USHARIKA WA KKKT KIJITONYAMA NA KWAYA YA UINJILISTI KIJITONYAMA TUNATANGAZA KWA MASIKITIKO MSIBA WA MWENYEKITI WA KWAYA YETU MR. EDMUND MUSHI KILICHOTOKEA TAREHE 06/02/2011 KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, MAZIKO YAMEFANYIKA MACHAME MOSHI TAREHE 09/02/2011, MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI,

AMEEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi. Familia ya wanamichezo hasa wa volleyball tutamkumbuka sana Edmund, alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya mpira wa wavu, mchezaji mahili, kiongozi wa kuigwa na mfano halisi kwa wachezaji wa volleyball.nakumbuka miaka ya 90, nikiwa kiongozi wa timu ya taifa ya wavu kule Nairobi kwenye mashindano ya kanda ya 5, tulikumbwa na wakati mgumu sana kifedha kwa wachezaji. Marehemu akiwa nahodha wa timu, alisaidia kuweka mambo sawa kwa kutumia pesa zake na kuwezesha timu kumaliza mashindano.

    ReplyDelete
  2. Jamani Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen

    Poleni sana wafiwa woooote na zaidi mke wake Susan Matingas Mungu hatakuacha Suzi usimlilie alieondoka bali jililie wewe na nafsi yako.

    ReplyDelete
  3. RIP kaka.. Wafiwa poleni sana.

    ReplyDelete
  4. RIP kaka Mushi...Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  5. Tutakukumbuka mpendwa Edmund, RIP.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana wafiwa. Mungu amueke pema. Tulikuwa naye wakati wa YMCA Volleyball team huko Dar katika miaka ya 88 na mapaka nilipondoka 92. Namkumbuka sana sana. Ni masikitiko makubwa kuondoka kwake.
    Sinan
    Dubai

    ReplyDelete
  7. I know Edmund kama mzee wangu wa kanisa pale Kijitonyoma Lutheran. kWAKWELI NIMEKUWA SHOCKED kuiona hii news hapa. Ila napata faraja kwani kuna makao mpya tuliahidi pale alipo yeye na sisi tutakuwepo... Tulimpenda MUNGU kampenda zaidi... MUNGU awape faraja familia kwenye kipindi hiki kigumu na poleni kwaya ya uinjilisti kwa kupoteza mwenyekiti wenu

    ReplyDelete
  8. HUYU MZEE alikua zaidi ya baba kwa familia na zaidi ya mume kwa mke wake suzi.pia zaidi ya mwenyekiti kwa kwaya ya uinjilisti kijitonyama.ameondoka kishujaaa na ushindi kwa vita ya shetani,sote tutamani jinsi alivyoishi kwa imani na utumishi mwema.tutamkumbuka sana.naamini sasa animba na kusifu pamoja na malaika mbinguni.MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU EDMUND MAHALI PEMA PEPONI,AMEN!

    Abel
    kijitonyama-DSM.

    ReplyDelete
  9. Tulimpenda sana lakini Mungu kampenda zaidi. E. Mushi alikuwa Mwenyekiti wa Kwaya yangu ya Uinjilisti, mzee wa kanisa, mwenyekiti wa kwaya za UKUU na n.k. Mungu awe FARAJA katika familia yake wakati huu mgumu. RIP

    ReplyDelete
  10. .......baba mdogo umetutoka ulikuwa unatupenda na kutuongoza vizuri wanao kwa moyo wote..ulinipeleka airport nikiwa naelekea kusoma mwaka jana ukiwa na mama yangu SUZAN MATINGA laiti ningetambua ningerudi tena kusema kwaheri......WE LOVED YOU SO MUCH.......REST IN PEACE BABA MDOGO......pole mama yangu SUZAN MATINGA MUNGU AKUPE NGUVU.....WADOGO ZANGU NARU,BRIGHT,ELINA,COMET NAWAPENDA SANA.....POLENI TRA NA KIJITONYAMA......REST IN PEACE EDMUND MUSHI
    NEEMA
    INDIA

    ReplyDelete
  11. Mungu aliyetupa kushuhudia maisha yako ya Kikristo, atusaidie sisi tuliobaki kuiga maisha haya ya ushindi kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu akutie nguvu Suzan, tumejifunza sana toka kwako kwa moyo wa Ukriso na kujitoa kwako kwa ajili ya mwenzio.

    Ni imani yangu Mungu hatakuacha pamoja na watoto. Natoa pole kwa Usharika na kwaya yake ya Uinjilisti. Tuseme kama Ayubu; Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe.

    Amin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...