Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Wakimsikiliza Mwenyekiti wa Mkutano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Bi Samia Suluhu Hassan
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Wakimsikiliza Mwenyekiti wa Mkutano Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Bi Samia Suluhu Hassan wakati wa kujadili Utatuzi wa Changamoto za muungano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Water Front jijini Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Bi. Samia Suluhu Hassan akifunguwa kikao cha Pamoja cha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujadili utatuzi wa Changamoto za masuala ya Muungano kulia Waziri wa Nchi Ofisiya Makamu wa Pili Zanzibar Bw Mahamed Abuod,katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili Serikali ya Mapinduzi Dk Khalid Salum Mohamed. Picha na mdau Ali Meja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Lini itakuwa zamu ya Serikali Ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kukutana na Tanganyika (aka Tanzania bara) baada ya kikao hiki na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar?

    ReplyDelete
  2. Mie nashangaa kutomuona mshiriki wa pili katika mazungumzo hayo naye ni Tanganyika!!!!!

    ReplyDelete
  3. huu muungano ufe. hebu oneni vituko hivo. makamu wa raisi mzanzibari, halafu waziri mwenye porfolio ya muungano ktk ofisi ya makamu wa raisi tena ni mzanzibari. teuzi za jk hizo, halafu wananchi tukilalamika mnasema eti udini. MUUNGANO UFEEE!!

    ReplyDelete
  4. Naungana nanyi kudai Tanganyika na kutaka MUUNGANO UFE. Tunakuombeni ndugu zetu wa Tanganyika mtuunge mkono sisi(Wazanzibari)tuwe na sauti moja ili haya yafanikiwe.SOTE TUMECHOKA NA MUUNGANO WA KINAFIKI.

    ReplyDelete
  5. jamani ndugu zetu wa tanganyika hebu andamaneni ndio watajua kuwa na nyie mnataka Tanganyika-hebu tuuwe huu muungano jamani tunasubiri nini-Unafiki mtupu-ulaya unaingiza bidhaa nchi zote 27 hulipi cent ya ushuru au ukilipa unaidai nchi yenu-hapo ukitoa kibegi tu kwenda bara mabegi yanapekuliwa-afadhali zanzibar unatoka huulizwi-TUMECHOKAA JAPO TUPO NJE YA NCHI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...