Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda (katikati) akiwa katika matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM katika sherehe zilizofanyika kijiji cha Tungamalenga jimbo la Ismani wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa mkoa ambao Mh. Pinda ni mlezi wa CCM. Kushoto kwake ni mkewe Mama Tunu Pinda na kulia kwake ni mbunge wa jimbo hilo Mh. William Lukuvi ambaye pia ni Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu anayeshughulikia sera na uratibu wa bunge
Kamanda wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa Salim Asas (kulia) akiagana na waziri mkuu Mizengo Pinda katika uwanja wa ndege Nduli baada ya waziri huyo ambaye ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa alipomaliza ziara yake ya kuadhimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM ,sherehe zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Tungamalenga jimbo la Ismani wilaya ya Iringa. Picha na habari na mdau Francis Godwin

WAZIRI mkuu Mizengo Pinda amewaonya mawaziri na wabunge kufanya kazi kwa kujituma zaidi badala ya kuendelea kujivunia vyeo ambavyo wamevipata na kuwa mchakato wa kukifanya chama cha mapinduzi (CCM) kuendelea kuwa imara umeanza ili kutenganisha siasa na biashara .

Pamoja na kauli hiyo pia amewaonya wakurugenzi wa wenyeviti wa Halmashauri za wilaya ambao wameontyesha kushindwa kuwatumikia wananchi na kuendekeza starehe za ziara .

Waziri mkuu ambaye ni mlezi wa CCM mkoa wa Iringa alitoa maagizo hayo leo wakati wa maadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kimkoa kwa mkoa wa Iringa katika kijiji cha Tungamalenga wilaya ya Iringa .

Alisema kuwa CCM ni chama chenye nguvu sana ila baadhi ya wagombea wa nafasi mbali mbali ambao wanaingia ndani ya chama hicho kwa ajili ya kujinufaisha ndio ambao wamekuwa wakifanya watu kujenga chuki na CCM na serikali yake jambo ambalo halitavumiliwa kwa mbunge ,ama kiongozi awaye yeyote ambaye atashindwa kutimiza wajibu wake.

Waziri Pinda alisema kuwa wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiuza nyumba zao ili kugombea ubunge na udiwani na baada ya kupewa nafasi hizo wamekuwa wakitumia muda mwingi kufikiri jinsi ya kurejesha nyumba zao badala ya kuwatumikia wananchi na ndio sababu ya CCM kuanza mchakato wa kutenganisha siasa na biashara .

Hata hivyo aliwataka viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kufanya tathimini ili kujua sababu ya kura za mgombea urais wa CCM kupungua zaidi katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana na kama tatizo ni nguo ambazo zimekuwa zikitolewa na CCM basi kuangalia uwezekano wa kuziuza nguo hizo badala ya kugawa bure.

Pia aliwataka wataalum kuepuka kukaa maofisini huku wakipata viyoyozi na badala yake kutoka kwenda kwa wananchi ili kujua matatizo yao yanayo wasumbua kama njia ya kupunguza vilio vya wananchi kwa serikali yao.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...