JK akiwa katika ,mazungumzo na Makamu wa Rais Dr.Mohamed Gharib Bilal(watatu kushoto),Waziri mkuu Mizengo Pinda(wanne kushoto) pamoja na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo jioni akitokea nchini Ivory Coast ambapo alishiriki katika juhudi za kutatua mgogoro wa kisiasa nchini humo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Karibu nyumbani mkuu... Lakini nauliza, je hii protocol ya kuwa na wapambe kumkaribisha mheshimiwa kila anapotoka safarini haujapitwa na wakati?
    Tukumbuke, huko barabarani kuna ishu kubwa sana ya foleni kila kona, nyingine husababishwa na mipango ya kuwakimbiza maofisa kwenye mapokezi kama haya wakati sidhani kama yanaongeza kitu chochote cha muhimu katika uongozi ila kero nyingi tu kwa watumiaji wa barabara
    Naweza kutoa tu mfano mzuri ambao unaweza kutumika... Pawe na maongezi mafupi tu na waandishi wa habari kutufahamisha matokeo muhimu ya safari uliyoifanya, viongozi wengine hapo watakuwa kazini kuendeleza ujenzi wa taifa.
    Karibu mkuu...

    ReplyDelete
  2. Mimi nafikiri haya mapokezi yangeweza kufanyika Ikulu itakua rahisi zaidi kwa viongozi husika kufika na kushiriki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...