Waheshimiwa wabunge wa CHADEMA wakiondoka ukumbi wa Bunge kususia upigwaji wa kura wa kukubali ama kukataa kuwepo kwa kambi ndogo ya upinzani, na wao kukubali kujumuisha wabunge wa vyama vingine kwenye serikali kivuli ya kambi ya upinzani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ujinga mwingine wa watu tunaowaita wawakilishi wetu sasa nani atatuwakilisha na kutoa kilio chetu bungeni kama huu mchezo utaendelea? Chadema tumewachagua siyo kwa kukimbia vikao hebu kaeni chini mlifikilie hili suala kabla hamjalia uchaguzi ujao...

    ReplyDelete
  2. Nawaunga mkono wabunge wa Chadema kwa sababu ni vichwa, kwa mtu mwenye ubongo wa shake well before use unaweza hawapo sahihi.
    Suala la chama cha CUF kuwa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa kwa kushirikiana na CCM huko Tanzania visiwani, lakini kwa wakati huo huo kikataka kujiunga kwenye kambi ya upinzani hapa Tanzania bara, kwaminajili ya kupinga serikali inayoundwa na chama ambacho ni mshirika wake huko Tanzania visiwani, lina utata wa kisheria, hivyo nashauri wahusika walipeleke suala hilo mahakamani lipatiwe tafsiri iliyo sahihi.

    ReplyDelete
  3. Wewe kanjanja hapo juu una akili lakini?
    Hao CUF wanalazimisha mambo ya kule kisiwani yatokee na huku balaa wananchi tumewashtukia na mwaka 2015 watapata wabunge wasio zidi 5 wanajimaliza wenyewe na kwanza wewe any.10;50;00 hukuichagua Chadema

    ReplyDelete
  4. Duu kazı kweli kweli yaani nchi yetu inaelekea pabaya sana,matatizo mob kwani wakiungana na wenzao wa upinzani kitapungua nini na nguvu itakuja vipi kama haa wapinzani wanataka makundi kibaoo!!Chadema kweli matatizo tuu !

    ReplyDelete
  5. REVOLUTION.... WABONGO MMESHAZOE KUONA WATU VICHWA CHINI SASA HAOOO... THEY DARE TO PROTEST.. NA WATAPATA KURA YANGU NEXT TIME...

    ReplyDelete
  6. ....CUF, you can't eat your cake and have it! Kwa kuwa CUF ni chama kimoja, haiwezekani kikawa ni chama tawala visiwani na wakati huo huo kikadai kuwa chama cha upinzani bara, no way! CUF ni chama tawala tu kama sisiemu. Wasitake kutuulia upinzani bara, washindwe na walegee!

    ReplyDelete
  7. Nyie mnaoitetea chadema naona hamna akili timamu! kwa sababu KEnya kuna mseto mbona watu maisha yao yanawaendea! Chedema tumewastukia! hawafai kuongoza , hivi hawa wakipewa madaraka tutapona kweli???

    ReplyDelete
  8. asante mh spika kwa ufafanuzi Mzuri..tuna mambo mengi ya msingi ya kujadili sio kupoteza muda kwenye kupiga magoti sijui na kuinamisha kichwa au mkunjo wa goti...kwa hilo kula dala makinda

    ReplyDelete
  9. CHADEMA... mpo bungeni kwa ajili ya maslahi yetu au yenu? Yaani bado mnalilia uongozi tu! Sasa kwa nini mna protest kwa kutoka nje? Ina maana hoja zenu hazina nguvu? Acheni hizo

    ReplyDelete
  10. Wakiondoka, wanyimwe matupurupu...watarudi upesi sana!

    ReplyDelete
  11. Watu msilopoke hovyo, kwani hoja waliyoipinga ilikuwa inahusu uwakilishi wa matatizo ya wananchi? Sawa kabisa watu wamechoka kuona CCM na rafiki zao wakipindisha sheria kutaka kuua upinza. Huwezi kuwa mtawala hapohapo kwenye upinzani wapi na wapi? Aliyefananisha na Kenya nadhani hajui kuwa Kenya na umoja wa wapinzania ndio unatawala ni tofauti kabisa na TZ.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...