Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) Ananilea Nkya akiwaeleza wanachama wa chama hicho (hawapo pichani) kuhusu mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa 2010 wakati wa mkutano mkuu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mzuri Issa ambaye ni mratibu wa TAMWA Zanzibar na kushoto ni Gladness Munuo.
Gladness Munuo na Nasima Haji Chumu ambao ni wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakikata keki kwa niaba ya wenzao huku wanachama wengine wakishuhudia mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Nchini Tanzania (TAMWA) wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano uliopo kwenye ofisi za chama hicho huko Sinza Mori jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda -Maelezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. TAMWA imetoka mbali sana. Tungewasikiliza wale 'naysyers' miaka ile hasa midume iliyokuwa inatucheka tusingenda popote! TAMWA Juu, Juu, Juu, Zaidi na Zaidi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...