Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mdau AvoldMarch 19, 2011

    Kudadadeki! Hawa jamaa wakija Bongo wanajifanya wajuaji kumbe kwao HOHEHAE!

    ReplyDelete
  2. Kweli kama hii hali iko miji ya India, hakyanani kwenye miji yetu ya Tanzania nafuu! Duh, ila cha kushangaza wahindi wanawekeza Africa sana wakati wananchi wao ni masikini balaa!

    ReplyDelete
  3. Sasa hiyo kudadadadeki na wallahi mbona haviendani?. Msichanganye jina la mungu na "kudadeki" ambayo asili yake ni tusi. Please!.

    ReplyDelete
  4. jamani hapo pakistan sio india...lol!

    ReplyDelete
  5. Hizo plate number sio za India, hapo sipo ndugu yangu.hata mabasi India hamna kama hayo, mabasi yote ya uniform color...hapo sio India

    ReplyDelete
  6. hapo sio india
    afu msijindanganye kuwa miji ya bongo yana unafuu kuliko india.
    hawa jamaa miji yao imeenda shule, fly-over kila sehemu.
    barabara zao 95% mijini kuna lami...sasa compare na bongo
    na msisahau hawa jama wanatumia umeme wa nyukilia, sisi umeme wa manati. sasa comparison hapo iko wapi. ni sawa na kulinganisha, mbuzi na kuku

    ReplyDelete
  7. Mdau Bingo umenifurahisha sana, Wabongo wana dharau sana na India wakati uchumi wao hata kwa manati hawaingii ndani,Hao jamaa wako mbali sana msijidanganye...kwanza mi nimesafiri sana India na kaka Michuzi uwe unatafuta miji useme huo ni mji gani manake sijawahi kuona sehemu yeyote kama hiyo India, lakini mi naona pamefanana na Bangladesh..mabasi yao ya wahindi yako kama hivi... rangi yao nafikiri ni nyekundu tupu
    http://tinyurl.com/6b49v5a

    ReplyDelete
  8. Hello
    Mimi ni Mwanafunzi nasoma India nakaa Jammu and Kashmir North India,Ni kuzuri sana kuliko sehemu zingine,watu msidangayike India ni kama Bongo, i dont think that is india lakini mdau juu kapatia panaweza kuwa Pakistani...
    Linki ya Jammu na Kashmir on flicker http://www.flickr.com/photos/rangan-datta/4379494930/in/photostream/
    Mdau
    India

    ReplyDelete
  9. mimi ni mwanafunzi na niko mwaka wa 3 sasa huku india nimetembea maeneo km hyderabad,mysore,delhi,rajastan nk kwakweli waindi wanatumia sana usafiri wa bike na mara nyingi sana km unavyojua jamaa anawana sheria kabisa barabarani kwahiyo bike moja kukaa wa 5 au 7 so mbaya kwao pia pamoja na hayo mafly over india bado maskini sana hasa wanainchi wake ni bora hata bongo mtu ni maskini lakini analala lwenye kibanda cha mbavu za mbwa lkn india wanalala barabarani au slams za kufa mtu azifai yaani kwa bongo wanalala vichaa labda lkn huku ni suala la kawaida pamoja na kuwa na treni za umeme ni mara 10 ya bongo kwenye barabara ya vumbi

    ReplyDelete
  10. Mdau wa mwisho hapo juu nimependa maoni yako yenye full experience na picha ya India..ila kuna wadau waliotangulia wanabisha tu..eti India ni poooa...acheni kuchangia maoni km hamna experience yoyote juu ya jambo fulani!

    ReplyDelete
  11. Ndo mambo ya dunia ya tatu.

    ReplyDelete
  12. hapo sio india,..
    mie niko india mwaka wa tatu huu,,nimetembea sana na ni kweli umasikini upo,,ila asilimia kubwa watu wapo poa san,,hata siku moja tusilinganishe tanzania na india,,,mtambue kuwa hadi mataifa makubwa kama marekani na uingereza yaitegemea india katika sekta fulani muhimu,,uchumi wa asia umesimama CHINA NA INDIA.

    ReplyDelete
  13. heeee!!! mulioko india which is which?mbona kila mtu ana lake? mi india siijui ila ipo kwenye richest asian countries in world ranking na ni ya 12 lakini baadhi ya miji ukiiangalia hata huko Tanzania kuna afadhali ila India tajiri ni tajiri kweli na maskini ni wa kwelikweli.tofauti na kwetu wa hali ya kawaida ni wengi kuliko matajiri na mafukara

    ReplyDelete
  14. Wewe ambao uko Hyberbad 'maskini wako kila sehemu'na slums ziko hata Brazil Ndugu... na kuna sehemu ambao maskini wao katika hali mbaya zaidi lakini i dont think unaweza ku-compare Bongo na india na mimi nilifika tu kitambo

    ReplyDelete
  15. Jamani india Kunani?? Mkooooje? Weraa weraaa!!! Mnanikumbusha mbali mi nimesoma india nimemaliza juzi tu lakini msitake kutudanganya hapo sio india kabsaaaaaaaa! halafu kwa wadau walioweka link..Mbona nashindwa ku-copy na ku-paste hiyo linki? Kwanza india mjueni hivi, Kumegawanyika sana.. Kuna North india kwenda juu ni kuzuri tu lakini south ni kubaya kiasi fulani tho kuna sehemu nzuri sana India bongo hupati ng'o ni kama Ulaya kwenu, ...msijidanganye kwamba ni kama Bongo..ah ah..na hao watu wa india Wamegwanyika kwasababu wengine wanakaa kwa matajiri wengine wanakaa kwa maskini..Hyderbad of coz mna Slums nyie...nendeni mkasome miji ya bei...miji inatofautiana

    ReplyDelete
  16. Kweli nimeamini kwamba the Media is responsible for stereotypical information.. nilikuwa nawakasirikia western media wanavopiga picha Sudan sijui mashambulizi janjaweed na watoto wenye njaa halafu wanaleta huku @Ulaya wanasema 'This is Africa' kumbe hata nyinyi African Media mko hivi hivi? kaka Michuzi, hiii post ni bogus sana samahani kama nimekukosea kwa kusema hivo lakini, mtu akipiga picha Sudan na akaenda kusema ati 'this is is Tanzania' bila kufanya research eneo hilo ni eneo gani, mimi ningekasirika sana..sasa naona na wewe umefanya hivo hivo.. I dont know what image u r painting of India lakini kwa sisi ambao tumepapita na tumepaona Kuzuri kupo saaana tu na Kubaya kupo lakini hapafanani kabisa na Bongo...bongo barabara mbovu, umeme hamna,maji shida, majengo mazuri yanahesabika, mall ndo 'mlimani city' holiday areas Zanzibar, Tanzania Bado saaaana saaana hata nchi za Afrika zimetuzidi hatuwezi anza kujifananisha na nchi za Ki-Asia... unaweza kufananisha na india ambayo ni semi-continent? Uchumi stable, wanajenga kila kukicha ndani ya miaka mitano zinajengwa mall 100, magari wanajitengenezea wenyewe,na wanaendesha magari yao, wantumia vitu vyakao tu, they are the producing source of many manufacturing industries of the world, tena usitake nianze na movie zao LOL...hapana Ankal na wadau wake,Fanya Research kwanza hili ni tusi, hapo ni Pakistan

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...