Familia ya Inj. Mbogo Futakamba inapenda kutoa shukurani za dhati kwa Ndugu, Jamaa, Marafiki, Wafanyakazi na Majirani wote waliojitoa kwa hali na mali katika msiba wa Bibi Gloria Mbogo Futakamba aliyetangulia kwa BWANA tarehe 12/01/2011 na kuzikwa tarehe 15/01/2011 kwenye makaburi ya Kinondoni – Dar es Salaam.
Shukurani ziwaendee Wafanyakazi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Wizara ya Maji, Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Mamlaka za Maji nchini (UWSA’s), Ofisi za Mabonde ya Maji (BWO’s), Kanda za Umwagiliaji (ZIU’s) EWURA, DAWASCO, DAWASA, Mawaziri na Manaibu Waziri pamoja na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Washirika wa Maendeleo ya Sekta ya Maji (DP’s) Maaskofu na Wachungaji wa Makanisa ya TAG na BCIC, Umoja wa Kinamama UPENDO WOMEN GROUP – Kinyerezi na Majirani wote wa Kinyerezi.
Shukurani za pekee ziwaendee madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Tabata kwa huduma yao nzuri.
Kwa kuwa hatuwezi kumshukuru kila mtu binafsi na kumuorodhesha tunaomba ujumbe huu upokelewe kama shukurani zetu sisi wanafamilia. Asante.
“NIKASIKIA SAUTI KUTOKA MBINGUNI IKISEMA ANDIKA, HERI WAFU WAFAO KATIKA BWANA, NAAM, ASEMA ROHO, WAPATE KUPUMZIKA ……..” UFUNUO 14:13

mungu mkubwa ,wote twaelekea huko.nikumshukuru mungu kwani yeye ndo mwamuzi wa kila jambo,kwa kupitia vifo vya wapendwa wetu ,tuna pata mafunzo na kutukumbusha sisi wanaadamu,dunia hii ni ya kupita,tusijisahau.nilimpenda sana shemeji yangu. kaka s.
ReplyDelete