Mama akimfunga kamba kijana Hassan ili
kumdhibiti nyumbani kwao Tanga


Na Francis Godwin, Tanga
"... wewe kaka acha tu! huyo ni mkorofi sana hivi ukimfungulia kamba hapa anazunguka mitaa yote ya mji wa Tanga na hapo alipo ana majeraha ya kupigwa na kuchanjwa na nyembe kutokana na ukorofi wake hivi tumeaona njia pekee ni kumfunga kamba na kumchunga kama ng'ombe akiwa malishoni japo na usiku akilala tuna mfunga kamba pale anapolala" alisema mwanamke huyu.

Hata hivyo anasema mbali ya kufungwa kamba pia kwa upande wa chakula wamekuwa wakimwekea katika sahani yake maalum na kula akiwa amefungwa kamba huku kwa wiki ama mwezi huoogeshwa mara moja.

Alisema kuwa sababu za kufungwa na kutengwa na familia ni kutokana na tatizo hilo la utindio wa ubongo linalomkabili na kupelekea hali ambayo ndani ya familia yao wamekuwa wakiona kama ni aibu kwa kijana huyo kutembea mitaani na tatizo hilo.

Pia alikili kuwa kijana huyo amekuwa na uwezo mkubwa wa kutambua japo hajapata bahatika kupelekwa shule na kuwa sehemu kubwa hata kutamka baadhi ya maneno ameanza kujifunza baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kumfunga kamba nje ya nyumba hiyo na hivyo kubahatika kujifunza kuongea kwa kusikika kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakipita eneo hilo.

“Ujue awali tulikuwa tukimfungia ndani pasipo kutoka nje na jua ameanza kuliona sasa ndani ya miaka mitano hii ila awali hakuwa anatoka nje kabisa na kila huduma alikuwa akipewa ndani na siku zote alikuwa ni mtu wa kushinda ndani amefungwa .....kakangu wewe usimwone hivi huyo hapa ukijaribu kumfungulia kamba atazunguka mitaa yote kuingia katika nyumba za watu na kufanya vurugu hadi wenyewe wanampiga na kumchana na viwembe ....kwa usalama wake na kutuepushia aibu tumeona ni vema kumfunga kama ng’ombe wa maziwa hapa katika kamba”

Hata hivyo alisema kuwa kijana huyo amekuwa akifungwa kama na mama yao mzazi kwa maagizo ya baba yao na kuwa zimekwisha fanyika jitihada mbali mbali za kujaribu kumtibu katika hospitali ya mkoa wa Tanga kiasi cha kijana huyo kuanza kupona ila wazazi wake walimkatisha dozi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha kwa maana ya kuwa na nauli ya daladala ya kwenda Hospitali mara kwa mara.

“Hapa unapomwona Hasani ni kama amepona kwani hakuwa hivi alikuwa ni zezeta kabisa ila sasa hivi kutokana na kutibiwa ameanza kupona na kuwa na uelewa hata wa kutambua jambo...”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwa kweli inasikitisha sana na mateso makubwa!.....hope baada ya hizi taarifa, labda anaweza kusaidiwa na vituo ambavyo vinashughulikia watoto wa aina hiyo! So sad...

    ReplyDelete
  2. This is a brain damaged child, very sad indeed.wazazi wake wameteseka sana kumlea miaka yote hiyo iliyopita.Tatizo moja kubwa ni kwamba ni rahisi kidogo kumlea alipokuwa mdogo na sasa amekua ana nguvu na bila shaka mkorofi sana, na wazazi wazeeka.He should not be at home, he should be in an institution, but are there such facilities in Bongo? Very sad indeed

    ReplyDelete
  3. Inatia huruma sana. Lakini haya yote kwa vile serikali haijihusishi na ustawi wa jamii kabisa. Hivyo kila kitu ni mikononi mwa aliyekileta kiumbe chage duniani.

    Niliona habri ya wakenya pia wanavyo wafunga watu wenye ugonjwa wa akili kwenye CNN international nililia. lakini kama ninavyosema hii yote ni kwa vile serikali haisaiidii wala kuwezesha watu kuelewa kuwa ugonjwa huu sio aibu kwa familia..

    Serikali hata kama haitasaidia kutunza basi ingesaidia japo kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala haya. Kwa wenzetu hawa wanatuzwa vizuri tu na wengine wanapewa dawa na kuweza kuishi na kujitegemea wenyewe.

    ReplyDelete
  4. Mdau USA-(Home Health Aide,Direct Support Professional,Nurse aide)March 18, 2011

    Nimesikitika sana jinsi hawa watu waisvyonathamni nyumbani, maana hawa watu ndo wanatuweka mjini huku SANAAAAA tu tukichoka kupiga box .

    ReplyDelete
  5. hivi polisi wana habari jambo kama hili linatokea hapo tqnzania. hii ni aibu kubwa sana. kwanini huyu mamu ana mfanyia mtoto wake unyama kama huo. jambo kama hilo likitokea huku ninakoishi huyo mama ange enda jela na huyo mtoto angechukuliwa na kulelewa na watu wengine. huyu mama anatakiwa apate adhabu kubwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo. i am sure tuna watu wenye kutetea haki za watoto nchini mwetu, ninaomba msilinyamazie hilo jambo.

    ReplyDelete
  6. Polisi hiyo siyo kazi yao. Kuna wizara ya watoto na wakina mama, kuna ustawi wa jamii, hao wote kai yao kubwa ni kuendeleza jamii kwa ujumla. Lakini kwa wenzetu hapa nyumbani kazi yao kubwa ni kukaa ofisini na kunywa chai, tumekwenda shule bwana kazi za kwenda majumbani mwa watu siyo yetu. Na kama manbisha hatuna watu wa kusema chochote kuhusu huyu mtoto kutoka huko uatwi wa jamii au wizara ya watoto na wanwake. Watu wanpata kazi ni kunywa chai tu, na kwenda kwenye mtandao kuangalia mapicha mabovu wakiwa kazini, inasikitisha sana kwani watu wanapokea mishahara ya bure, na ndiyo maana hata kila kitu ni duni hata wafanyakazi kwa kuwa hawafanyi kazi hata haki zao hawazijui tena. sasa itakuwa haki ya kija mwenye akili mbovu.

    ReplyDelete
  7. it realy pains. Please the human rights associations should look on that guy

    ReplyDelete
  8. Polisi haihusu hapo sababu wazazi wake hawajampiga ama kumtesa kihivyo.. wazazi hawajapewa info na elimu ya kumtake care so na wao hawajui wafanye nini..

    Tatizo hapo ni serikali ndo inatakiwa iingilie kati kwenye mambo ya institution za watu wenye matatizo ya akili.. ustawi wa jamii unatakiwa upate funds za kutosha za kujiendeleza kusudi na wao wawaendeleze wananchi wanaotakiwa kujua kuhusu haya maswala na familia zenye watu wenye matatizo ya akili. Fikiria vitu kama DEPRESSION... huku majuu ukipiga simu hospitali wanakushughulikia haraka sababu inafika stage watu wanataka kujiua.. sasa ukipata depression Bongo unaenda wapi?
    Hivi ni vitu inabidi tuviongelee na vifanyiwe kazi..

    ReplyDelete
  9. unajua bwana na bibi serikali isivyowajali wananchi wake kuna waheshimiwa wamekaa ofisini wanakunywa chai wanaendeshwa kwenye mashangingi ni kosa kubwa sana kuwaABUSE wagonjwa wa akili.hivi sisi waafrika mbona wabinafsi?unapokuwa kiongozi masuala ya jamii ni muhimu sana ninauchungu ninaifanyia kazi hii picha nitaipeleka itv bbc na chanel5 usa na waalimu wa kuhusika na jamii kimataifa.HIVI WAZIRI ANAYEUSIKA NA JAMII YUPO AU ANATANUA TU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...