Na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Loliondo

Maelfu ya watu wanazidi kumiminika katika wilaya ya ngorongoro kata ya digodigo katika kijiji cha Samunge huku baadhi yao wakiwa mahututi sana na wengine Kupoteza maisha kutokana na msongamano wa watu na kuchelewa kupata huduma.

Wananchi hao ambao wametoka katika mikoa mbalimbali huku wengine wakitoka nchi za jirani ikiwemo nchi ya Kenya na Uganda wamemiminika katika kujiji hicho wengi wao wakiwa wanataka dawa kutoka kwa mchungaji mstaafu, Ambilikile Mwasapile, ambaye anatibu maradhi ambayo yanawasumbua kwa muda mrefu na ambayo walikuwa hawategemei kama wangekaa wapate dawa zake.

Pamoja ya kuwa watu wengi wanazidi kumiminika wilayani ngorongoro kupata matibabu kwenye nyumba ya mchungaji huyo lakini pia mamia ya watu wengine wamekwama jijini Arusha na katika eneo la Mto wa Mbu kutokana na kukosa usafiri wa kuweza kuwafikisha nyumbani kwa mchungaji Mwasapile huku wengine waliofika katika nyumba ya mchungaji huyo na kupata huduma wakiwa wanashindwa kurudi makwao kutokana na kukosa usafiri mara baada ya magari ambayo yaliwaleta kuondoka kutokana na kukaa muda mrefu.

Mbali na kuachwa na magari pia maelfu ya watu ambao wanaenda kupata matibabu wengi wao wamekuwa wakipata shida sana kwa ajili ya malazi na chakula kwani wanalazimika kulala kwa muda mrefu kutokana na wingi wa watu wanaowakuta hali inayowasababishia wananchi hao kukaa kwa muda hata wa siku tano na kuendelea na kulazimika kulala chini na wengine kupata chakula kwa njia ya shida sana hali ambayo inaleta hofu kubwa kwani watu wengi wanaofia magonjwa ya milipuko ambayo yanaweza tokea kuotokana na msongamano huo wawatu wengi .

Pia katika msongamano huo wa watu umeleata madhara kwani pia kuna baadhi ya wagonjwa ambao wameletwa wakiwa mahututi wamefariki kutokana na kuchelewa kupata huduma mapema na mpaka kufikia Juzi watu watu saba walikuwa wamefariki dunia akiwemo mtoto mmoja.

Mwandishi wa habari hizi mbali na kushuhudia maiti hizo bado aliwaona wagonjwa wengi ambao walikuwa wameletwa kupata huduma huku wengine wakiwa wanaonekana kufika sehemu hiyo wakiwa na dripu mikononi na wengine wakiwa hawajiwezi kabaisa.

Pamoja ya kuwa mchungaji Mwasapile alijitaidi sana kuhudumia wagonjwa ambao walifika sehemu hile lakini haikusaidia nahadi kufika jana jioni ilibidi waongeze wachungaji wengine wawili kumsaidi mchungaji huyu ili kuweza kupunguza watu kwani kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wagonjwa wanazidi kumiminika zaidi .

Mchungaji Mwasapile alipoongea na gazeti hili alisema kuwa analazimika kufanya kazi kwa muda mrefu ili kuweza kuwahudumia wagonjwa ambao wanafika hapo na pia alibainisha kuwa ameoteshwa kuwa watu watu bado wanaongezeka na wanatoka katika nchi mbalimbali na mabara mbalimbali hali ambayo itafikia mahali hata itamgarimu mtu kuchukua hata waki tano kupata huduma.

Mchungaji huyo alisema kuwa yeye mungu alinena naye kwa njia ya ndoto kuhusiana na dawa hiyo inayotokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula maarufu cha Twiga, tangu mwaka 1991 lakini alianza kutibu ugonjwa mmoja ambao ni wa ukimwi tu na ilipofika mwaka jana mungu alinena naye tena na ndipo alimwambia dawa hiyo inatibu pia hayo magonjwa mengine.

“na mungu aliponiotesha aliniambia kabisa na mtu ambaye nitaanza kumtibu na kweli alikuja mama mmoja wa hapa hawa kijijini na nikampa akapona baada ya mama huyo walikuja wanafunzi wawili pia niliwatibu nao wakapona na ndipo wakaanza kueneza na watu wakaja nikawapa na wamepona kabisa”alisema Mwasapile

Alisema kuwa dawa hii ainyeki mara mbili tiba yake ni mara moja tu na alisema kuwa kwa upande wa watu wenye ugonjwa wa HIV itanawatibu baada ya siku 21 ambapo alifafanunua kuwa akienda kupima mara ya kwanza ataonekana anavyo ,mara ya pili ataonekana anavyo yaani wiki ya pili na akienda wiki ya tatu ambayo itakuwa ni baada ya wiki 21 atakuwa hana kwa upande wawatu waenye kisukari alisema kuwa wao wanapona baada ya kunywa iyo dawa tu.

"Wanaopona HIV waache kujiingiza katika matendo ya kupata maambuki kwani hawatapona tena, Hii dawa sio kinga ni tiba na hairuhusiwi kunywa zaidi ya kikombe kimoja,"alisema Mchungaji Mwasapile.

Kwa upande wa msaidizi wa mchungaji huyo(Babuu), Marko Nedula alisema kuwa watu wengi wanaofika kupata huduma kwa mchungaji huyo wanatoka nje ya wilaya ya Ngorongoro pamoja na wengeji ambapo alifafanua kuwa awali wenyeji walikuwa wanazarahu dawa hiyo na kusema kuwa hawamuamini lakini baada ya kuona wageni wengi wanajitokeaa kunda kunywa ndio na wao wameanza kujitokeza kwa wingi.

Pia alisema kuwa anapenda kuwasihi watu ambao wanawaleta wagonjwa waho kujitaidi kuwaleta wagonjwa wakiwa angalau wananafuu kwa kiasi na wasiwachukuwe wagonjwa wao hospitali wakiwa mahututi kwani kwa sasa ivi msongamano wawatu umezidi hali ambayo inafanya kuchelewa kuwahudumia .

”unajua napenda kuwaambia wasiwachukuwe wagonjwa wao wakiw amahutiti kwani ndo inaweza kuwasababishia mathara ikiwemo wakiwaleta hapa wanaweza kuwapoteza kwani wakija wanakuta kunawagonjwa wengine wamekuja na niwagonjwa zaidi hadi huduma kuwafikia itachukuwa mda kitu ambacho kama alimchukuwa mgonjwa mahututi hospitalini anaweza kuupoteza maisha na kama wata wachukuwa basi wabebe dawa ambaozo zitawasaidia hadi pale mchungaji atakapo wafikia kuwapa huduma.

Pia gazeti hili lilibahatika kuzungumza na mmoja wa wanakijiji wa kijiji hicho aliyejulikana kwa jina la Ana Mateyo ambaye yeye alisema kuwa wamefurahia sana dawa hiyo kupatikana katika kijiji chao kwani wamekuwa wakifanya biashara kwa kasi kubwa mno na kusema kuwa wamekuwa wakipata hela kwani soda tu wamekuwa wakiuza shilingi 1000 huku maji ya kunywa wakiwa wanauza shilingi 2000.

Alisema kuwa pia wamefurahia sana kwani hata wao wenyewe kupitia babu huyo wanaweza kujikwamua katka maisha magumu kwani wanajiingizia kipata kila siku na wanafanya biashara kwa kiasi kikubwa sana.

Kwa upande wa mgonjwa mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Maramu Juma alisema kuwa yeye anafurahi sana kwani alifaika ngorongoro akiwa anaumwa na amebebwa lakini tangu anywe iyo dawa amesisimama mwenyewe na anatembea kitu ambacho amemshukuru mungu kwa kumleta mtumishi huyu katika nchi ya Tanzania.

Baadhi ya wagonjwa ambao waliohudhuria katika kujiji hicho waliomba jeshi la polisi mkoani Arusha kuongeza askari wa kutuliza gasia ambao wataweza kuwapanga watu na kuwaelekeza kufuata utaratibu uliowekwa ili kuweza kusaidia vurugu zisitokee.

Walisema kuwa mgambo ambao wapo katika eneo hilo hawawezi kutosha kutuliza vurugu hizo kwani jinsi siku zinavyozidi kwenda ndivyo wananchi wanavyozidi kuongezeka na wakija wale waliochelewa huleta fujo na kutaka kuanza kupewa dawa wao badala ya wale walio tangulia.

“tunaomba jeshi la polisi liongeze idadi ya askari waweze kusimamia utaratibu kwani muda mungine babu anashindwa fanya kazi kutokana na vurugu unakuta mtu amekuja hapa leo na kuna mungine kaja juzi yule wa leo ataki kufuata utaratibu uliowekwa analeta fujo kitu ambacho kinaleta ata uvunjifu wa amani “alisema mmoja wawagonjwa aliyejulikana kwa jina la Godfrey Lymo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. wenye dala dala arusha kwanini wasichukue hiyo njia, na wenye matent ndio wakati umefika wa kufanya biashara weka tent lako na watu wapate accomodation na wewe upate mshahara. mama ntilie nao huu ndio wakati wa kuanza biashara while there are waiting for treatiment

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kwamba mgonjwa yeyote pamoja na wanaomjali hujaribu kupata tiba yoyote na kwa namna yoyote ili kutibu gonjwa linalomsumbua mgonjwa na jamii yake. Hata kama uwezo wa tiba hiyo haijathibitishwa, bado itatumika tu. Desparation inaweza kumfikisha mtu mzima na akili zake katika situations za ajabu kama simulizi za huko Loliondo.

    Wiki mbili zimepita sasa tangu ndugu yangu mmoja yalipomkuta mikasa katika hospitali kubwa tu, Dar es Salaam. Katika hospitali ya kwanza alipewa rundo la mividonge baada ya kudundwa pia sindano nne za kuzuia maumivu na kutapika. Maabara wakasema iko malaria mbili.
    Ilipobidi kwenda kwingine baada ya mgonjwa kuzidiwa, na pale wataalamu wakafanya mavipimo yao na kugundua malaria moja pamoja na kitu ingine, ati labda utumbo umejikunja!!! Very contradictory. Hospitali ya tatu (in 36 hours) hata kabla ya kufanya vipimo wakataka kumdundika QUININE 9 based on lab report ya wengine! Baada ya kukataa hayo na kusisitiza vipimo kamili, mgonjwa akakutwa hana malaria hata chembe moja ila alihitaji kuongezewa maji mwilini, kwa maana ilikuwa case ya dehydration!!! Huduma mbovu kama hizi haziwezi kuwa pendeleo la mgonjwa yeyote. Na hii ndo hali halisi unless upo uwezo wa kwend kwa makaburu pale Trauma Centre.

    Ya Loliondo yawezekana kabisa kuwa siyo kipimo cha watu kujazwa UJINGA bali ni kile cha watu kukata tamaa na huduma mbovu katika nyanja mbalimabali.
    Rundo la watu wanaomiminika kwa matumaini kwenda Loliondo si tukio la kwaida hata kidogo. Nini mindset ya watu wote hao kufuata NENO tu?
    Je inawezekana ku-speculate kwamba ni matokeo ya kukata tamaa baada ya miaka 50 ya ubabaishaji wa mijizi ya MAFIA waliomo ndani ya CCM? Leo hii yule Babu mchungaji akiibukia kunadi sera za CDM kama dawa ya matatizo mengine ataitwa mhaini?

    ReplyDelete
  3. Ahsanteni kwa taarifa nzuri na uandishi mzuri. Mungu awabariki

    ReplyDelete
  4. I have been following this episode with great interest. I have what I would call a conventional medical background, to me you heal and you dont ask how.So if this muheshimiwa can heal I have no issues,I have no conflict,and I have no reason to disbelieve him.If we blindly disbelieve him we are no better than those who blindly believe in him.
    I only want a scientific proof of cure, ie pretreatment diagnosis and post treatment status.
    If he talks to God, no problem. for the prophets of the old talked to God, but for sure he cant be a prophet (Quraan 33:40)
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  5. kwa imani hakuna kisichowezekana....idadi kubwa ya watu inayozidi kumiminika LOLIONDO inathibitisha yaliyosemwa na manabii kuwa watu
    {sisi} tunaamini sana ktk miuzija kliko 'NENO LA MUNGU',yani kwa hali inavyozidi kubadilika tuwe makini yasije tokea yale ya KIBWETERE.....kwa sasa BABUUU!!! hata akiamua kuanzisha chama au dini yake atakuwa na wafuasi wengi sababu tu ya miujiza,japo c kila muujiza hutoka kwa Mungu tukumbuke kuwa hata Shetani anauwezo mkubwa sana wa kutenda miujiza na kuwavuta wengi...ni vema tusubiri uthibitisho wa kimaabara kabla ya ukurupuka kwa kupenda njia za mikatomikato.

    ReplyDelete
  6. Hivi ina maana hatuwezi kupata ushuhuda na uthibitisho toka maabara? Hamna watu ambao wametibiwa toka hiyo 1991 Babu aliyoanza kutibu?

    Na je hamna wagonjwa ambao walishapona wanaoweza kutoa ushuhuda hadi tusubiri maabara za wizara ya afya na NIMR? Ni kiasi gani mara hii serikali yetu kupitia wizara ya afya itakuwa serious kwenye hili na isichakachue majibu? Si ajabu wakatoa majibu ya utafiti mwingine kabisa badali ya ule waliotumwa kuufanyia kazi huko Loliondo.

    Kwa kifupi, siziamini kazi za serikali zinazohitaji umakini wa hali ya juu kama hili, so ningeshauri njia mbadala zitumike.

    Kama kuna wagonjwa wenye ushuhuda ni vizuri wakatumika kwani wana profile zao katika mahospitali mbalimbali nchini.

    ReplyDelete
  7. Oh! Asante mungu,asante sote tunaolitazama kwa umakini na pia kwa kusaidiana na uweza wetu wa kibinadamu.hali hii ni tete kwa taifa letu na hata watu wengine.Tupo katika wakati mgumu mno kimaisha ambapo tunapata mkanganyiko wa mambo mengi mno pamoja.Familia zetu au mtu yeyote yule, tusiposimama sawasawa kutoa muda wa kutafakari iwe kwa kutumia maandiko matakatifu, maarifa yetu, weledi na vipawa vingine hatuwezi kufika mbali.Nikiwa peke yangu na hata wakati mwingine najaribu kumshirikisha my wife au marafiki zangu na watu wengine kwamba yako mengi sana wakati wetu huu.taabu inakuja yote haya tunayapokeaje ili kuendelea kuishi bila fujo kichwani."Reality is very Complex." and indeed it is! Chonde tujitahidi kushikilia vichwa vyetu tumrudie Mungu kwa ibada za dhati, tumwombe mungu watalaamu wetu watupe tiba za kweli bila kuchoka wala kutaka rushwa, elimu yetu iwe bora na weledi utamalaki katika jamii yetu.Amina.

    ReplyDelete
  8. Ninachokiona hapa kinachomponya mtu ni imani. Watu wanakwenda kwa imani tu na pale wanapoombewa na kuamini kwamba dawa itaponya basi wanapona kwa imani, dawa ni sehemu ya kumfanya mtu aamini kwamba itamponya lakini kikubwa hapa ni imani. Tunaishi katika nyakati za mwisho kuna miujiza mingi itatokea ila tuwe macho ili imani yetu isije chakachuliwa!

    ReplyDelete
  9. wadau hebu fuatilieni na mpate ukweli wa haya matibabu. kama inawezekana onaneni na mtu aliyefika kwa huyo babu akanywa hiyo dawa na hatimaye akapona.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...