mara nyeupe?au walikuwa wanaonyesha mitindo?

    ReplyDelete
  6. Simba wanatisha.Wametoka sare na timu mbili za Brazil kwa dakika tisini wakati watani zetu walifyata mkia dakika tisini kwa kucheza na timu mojawapo tu. Je, wagekipiga na tumu zote mbili ingekuwaje?

    ReplyDelete
  7. Ni ujinga kusifia draw na timu ya tatu ya Brazil.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...