Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki (katikati mbele), akiwa na wanamuziki wapya kutoka bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akiwatambulisha wanamuziki hao kwa waandishi wa habari. Wanamuziki hao waliojiunga na bendi hiyo ni Mwimbaji Rogert Katapillar, Rapa wa bendi hiyo Saulo John 'Ferguson' ambaye aliibukia katika bendi hiyo hiyo ya Extra Bongo na Kiongozi wa Wanenguaji wa Twanga, Super Nyamwela, Danger Boy na Otilia. Picha na John Bukuku

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. MMMhhhhhh hapo ni kazi kweli kweli safari hii...ngoja tusubirie matokea

    ReplyDelete
  2. Siyo ajabu kwa wanamuziki kuhama bendi,hii yote ni kutafuta maisha,hakuna haja kabisa ya kulaumu kitendo hiki maana hata hiyo Twanga pepeta huvunja bendi za wenzao.Kwa wanamuziki hii ndiyo changamoto ya kujiendeleza kimaisha, pia twanga imekuwa na wanamuziki wengi kiasi hata wengine huwa wamefunikwa kabisa ni kama hawapo ktk bendi,niliangalia video ya twanga "mwama dar-es-salaam"ukihesabu waimbaji 10,wacheza shoo 10,wapinga vyombo 10 !!!yaani jumla watu 30 mbali na mafundi mitambo nk.sasa hizi si bendi tatu jamani !!!Big up Rogat Hega na wenzako huu ni wakati wa kuamka na siyo kutumiwa na twanga kwa kuwatajirisha wamiliki na msirudi nyuma !!!!!.naomba hii isiminywe
    ankal,maana habari yoyote mbaya ya Twanga huwa humuoitoi tumegundua tatizo hiliktk blog hii ya jamii.
    mdau Mikocheni Dar.

    ReplyDelete
  3. Ni sawa hata mimi nawaunga mkono wanamuziki waliotoka Twanga,Ukiangalia sana huwa wanafanyishwa kazi kama punda,hawana hata muda wa kupumzika na malipo ni madogo,pia wao hunaswa kwenye mikataba inayowafanya wawe kama watumwa !!!!Huu ni wakati wa kuamka usingizini wasanii msikubali kutumiwa na hawa wamiliki wa mabendi,pia muwe na wanasheria watakaokuwa wanaipitia mikataba yenu kabla ya kusaini.Muziki na sanaa kwa ujumla ni ajira kama ajira nyingine yoyote pia ina manufaa kama kutakuwa na mikataba ya kueleweka.Kazi kwenu Twanga,nadhani huu ni mwanzo tu bado kuna wanamuziki wengine watatoka hivi karibuni.Ally Choki kaza buti wala usihofu huku ndiko kukomaa ki maisha nasi tutakupa tafu tu bila kusita.
    Mpenzi wa muziki Vijana Hostel.Kinondoni Dar.

    ReplyDelete
  4. DUH choki utawaweza hao twangapepeta kweli?. subiri majibu yao

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Mikocheni usitake kumuonea Ankal. Mbona kaitoa hiyo comment yako sasa. Kama mwenyewe ulivyosema Twangapepeta wana wanamziki wengi sana,sasa hicho ni kitu cha kubania kisitolewe. Manake wanamziki kwao kutoka na kurudi ni kitu cha kawaida na ndiyo maana utakuta bendi haiathiriki hata mara moja kutokana na wao kuwa na shehena kubwa ya vipaji. Elewa kwamba ASET inayomiliki bendi hiyo ya Twanga moja ya majukumu yake nikuvumbua vipaji, kuvilea na kuvipatia ajira ndani na nje ya nchi. Ndiyo maana utaona huwa hawatetereki hata wakiondoka wanamziki sita kwa mpigo, kwani wanakuwa na hazina kubwa always. Sasa ukiangalia hapo walioondoka ni mwimbaji mmoja na rapa mmoja, wakati wako wanawaimbaji 11. wengine watatu ni madansa tuu wakati Twanga kuna madansa 14. Kuna kuyumba hapo kweli?.

    ReplyDelete
  6. Ni vizuri wapungue kwani watu wakijazana wengi wanaweza kuathiri hata ufanisi katika kazi, kwa kutegeana na kupigana majungu

    ReplyDelete
  7. ANONY WA MIKOCHENI HAPO JUU, MBONA HIYO HABARI NI NJEMA TUU KAMA NI HIVYO. TWANGA PEPETA NI BENDI YA JAMII KAMA ILIVYO BLOG YA MICHUZI.vijana wamejipunguza katika kutafuta maisha pengine. Na twanga kutokana na na,mba kubwa waliyokuwa nayo mimi naona ni vema wakawapunguza wengine. Wabaki kama 15 kwa ujumla wao, kazi itakuwa bomba zaidi na itakuwa rahisi kuboresha maslahi ya group dogo kulipo linapokuwa kubwa

    ReplyDelete
  8. 'Mzee wa farasi' mtafute na 'kocha wa Dunia' ukamilishe kikosi. Palipo na ushindani ndo kuna huduma bora!

    ReplyDelete
  9. Jamani jana nimeenda MANGO walikopiga hawa jamaa wa Twanga pepeta usiku wa kuamkia leo, kulifurika utadhani hakuna starehe sehemu nyingine. Jamaa walipiga kazi tokea saa tatu usiku mpaka saa kumi alfajiri, watu wakawa bado hawataki kuondoka kutokana na jamaa walivyoamua kukamua. Kuna rapa huyo anaitwa Msafiri Diof ni funga kazi, kutokana na rap zake zilivyochengua watu.

    ReplyDelete
  10. Kocha wa dunia Muumin Mwinjuma inasemekana ameomba kujiunga twangapepeta na jana alikuwa mmoja wa kivutio pale alipopanda kwenye stage na kuanza kuimba wimbo mpya wa Twangapepeta uitwao KAULI walioimba na BOZI BOZIANA

    ReplyDelete
  11. BREAKING NEWS. Inasemekana Twangapepeta wamejibu mapigo kwa Chief Kiumbe ambaye ndiye mwajiri wa Ally Choki,kwa kumrudisha mpiga solo John Kanuti na pia imemchukua kiongozi wa EXTRA BONGO ajulikanaye kwa jina la KHADIJA MNOGA a.k.a kimobitel.
    Lol, Kaz kweli kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...