Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Mapinduzi nahodha wa Simba Sc Nicco Nyagawa baada ya timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar kuilamba yanga bao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika usiku huu uwanja wa Amaan Stadium Zenji
Rais wa Zanzibar akiwa na viongozi wa michezo
akiwatakia mchezo mzuri watani hao wa jadi
mojawapo ya eksheni katikati ya uwanja usiku huu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akipozi na kikosi cha Simba kabla ya mchezo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akipozi na kikosi cha Yanga kabla ya mchezo
Moja haikai, mbili haikai na rivasi ndio imegoma kwa kocha wa Yanga Kondic Papic wakati wa kipindi cha lala unono na Simba wako mbele kwa bao 2-0.
Kina Ras Makunja walikuwa hawana msalie kabisa. Hata kocha wa Simba nusura azuiwe kwenda kwenye benchi la ufundi
Ras Makunja akimzuia daktari wa timu wa Yanga kwenda benchini
Wachezzji wa Simba wakichekelea ushindi
Simba woyeeeeeeeeee...
Picha zote na habari na
Francis Dande wa Globu ya Jamii

Klabu za Yanga na Simba za Dar es salaam zimepambana usiku huu katika fainali ya kombe la Mapinduzi Cup ambapo Simba wameondoka kidedea kwa kuinyuka Yanga bao 2-0 na kutwa ubingwa wa kombe hilo, katika michuano iliyoshirikisha timu za bara na visiwani.
Mussa Hassan Mgosi na Shija Mkina ndio wafungaji wa magoli hayo. Mabingwa wa mwaka jana walikuwa Mtibwa Sugar.NA MPIRA UMEKWISHA...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. uncle,mbona umetoa ujumbe kwa masikitiko?kwi kwi

    ReplyDelete
  2. KANDAMBILI ZIMEKATIKA MARA MBILI YAKHEEEEE JAMAAA KALIWAAAAAA!!! Goli Ngapi Yakheee ah Mbili tuuu Tehtehteh! . MZ.

    nani kasema mnyama usiku haoniiiiiiiiiiii ????? Mwanza kule ilikuwa mbinu ya kuwafurahisha CCM tu tuliwaachia kwajili ya Uchaguzi na sare za CCM. Michuziii upoooooo???

    ReplyDelete
  3. kweli simba tunatisha sasa ni zamu ya migogolo ichukue nafasi jangwani maana fedha za manji hazijasaidia kitu SIMBA oyeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  4. huyu askari naona ana ugonjwa wa akili ina maana kama kocha nae hatakiwi benchini inakuwaje au alipewa kadi nyekundu? ndo mana tunaambiwa askari wetu wanahitaji maarifa na si miguvu!

    ReplyDelete
  5. MAFUNZO YA HAWA MAPOLICE WETU WANAPEWA ZAIDI PRACTICAL KULIKO THEORY KWANI WAO WANAKUWA NA GAZABU HATAPASIPO TAKIWA ASWA WAKIWAONA WAKUBWA NDO SIFA ZINAPANDA NI VICHEKESHO UNAZUA KOCHA MADAKTARI , UNAZUIA ZUIA TU PILA HATA KUULIZA ! ASARA TUPU

    MDAU PARIS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...