Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria mchezo wa soka kati ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya ‘ Bongo Fleva ‘ na timu ya Moro All Stars ya wachezaji wa zamani waliowika katika timu mbalimbali za ligi kuu Tanzania bara katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro leo. Mchezo huo ulikuwa ni maalumu wa kutafuta fedha za kuwachangia walioathirika na mabomu ya Gongo la Mboto, wenyeji walishinda bao 3-1.
Mwamuzi wa mchezo kati ya timu ya Morogoro All Stars na Bongo Fleva , Hamis Kambi ( wa pili kutoka kushoto) akizungumza na manahodha wa timu hizo, Kharid Ramadhan ‘ aka Tundaman ( Bongo Fleva kulia) na Profesa Madundo Mtambo ( Moro All Stars wa pili kutoka kulia) kabla ya kuanza kwa mchezo wao maalumu wa kutafuta fedha za kuwachangia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, wenyeji walishinda bao 3-1.
Mlinda lango wa timu ya soka ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, Kharid Ramadhani ‘ak a Tundaman’ akidaka mpira uliotokana na kona iliyochongwa na mchezaji na aliyekuwa Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa , Taifa Stars, pamoja na Mtibwa Sugar , Mecky Mexime ( hayupo pichani) wa timu ya Moro All Stars , katika mchezo huo wa kupata fedha za kuwachangia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, wenyeji walishinda bao 3-1


Unene!! Unene!!Matumbo hayo!!!? Jamani wakati umefika wa kuielimisha jamii kuwa overweight & obesity ni tatizo. Waliosoma ndo kwanza wanabobea kwa kunenepa bongo ili mbaya. halafu wanakwepa kula vyakula organic-vilivyozalishwa na mkulima nchini. This is the next Bomb linalosubiri kulipuka in Tz. Magonjwa ya moyo, visukari nk vitaigharimu sana nchi in the future hasa ukizingatia umasikini na uchumi mbovu wa nchi. Nyerere alihimizi watu wafanye mgambo angalau. But now I don't know kama serikali inaongelea hili au ina mkakati wowote. SORRY ni tatizo hili.
ReplyDeletewewe mdau hapo juu acha watu wanenepe tatizo liko wapi < magonjwa yote yanatibika sikuizi kwa BABU . au wewe hujui .
ReplyDeletebongofleva wanashinda kwenye mashindano ya kutoa misaada tu... oyeeee!
ReplyDeleteduhh.madundo kishaukwaa u profesa??big up sana madundo.nakumbuka aliwahi kuipiga simba goli 2 miaka ya tisini.wakati huo akichezea reli ya moro,"kiboko ya vigogo "
ReplyDelete