Ajali hii imetokea leo mchana maeneo ya Igeme, Mahenge. Hilo roli limesheheni mafuta aina ya DIESEL likitokea Dar. Hakuna maafa yaliyotokea, ila ile tabia ya kukimbilia ma-roli pindi yanapopata ajali yakiwa na shehena ya mafuta kwa kujipatia kipato bada ipo katika jamii ya Watanzania kama uonavyo pichani. Ilibidi Polisi waje kuwatawanya raia waliokua wamefika hapo tayari kwa kulishambulia tenki. Mmiliki wa roli hilo alituma mapema gari jingine kwa ajili ya utaratibu wa kuhamisha wese hilo. Polisi nao walifika mapema na kufanikiwa kudhibiti usalama wa mali na uhai. Picha na mdau Remsi Francis SungwaGari la Polisi na askari eneo la tukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...