Ankal,Salamalekoo..
Natumai humzima na unaendeleza vyema libeneke la Blogu ya Jamii.
Ankal mimi ni mdau sana wa blog ya jamii, napenda kusoma habari mbali mbali za wana jamii ila na mimi leo yamenikuta naomba unirushie haka kaujumbe ili jamii ielwe kinachoendelea na wenye nchi nao wapate ujumbe.
Ankel hii nchi imetufanya wazawa tuishi kama wakimbizi kwenye nci yetu wenyewe. Sijaona mimi nchi duniani inambana raia wake kama hii, yaani wanahakikisha wanawabana raia wake wasifurukute.
Ankel mimi nina kaduka kangu napika mikate hapa kimara ni kama kamama nitilie fulani tu kwa sababu nauza kama mikate mia tu kwa siku, wakaja jamaa wanadai wanatoka ofisi ya vipimo wanataka kupima uzito wa mikate, mimi nikawauliza wanaipima kwasababu gani?
wakasema inatakiwa ipimwe kwa sababu kuna standard ya mikate na bei zake ili nisiwaibie wananchi. Wakasema kupima item moja ni shilingi 30,000.00 Thelathini elfu, ankel nilitetemeka, nikawauliza mnapima kila kitu wakasema ndio na risiti ya serikali wanayo.
Mimi nikajiuliza natengeneza vitu kama kumi vitumbua,maandazi,crips,mikate ndizi, scones , chapati nk.
Ankel kupima tu kwa mara moja kama una items kumi ni laki tatu. Hao ni wamoja tu, kuna TFDA wanataka kucheki ubora wa itema kila item si chini ya dola 250, hawa ankel wanachaji kwa dola hapa hapa kwetu Tanzania, na wengine ni TBS , na wengine ni TRA na wizara ya Afya. Mimi naomba niulize Ankel hivi hawa wasimamizi wa sheria zetu wanajua kweli hesabu?????????????
hivi wanajiuliza huyu ng'ombe wanayetaka kumkamua hivi ana hayo maziwa au wanataka atoe damu??? Jaribu kufanya hesabu uone huyu mtu anatakiwa kulipa hizi kodi kiasi gani. Faida ya mkate mmoja kabla hujatoa labour charge ni shilingi 150.
Haiwezekani ukatengenezwa utaratibu ili mtu akienda kulipia leseni alipe vitu vyote vinavyohusu biashara yake ili kuepuka hii mianya ya rushwa? Nafikiri ikiwa pamoja inasaidia kujua biashara moja unaichaji kiasi gani kuliko hivi ambavyo kila mtu anataka kuchukua chake?
Sasa mimi nauliza hivi nikitengeneza mkata gm 500 nikauza shilingi elfu mbili na wateja wangu wako happy na wananunua kuna shida gani? na hata kama hawanunui hasara si yangu?????? kwani maana ya soko huria ni nini jamani?
Pili nauliza hawa wafanya biashara wa vitumbua na maandazi mitaani vimepimwa uzito? ua watu wanatafuta tu pa kuumiza wenzao? Hivi sisi Watanzania jamani hata kuuza maamndazi kwenye nchi yetu wenyewe tushindwe tutaenda wapi???
Sasa tunashangaa nini wale wawekezaji wa kichia wanaofanya umachinga si ndio tunavyotaka?? hatutaki kuona mmatumbi mwenzetu anapata. Mimi sielewi.
NAOMBA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA TUSAIDIANE KULIPA KODI TUSISAIDIANE KUKWEPA KODI TAFADHALI.
Ankel naona ntaandika hadi kesho naomba msaada wako kwa hili

Pole sana mdau kwa kweli ni habari ya kusikitisha sana kwa maana Serikali yetu inafuata mfumo wa kikoloni nao ni kunyonya wananchi wao kwasababu toka uhuru upatikane wazalendo wameshindwa kutunga sheria za kizalendo zenye kulenga kumkomboa na kumuendeleza mwananchi wa kawaida. Serikali haina msaada wowote kwa mwananchi wa kawaida lakini huyo mwananchi wa kawaida akijututumua ili ajiondoe kwenye dimbwi la umasikini serikali inakuja na nyundo kuvunja.. wameweka ukuta wa maendeleo ni matajiri tu ndio wenye kuruhusiwa kuzidisha utajiri wao halafu wanapanda kwenye majukwaa kuhubiri uongo wa maendeleo..
ReplyDeletePole ndugu yangu yaani hiyo nchi yetu imejaaa watu wenye roho za ubinafsi na wizi. Inasikitiha sana lakini ndio wanavyopata mifano toka kwa hao walio juu yao. Unategemea nini? Mimi Tanzania kwetu lakini kumenishinda. aliye nacho anacho asiye nacho hata hicho kidogo ananyang'anywa. Uliza watoto wa kinafulani wenye mabiashara kila kona hapo mjini Dar nani anawasumbua? Hizi dhambi watatubia wapi jamani?wanafikiri watabeba waende navyo lakini siku moja watakuja kugundua kwamba wataondoka kama walivyo. waache wakazane tu biblia inasema maskini na tajiri wote watakutana kuzimu. Patamu hapo!
ReplyDeleteWatanzania bado tumelala...angalia TUNISIA na MISRI...wameshachoshwa na wezi! Siku moja tutaamka na kugangamara!
ReplyDeleteMdau kutoa salaam unasema Asalaam Aleikum!
ReplyDeleteHayo mambo ya kila mtu kutumia ofisi yake kudhulumu watu wengine ni sugu mno!Ni hatari sana, Pole Mdau. Bado watakukamua kwenye umeme na Dowans yao, Nchi la Nyerere hilo balaa tupu!
Hehe na bado unafikiri Dowans italipwaje?, kweli ndio maisha bora kwa kila mtanzania. Wadanganyika siku hizi hawadanganyiki tena siku isiyokuwa na jina tutakuwa kama Misri na Tunisia nyie chezeeni tu watu
ReplyDeleteMdau wa Sat Jan 29, 09:09:00 PM 2011, nawe inabidi ukaipige mswaki shule yako ya lugha ya kiarabu.
ReplyDeleteMdau mtoa mada aliyeandika 'Salamaleko' yuko karibu zaidi na usahihi kuliko wewe. Kwa usahihi ilibidi aandike 'Salaam Aleik', kwa kuwa analmsalimia bwana 'Ankel' ambaye ni mtu mmoja asalimiwaye (singular). Asalaam Aleikum hutumika, kwa usahihi, kusalimia zaidi ya mtu mmoja. Yaani, kama unawasalimia watu wawili au zaidi kwa pamoja inabidi useme 'Asalaam Aleikum (aleikoum/aleykoum). 'kum' au 'koum' ni kionyeshi cha uwingi!
He heee, ntafungua GUBOLU (bilogi) la lughat el araabiyaa! vere suun.